Daily Archives: March 30, 2020

DKT SHEIN AMEONGOZA WANANCHI NA VIONGOZI KATIKA MAZISHI YA WAZIRI KIONGOZI WA KWANZA WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameongoza Mamia ya Wananchi, Viongozi  wa Serikali  na  Vyama vya Siasa  katika Mazishi ya aliyekuwa Waziri Kiongozi wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Ramadhan Haji Faki yaliyofanyika Kijijini kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Marehemu amesaliwa katika Msikiti Mkuu wa Mwembeshauri na Sala kuongozwa na  Mufti Mkuu wa Zanzibar.

Nd. Ramadhan Haji Faki  amezaliwa mwaka 1930  na amefariki jana Jijini Dar es salaam akiwa na umri wa miaka 99

Marehemu Faki ambae alikuwa Mjumbe wa Kamati ya watu 14 ya Chama cha ASP iliyoongoza Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 alishika wadhifa wa Waziri Kiongozi Mwaka 1983 hadi 1984.

Katika uhai wake Marehemu Faki alitumikia Jeshi la polisi kwa muda wa miaka 14 akipitia vyeo mbali mbali na mwaka 1966 alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania na kutunukiwa vyeo kuanzia Kapteni hadi Brigedia Jeneral na pia alishiriki Vita vya Kagera.

Kabla ya kuwa Waziri Kiongozi mwaka 1980 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Baraza la Mapinduzi na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi mwaka 1964 hadi 1984.

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohamed Aboud ameongoza ujumbe wa Serikali kutoa Rambi rambi  kwa  Familia ya Marehemu.

MHE NADIR YUSSUF AMEWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA KUJIKINGA NA UGONJWA WA KORONA

Mwakilishi wa Jimbo la Chaan Mhe. Nadir Abdullatif Yussuf amewataka Wananchi kuchukua tahadhari katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.

Akizungumza na Masheha na Wakaazi wa Jimbo hilo  amesema  kila mtu anapaswa kuwa makini na kusikiliza taarifa za Serikali zinazoelekeza juu ya kujikinga na Maradhi hayo.

Nao Wakaazi hao na Masheha wamempongeza Mwakilishi huyo kwa kushirikiana nao katika kupambana na janga hilo na wameahidi kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali.

Mwakilishi huyo amekabidhi vifaa vya kunawia mikono na Sabuni kwa Wakaazi wa Jimbo hilo.

error: Content is protected !!