Daily Archives: March 28, 2020

WANANCHI WANAOKWENDA KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA KUFUATA TARATIBU UNAOTOLEWA NA MADAKTARI

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Mjini Bi Marina Joel  Thomas  amewataka  Wananchi  wanaokwenda  kuangalia  Wagonjwa  katika  Hospitali  ya  Mnazi mmoja  kufata  utaratibu  unaotolewa  na  Madaktari  wa  kutokuwepo  kwa  mkusanyiko  katika  maeneo  ya  Hospitali  hiyo .

Akizungumza  mara  baada  ya  kumalizika  kwa  uangalizi  wa  Hospitali  hiyo   amesema   kuwa  atahakikisha  anatoa  Elimu  ya kutosha  kwa  Watu  wanaokwenda  kuangalia  Wagonjwa  wao  na kuondosha  Mkusanyiko   katika maeneo  hayo  hali  ambayo  ni  hatarishi  katika  Jamii  kiujumla

Aidha Bi Marina  amewataka   Madaktari  hao  kuendelea  kutoa  Elimu  kwa  Wananchi  hao  juu  ya  suala  zima  la  kujikinga  na  Maradhi  ya CORONA  kwani kufanya  hivyo  kunaweza  kuondokana  na  Maradhi  hayo  katika  maeneo  mbalimbali .

Mkurugenzi  Utawala  na  Uwendeshaji  Hospitali  ya  Mnazimmoja  Dkt.  Abubakar  Khamis  Hamadi  amesema   kuwa  licha  ya  kufanya  jitihada  ya  kutoa  Elimu  kwa  Wananchi  lakini   bado  inaonekana  Wananchi  hao  wamekuwa  wakaidi  na  kutoskiliza  ushauri  kutoka  kwa  Madaktari   hao.

Hata hivyo   Dkt.  huyo  ameiomba  Serikali  ya  Mapinduzi  ya  Zanzibar  kushirikiana  katika  suala  la  kuhakikisha  wanaondosha  mikusanyiko  mbalimbali  ambayo  kwa  sasa  imekuwa  ni  hatarishi  na  huweza  kuleta  Madhara  makubwa  katika  Jamii .

JUMUIYA YA WASTAAFU NA WAZEE ZANZIBAR KUTOA ELIMU JUU YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA

Wajumbe wa Kamati tendaji wa Jumuiya ya Wastaafu na Wazee Zanzibar (JUWAZA) wanakusudia kuzunguka kila Sheiha za jimbo la Kiembe Samaki ili kutoa Elimu juu ya kujikinga na Virusi vya CORONA hasa kwa Wazee.

Wakizungumza Wajumbe hao Nd. Fatuma Sukina na Nd.Amour Haji  wamesema lengo la kutoa Elimu hiyo kwa Wazee hasa Wazee wenye umri wa miaka 60 ni kuwapa Taadhari ya kujinga na Ugonjwa huo na kuwaelimisha jinsi ya kujinga ili kukwepa janga hilo ambalo limekumba Dunia.

Wamesema Vijana waliowengi wanachukulia kuwa Ugonjwa huu ni wa kawaida bila kuchukua taadhari yoyote na wanapaswa kusikiliza maagizo yanayotolewa na Serikali na kuyafanyia kazi ipasavyo.

Aidha baadhi ya Waratibu wa Jimbo hilo wamesema wataendelea kuunga mkono Serikali katika kutoa Elimu kwa Jamii ili Wananchi kwa ujumla waweze kupata Elimu dhidi ya kujikinga na Maradhi hayo.

error: Content is protected !!