Daily Archives: March 24, 2020

OFISI YA MUFTI ZANZIBAR IMEWAAGIZA WAUMINI KUTODHARAU MAAGIZO YANAYOTOLEWA NA WIZARA YA AFYA

Ofisi ya Mufti Zanzibar imewaagiza Waumini kuzingatia na Kutodharau Maagizo yanayotolewa na Wizara ya Afya juu ya Kujilinda na Maradhi yaCORONA.

Tamko hili limetolewa na Katibu wa Mufti Zanzibar Nd. khalid Ali Makame wakati akizungumza na ZBC kufuatia kwa baadhi ya Waumini kuonekana wanapuuza Maagizo yaliyotolewa na Wizara hiyo na kuendelea kupeana Mikono mara wanapomaliza kufanya Ibada.

Aidha Sheh Khalid amesema  Masheha  wananafasi kubwa ya kujua  yanayofanyika katika Shehia zao hivyo si vyema kuona  watu wanakiuka  kauli za Serekali  na kuzipuuza.

Hata hivyo amesema kutokana na Takwimu zinazo Ripotiwa kila siku juu ya Maradhi ya CORONA ni lazima kuwa na tahadhari juu ya Ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani liaeleza kuwa  Maradhi ya CORONA yanendelea kuongezeka katika  Nchi mabali mbali Duniani ambapo Virusi hivyo vinaweza kukaa kwa  muda wa Masaa Manane bila ya Kufa.

WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI KATIKA KIPINDI HICHI CHA MVUA ZA MASIKA ZILIZOANZA KUJIKINGA NA MARADHI

Mamalaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Zanzibar  imewaomba Wananchi kuchukuwa Tahadhari katika kipindi hichi cha Mvua za Masika zilizoanza kujikinga na Maradhi mbali mbali yakiwemo ya  Virusi vya CORONA

Mkuu wa shughuli za Hali ya hewa Zanzibar Nd. Hafidh Juma amesema taarifa za Afya zinaeleza kuwa Virusi vinavyosababisha Maradhi yaCORONA vinasambaa zaidi katika mazingira ya majimaji na baridi ambayo katika msimu huo ndio wakati wake.

Akizungumza na ZBC amesema miongoni mwa tahadhari zinazohitajika kuchukuliwa ni pamoja na kuweka mazingira safi katika makaazi yao hasa kwa kuondosha sehemu zinazotuama maji na kufuatailia taarifa za hali ya hewa mara kwa mara.

Akizungumzia kuhusiana na siku ya Hali ya Hewa Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Marchi 23 amesema Sherehe hizo zimeamuliwa kuahirishwa ili kuungana na agizo la serikali na amewasisitiza wananchi kuchukuwa tahadhari kwani utabiri unaonesha Mvua za Masika zitakuwa kwa kiwango kikubwa.

Amesema Mamlaka hiyo itaendelea kutoa Elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa kulinda Afya zao hasa katika matumizi ya Maji safi inayoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku hiyo inayosema Hali ya Hewa na Maji.

BARAZA LA MAASKOFU ZANZIBAR LIMEWAHIMIZA WAUMINI KUFUATA MAAGIZO YANAYOTOLEWA NA SERIKALI

Baraza la Maaskofu Zanzibar limewahimiza Waumini wa Kikristo na Wananchi kuzingatia Tahadahri na maagizo yanayotolewa na Serikali juu ya Ugonjwa wa CORONA ili kuepukana naVirusi hivyo.

Katibu  wa Baraza  hilo  Askofu Dickson Kaganga  ametowa  tamko  hilio katika  ibada  maalum  ya  maombi    ya  pamoja  kwa  Makanisa  yote   ya  kuiombea Nchi  kuepukana  na  Virusi  vya  CORONA ibada iliofanyika   katika kanisa la Kiinjli   la Kilutheri  Tanzania (KKKT) lililopo Mwanakwerekwe.

Amesema Wananchi  wote   wanapaswa kuchukua tahadhari kwa kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima na kutekeleza maagizo yanayotolewa na Watalaam  wa Afya na kuepuka  kupokea taarifa za uongo zinazosambaa katika Mitandao ya Kijamii.

Askofu  kagaanga  amewasihi  waumini  na  Wanachi  kuishi  maisha  yanayo mpendeza  Mungu  na  kumcha  Mungu  ili  kuifanya  Dunia  kuwa  mahala  salama  pa  kuishi  na  kuwa  mbali  na  Majanga  na  Maradhi.

Baadhi ya Wachungaji walioshiriki katika Maombi hayo wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuruhusu Ibada za Jumapili na kufanya Maombi juu ya tishio la Ugonjwa wa CORONA uliyopo Duniani ili kumuomba Mwenyezi Mungu kuondoa janga hilo.

Kwa mjibu wa Takwimu  tayari Ugonjwa wa homa ya CORONA  umewakumba watu zaidi ya laki mbili na elfu 60 katika Nchi zaidi ya 160 Duniani na hadi sasa kiasi watu elfu 11 wamepoteza maisha.

error: Content is protected !!