Monthly Archives: April 2020

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEENDELEA KUOKEA MICHANGO MBALI MBALI YA FEDHA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kupokea Michango mbali mbali ya Fedha Taslim jumla ya Shilingi Milioni Arubaini {70,000,000/-} zilizotolewa na Taasisi tofauti Nchini kwa ajili ya kusaidia nguvu za Serikali katika Mapambano yake dhidi ya kupiga vita kuenea kwa Virusi vya Corona Nchini.

Michango hiyo imetolewa na Uongozi wa Benki ya NMB iliyokabidhi Shilingi Milioni 30,000,000/-, Benki ya Maendeleo Vijijini {CRDB} Shilingi Milioni 30,000,000/- pamoja na Uongozi wa Bodi ya Uhaulishaji wa Ardhi Zanzibar Shilingi Milioni 10,000,000/-.

Akipokea Michango hiyo hapo Afisini kwake Vuga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mashirika na Taasisi zinazotoa huduma kwa Jamii zikiwemo zile za Kifedha zinapaswa kuendelea kuwahamasisha Wananchi katika kuzingatia njia zinazopaswa kutumiwa katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.

Alisema Serikali Kuu kwa upande wake inajitahidi kutumia nguvu zake kubwa katika juhudi za kutoa elimu ili kuona ufahamu wa kutambua hatari ya kuyaepuka maradhi yanayosababishwa na Vizuri hivyo unamfikia kila Mwananchi mahali popote alipo Mijini na Vijijini.

Alisema Mashirika na Taasisi hizo kwa vile zimekuwa zikitoa huduma kila siku kwa kundi kubwa la Jamii. Hivyo  ni vyema wakaitumia fursa hiyo kuendelea kutioa elimu hata kwa kutumia vipeperushi vitakavyosaidia utoaji wa Elimu ya kujiepusha na Maradhi hayo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Taasisi na Mashirika hayo kwa michango inayoendelea kutoa na kuwahakikishia kwamba itatumiwa kwa utafutaji wa Vifaa na zana zitakazosaidia mapambano dhidi ya kudhitibi kuenea kwa Virusi vya Corona.

Mapema Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Nd. Abdullah Duchi alisema mchango wa Taasisi yao ya Kifedha tayari umeshaingizwa kwenye Akaunti Maalum iliyoanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya Virusi vya Corona Nchini.

Alisema Uongozi wa Benki ya NMB umeguswa na tukio hilo lililoikumba Tanzania na Dunia kwa ujumla ambapo wanapaswa kuingiza nguvu zake katika kuona mapambano hayo yanafanikiwa vyema.

Naye Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania Dr. Joseph Vicent Taasisi hiyo ya kifedha Nchini imejitolea kushiriki kwenye Mapambano dhidi ya Virusi hivyo tokea kuibuka kwake kwa mara ya kwanza Nchini Tanzania huko Mkoani Kilimanjaro.

Dr. Joseph alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Uongozi wa Taasisi hiyo umedhamiria kusaidiana na Serikali zote mbili katika kuona ustawi wa Wananchi wote ambao ndio Mtaji mkubwa wa kazi zao kwa kuongeza Mapato unaendelea kuimarika vyema.

Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa Bodi ua Uhaulishaji  wa Ardhi Zanzibar Bwana Enzi Talib Aboud alisema Uongozi wa Bodi hiyo umeguswa na janga hilo pamoja na kufanya vyema katika majukumu yake ya kila siku ya ushughulikiaji na ufuatiliaji wa masuala ya Ardhi lakini umelazimika kushirikiana na Taasisi nyengine Nchini katika kuungana na Serikali kwenye mapambano hayo.

Bwana Enzi alisema mapambano dhidi ya Virusi vya Corona {COVIC – 19} yanapaswa kushirikisha kila Taasisi, Mashirika ya Umma, yale ya Kimataifa na hata Jamii ili kuiona Zanzibar na Tanzania kwa ujumla inabakia salama.

Alisema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikijumuisha Bara na Zanzibar bado inaendelea kuwa na unafuu wa kukumbwa na janga hilo la Virusi vya Corona ikilinganishwa na Mataifa mengine Duniani yakiwemo pia hata yake jirani ya Afrika Mashariki.

 

 

 

 

WIZARA YA AFYA IMETANGAZA ONGEZEKO LA WAGONJWA SABA WALIOAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA

Wizara ya Afya imetangaza ongezeko la Wagonjwa saba walioambukizwa Virusi vya CORONA na kufikisha idadi ya Wagonjwa mia moja na tano huku wengine 36 wameripotiwa kuopona na kuruhusiwa kurudi Nyumbani.

Katika Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed  imeeleza kuwa Wagonjwa wote wapya ni Raia wa Tanzania wanaotokea Unguja.

Amefahamisha kuwa Wagonjwa walioruhusiwa wamatakiwa kubaki nyumbani kwa siku kumi nne huku wakiendelea kufautiliwa kwa karibu na Wataalamu wa Afya kabla ya kurudi katika shughuli zao za kawaida.

Aidha Wizara hiyo imeendelea kuwasititiza Wananchi kuchukuwa tahadhari zote za kujiknga na Ugonjwa wa covid 19 hasa katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  pamoja na kuwaomba Wananchi wanaojihisi kuwa na dalili za Ugonjwa huo kuripoti kwa wWtaalamu wa Afya ili kufanyiwa uUhunguzi zaidi.

 

JAJI MKUU MSTAAFU WA TANZANIA AUGUSTINO RAMADHAN AMEFARIKI DUNIA

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhan amefariki Dunia katika Hospitali ya Agha Khan Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika uhai wake Marehemu Jaji Ramadhan aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu

Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za Rambirambi kwa Jaji mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Khamis Juma Familia ya Marehemu na Waumini wa Kanisa la Anglikana kufuatia kifo cha Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani

Rais Magufuli amesema Marehemu Augustino Ramadhani atakumbukwa kwa Utumishi uliotukuka kwa Nchi yake kutokana na alikuwa mtu mkweli mchapakazi Mzalendo na Mcha Mungu.

Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya Marehemu Augoustino Ramadhani mahali pema Peponi, Amina

MICHE ELFU SABA AINA YA MIKESHIA IMEPANDWA KATIKA MAENEO YALIOATHIRIKA KWA UCHIMBAJI WA MCHANGA

Zaidi ya miche  Elfu Saba aina ya Mikeshia imepandwa katika maeneo yalioathirika kwa uchimbaji wa Mchanga kiholela huko  kiongele Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja ili yaweze kurudi katika haliyake ya kawaida.

Zoezi hilo limefanywa na Idara ya Misitu na maliasili zisizorejesheka kwa kushirikiana na Wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza mara baada ya upandaji Miti katika eneo la Kiongele Mkurugenzi Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Nd: Sudi Mohamed Juma amesema wameamua kuanza na Wilaya ya Kaskazini “A” kutokana na kukithiri kwa uharibifu huo na tayari wameshapanda zaidi ya hekari tisa katika Wilaya hiyo.

Afisa msimamizi wa Sheria Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Nd: Haji wa Haji Hassan amewaambia Wananchi wanaopandiwa Miti katika maeneo yao kuithamini Miti hiyo kwa kuitunza kwani Miti hiyo itawasaidia katika harakati zao ya Kimaendeleo.

Kwa upande wa Wananchi walioshiriki zoezi hilo wamesema upandaji wa Miti hiyo utawasaidia katika kutunza Mazingira hivyo wameahidi kuilinda .

error: Content is protected !!