Daily Archives: March 21, 2020

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEZUIA NDEGE ZOTE KUTOKA NJE YA NCHI KUINGIA NCHINI

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imezuia Ndege zote kutoka Nje ya Nchi kuja Visiwani humu ikiwa ni hatua za kuzuia maambukizo ya maradhi ya Corona.

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mh.Mahmoud Thabit  Kombo amesema hayo leo katika Ziara ya kutembelea eneo maalum lililotengwa kwa waathirika wa Ugonjwa huo huko Kidimni ambapo pia ameionya Jamii kuacha tabia ya kueneza Habari zisizo sahihi za Ugonjwa huo.

Nae Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dokta Fadhil Mohamed Abdalla amesisitiza kuwa hadi sasa Zanzibar ina Mgonjwa mmoja tu wa matatizo hayo, na pia ameitaka Jamii kufuata utaratibu unaowekwa katika kujilinda na maambukizi ya Ugonjwa huo.

error: Content is protected !!