Daily Archives: March 29, 2020

JUMLA YA WAGONJWA WATATU WA WAATHIRIKA WA VIRUSI VYA CORONA IMEFIKIA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Mhe:Hamad Rashid Mohammed amesema kila Mwananchi anapaswa kuchukua tahadhari zaidi ya Kujikinga na kuwakinga wengine juu ya maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akitoa Taarifa juu ya kuongezeka kwa Mgonjwa mwengine na idadi ya waliombukizwa Zanzibar kufikia Watu Watatu amesema iwapo mtu yeyote hatokuwa  na  hadhari  ya  kuenea  kwa  Virusi  hivi  anaweza  kusababisha  janga kubwa kwa Taifa.

 

WANANCHI WAMETAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA UGONJWA WA VIRUSI VYA CORONA

Uongozi katika  Jimbo  la  Tunguu  umeanzisha  kampeni  maalum  ya  kuwahamasisha  Wananchi   juu  ya  namna  bora  za  kujikinga  na  Maambukizi  ya  Ugonjwa  wa  Corona.

Kampeni  hiyo  ilioambatana  na  ugawjai  wa  Ndoo  na  Sabuni  kwa  Wananchi  wa  Maeneo  mbali  mbali  katika  Jimbo  hilo   imeendeshwa  na  Mwakilishi  wa  Jimbo  hilo  Mh.Simai  Mohamed  Said   ambapo  amewasisitiza   kuchukuwa  tahadhari  ya  hali ya  juu  kwani  Ugonjwa  huo  sio  wa   kuufanyia  mzaha.

Amewashauri  Wananchi   kuendelea  kuelimishana  na   kukumbushana  mara  kwa  mara  umuhimu  wa  kunawa  mikono  na  kuepuka  mikusanyiko  isio  ya lazima  wakati  huu  Ugonjwa  huo  ukiendeleza  kukatisha  uhai  wa  watu  wengi  katika  Nchi  tofauti.

Baadhi  ya  Wananchi  walioshiriki  Kampeni  hiyo  wameiomba  Serikali  kuwachukulia  hatua  baadhi  ya Wafanya  Biashara  wanaopandisha  Bei  za  Vyakula  na   Vifaa  pamoja  na  Dawa  Maalum  za  kutakasa  Mikono    .

Wakati  huo  huo  Mh.Simai  ambae  pia  ni  Naibu  Waziri wa  Elimu  na  Mafunzo  ya  Amali  amekabidh   Kitanda  cha  Kulazia Wagonjwa  katika  Kituo  cha  kuhudumia  Watu  waliopatwa  na  Ugonjwa  wa  Corona  Kidimni  ambapo  Meneja  Msaidizi  wa  Kituo  hicho  Nd.Suleiman  Mohamed  amesema  juhudi  za  ziada  zinahitajika   kwani  ugonjwa  huo  ni  hatari.

 

WAKAAZI WA MTAA WA KIMARA BARUTI KATIKA MANISPAA YA UBUNGO WANAKABILIWA NA TATIZO LA DARAJA

Zaidi ya Wakaazi Elfu Moja wa Kimara Baruti katika Manispaa ya Ubungo Jijini   Dar es salaam wanakabiliwa na tatizo la Daraja katika Mto Gide unaounganisha na kata ya Makoka.

Wakizungumza na ZBC  Jijini Dar es salaam baadhi ya Wananchi hao wamesema ukosefu wa Daraja katika eneo hilo umesababisha  baadhi ya Watu ikiwemo Watoto Wadogo  kupoteza  maisha  wakati  wakitaka  kuvuka  katika  Mto huo pindi wanapokuwa Wanaenda Shule.

 

Pascal Manota  ni  Diwani wa Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam ambapo amesema kutoka na kadhia hiyo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na Wakala wa  Barabara   Nchini (Tarura) wametenga kiasi cha Shilingi Milioni 321 kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja katika Eneo hilo.

 

Nae Mkurugenzi wa Kampuni wa Mpe 2000 Limited ambao ni Wakandarasi wa Ujenzi wa Daraja hilo Bi Nevablack Mwangori amewahakikishia Wananchi kutekeleza Mradi huo kwa Mujibu wa Mkataba.

 

Ikumbukwe kuwa Ujenzi wa Daraja hilo ni Sehemu ya Mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania na ile ya Awamu ya Saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutatua changamoto zinazowakabiliwa Wananchi katika Maeneo yao.

 

error: Content is protected !!