Daily Archives: April 1, 2020

TANZANIA IMETANGAZA KIFO CHA KWANZA CHA MGONJWA WA COVID-19 MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

Tanzania imetangaza Kifo cha kwanza cha Mgonjwa wa covid-19 maambukizi ya Virusi vya CORONA kilichotokea katika Kituo cha matibabu ya Wagonjwa wa maradhi hayo huko Mloganzila Dar es salaam.

Taarifa iliyosainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu imeeleza kuwa Marehemu huyo ni Mtanzania Mwanaume mwenye umri wa miaka 49 aliyekuwa pia  anasumbuliwa na Maradhi mengine amefariki alfajiri ya tarehe 31.

Hadi kufikia sasa jumla ya Watu waliopata maambukizi ya Virusi vya CORONA imefikia 19 na mmjoa kati yao amepona maambukizi hayo.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR IMEPOKEA MSAADA WA VIFAA KWA AJILI YA KUPAMBANA NA MARADHI YA CORONA

Wizara ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya kupambana na Maradhi ya CORONA.

Vifaa hivyo vimetolewa na Mfanyabiashara Nd. Said Salima Bopar pamoja na  vikiwemo Vitanda, Magodoro, Vitakasa Mikono, Mashuka, pamoja na Friji la kuhifadhia Damu na Mashine ya uchunguzi wa Damu.

Waziri wa Afya Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema vifaa hivyo vimekuja wakati mufaka na vitasaidia katika kukabiliana na Maradhi kutokana na hali iliyovyo hivi sasa.

Amewataka Wananchi kutopuuza maagizo yanayotolewa na Serikali kwa kuacha kukaa kwa makundi hasa sehemu za Sokoni na sehemu nyengine za kutoa huduma ili kuepuka kuenea kwa maradhi yaCORONA .

Kwa upande wake Mfanyabisha huyo amesema ataendelea kutoa misaada yake kwa Wizara ya Afya katika kukabiliana na Maradhi mbali mbali ikiwemo ya Miripuko.

 

error: Content is protected !!