Daily Archives: April 2, 2020

WIZARA YA AFYA IMESEMA ZANZIBAR INA WATU WATANO WENYE MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

Wizara ya Afya imesema Zanzibar ina Watu watano wenye Maambukizi ya Virusi vya Corona na Watu wengine mia tatu na ishirini na nne wapo katika uangalizi maalum katika Kambi maalum ya Kidimni.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Waziri wa Wizara hiyo Mh.Hamad Rashid Mohammed amesema Wagonjwa hao ni Watanzania ambapo wamepata Maambukizi ya Virusi hivyo Nje ya Nchi.

Amesema kwa sasa Serikali imechukua hatua ya kuzifungia Baa na Kumbi za Starehe ili kuepusha athari zisiendelee kutokea hapa Nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk Jamala Taib amevitaka Vyombo vya Habari kuendelea kuelimisha Jamii juu ya kujikinga na Virusi vya Corona ili kuzuia Maambukizi.

 

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI WA TBC MARIN HASSAN MARIN AMEFARIKI DUNIA

 

Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC  Marin Hassan Marin amefariki Dunia.

Marehemu Marin amefariki leo Asubuhi katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es salaam.

Katika uhai wake Marehemu Marin aliwahi kufanya kazi iliyokuwa Televisheni Zanzibar (TVZ)  na Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ ) kabla ya kuhamia (TBC) hadi kufariki kwake.

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC amemueleza Marehemu Marin kuwa ni Kijana mbunifu aliyependa kujituma katika kazi zake.

Baadhi ya Wafanyakazi wa (ZBC) wamesema Marin hakuwa Mfanyakazi Mwenzao bali alikuwa ni Mwalimu aliyewaongoza vizuri kufanikisha Majukumu yao Kazini.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Awadhi Juma amemuelezea Marehemu Marini  jinsi alivyomfahamu

Marehemu Marin Alizaliwa Mwaka 1972 na miongoni mwa vipindi alivyowahi kufanya (TVZ ) na (STZ) ni pamoja na kutoka Afrika, Mawio, TVZ Doctor na Michezo ya Wiki.

TAASISI ZA UMMA ZIMESHAURIWA KUTENGENEZA MIKAKATI MAALUM KATIKA KUJIKINGA NA CORONA

Taasisi za Umma zimeshauriwa kutengeneza mikakati maalum  ili kuhakikisha Watu wote hawakai makundi katika kuendesha shughukli zao.

Akizungumza na ZBC Mkurungenzi kinga na Elimu ya Afya Dk Fadhil Mohamed Abdalla ofisini kwake Wizara ya afya amesema hali hiyo itawatoa wasiwasi Wafanyakazi wa Maofisini ili kufanya kazi zao kwa umakini.

Amesema mikakati hiyo ikitumika ipasavyo itaondoa matafaruku kwa baadhi ya Watendaji kuhusiana na maradhi ya Corona.

Akizungumzia kuhusu vitakasa Mikono yaani  Sanitaiza Dr .Fadhil amewatoa wasiwasi Wananchi wanaotumia kuwa ziko salama na hazina madhara kwa Watumiaji.

Akigusia suala la baadhi ya Vifaa vya Maofisini Dr .Fadhil amewataka Watumiaji wa Maofisini kutumia Dawa za vitakasa ili kusafishia vifaa vyao.

Baadhi ya Wananchi wameiomba Serikali kuendelewa kutoa Elimu zaid juu ya Elimu ya Maradhi ya Corona na kuahidi kufuata maelekezo yote yanayotolewa na Serikali.

 

error: Content is protected !!