Daily Archives: March 23, 2020

JUMLA YA WAGONJWA 12 WAMETHIBITISHWA KUAMBUKIZWA NA UGONJWA WA CORONA NCHINI TANZANIA HADI SASA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Wasafiri wanaotoka katika Nchi zenye Maambukizi ya Virusi vya Corona wanaokuja Tanzania watawekwa katika Karantini ya Siku 14 kwa gharama zao wenyewe.

Akilihutubia Taifa amesema hadi sasa Wagonjwa 12 wamethibitika kuambukizwa na Ugonjwa huo wakiwemo Raia wa Kigeni na Watanzania.

Rais Magufuli amefahamisha kuwa Wagonjwa wote wanaendelea vizuri na hadi sasa hakuna Kifo na vipimo 20 vya leo vilivyochukuliwa hakuna Mtu aliyekutwa na Maambukizi ambapo pia Mgonjwa wa kwanza aliyeripotiwa kupata Ugonjwa wa Corona   Tanzania ameshapona.

Kwa mujibu wa Takwimu tayari Ugonjwa wa Homa ya Corona umewakumba  Watu zaidi ya Laki Mbili na Elfu 60 katika Nchi zaidi ya 160 Duniani,  na hadi sasa kiasi Watu elfu 11, wamepoteza maisha.

 

DK.MAGUFULI AMEWATAKA WATANZANIA KUPUNGUZA HOFU JUU YA JANGA LA UGONJWA WA HOMA YA CORONA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Amewataka Watanzania kupunguza hofu juu ya Janga la Ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona na badala yake waendelee kufanya kazi na kujenga Uchumi kwa kuzingatia tahadhari zote za kujikinga.

Rais Magufuli ameeleza hayo katika Salamu zake za Ibada ya Jumapili Mjini Dodoma ambapo amesema kuwepo kwa Ugonjwa wa Corona isiwe sababu ya kutishana kiasi cha kumsahau Mwenyezi Mungu, na kutoa Wito kwa Watanzania wote Kumuomba Mwenyezi Mungu ili aliepusha Janga hili.

Rais Magufuli amekemea tabia za baadhi ya Watu wanaofanya Mzaha juu ya Ugonjwa huu ama kuwatia hofu Wananchi kupitia Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii, na badala yake ametaka Watanzania waendelee kuchapa kazi huku wakingatia tahadhari zinazotolewa na Wataalamu.

Aidha amewashukuru Viongozi wa Dini kwa kuungana na Serikali katika kuwahamasisha Wananchi kuchukua tahadhari na ametoa Wito kwa Viongozi hao kuendelea kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aepushe Janga hili la Corona.

 

IDARA YA MISITU NA MALIASILI ZISZOREJESHEKA IMETAIFISHA MCHANGA ZAIDI YA TANI 300

Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka imetaifisha Mchanga zaidi ya Tani 300 unaosadikiwa kuchimbwa kinyume cha utaratibu.

Akizungumza katika zoezi hilo Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Ndugu Sudi Mohammed Juma amesema Mchanga huo umekamatwa Maeneo ya Shehia ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini a ambao umekusanywa kwa kutumia Gari za Ng'ombe.

Amesema Serikali imepanga Maeneo Maalum kwa Uchimbaji wa Mchanga kwa ajili ya utunzaji wa Mazingira lakini bado kuna baadhi ya Wananchi  Wanachimba Mchanga kiholela jambo ambalo linaweza kusababisha hatarishi ya kimazingira hivyo amewaonya watakaokamatwa watachukuliwa hatua na kuwataka Viongozi na Masheha kutoa Ushirikiano ili kukabiliana na tatizo hill.

Afisa Usimamizi wa Sheria wa Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Ndugu Haji wa Haji Hassan amesema ni kosa kuchimba Mchanga sehemu zisizoruhusiwa na Idara tayari imeshajipanga kufanya Doria kukamata Gari za Ng'ombe zitakazokutwa na Mchanga.

Maeneo ya kiengele na Kivunge Wilaya ya Kaskazin a ni yaloyokithiri kwa Uchimbaji Mchanga Kiholela.

 

error: Content is protected !!