Daily Archives: March 10, 2020

VIKUNDI VYA USHIRIKA KWA WANAFUNZI WANAOHITIMU VYUO VYA MAFUNZO YA AMALI KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati Mhe.Juma Makungu Juma amesema kuanzisha Vikundi vya Ushirika kwa Wanafunzi wanaohitimu Vyuo vya Mafunzo ya Amali kutawasaidia kupunguza tatizo la Ajira kwa Vijana.

Akiwatunuku Vyeti Wahitimu katika Mahafali ya Saba ya Kituo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Naibu huyo Waziri amesema Serikali imetenga Pesa za Mikopo kwa Wahitimu wa Mafunzo hayo hivyo ni vyema kuitumia Fursa hiyo kwa kuunda Vikundi vya Ushirika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vyuo vya Mafunzo ya Amali Bakari Ali Silima amesema majukumu ya mamlaka ya Mafunzo ya Amali ni kusimamia lengo la Serikali la kuimarisha Mafunzo ya Amali Nchini ambapo imeweza kuwasomesha Ualimu ngazi ya Diploma Walimu wa Vyuo vya Amali.

Wahitimu hao wamesema ingawa Kituo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni kinatoa Elimu bora lakini Wanafunzi wanakabiliwa na matatizo ya uchache wa Dakhalia na Kituo cha Afya.

ELIMU ZAID INAHITAJIKA KUUWAHAMASISHA AKINA MAMA JUU YA SUALA LA KUJIFUNGULIA HOSPITALINI.

Elimu zaid inahitajika kuuwahamasisha akina Mama juu ya suala la kujifungulia Hospitalini ili kunusuru Vifo vitokanavyo na Uzazi.

Akizungumza katika zoezi la Usafi wa Mazingira Hospitali ya Kivunge lilianadaliwa na kikundi cha uzalishaji wa Umeme wa Jua na Ushonaji (Beafoot) ikiwa ni kuazimisha siku Wanawake Duniani Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kazi uwezeshaji Wazeee Wanawake na Watoto anaeshuhulikia masuala ya uwezeshaji Nd. Mauwa Makame Rajab amesema bado kuna baadhi ya Wanajamii hawana uelewa juu ya umuhimu wa kujifungulia Hopitalini.

Daktari dhamana wa Hospitali ya kivunge Dr.Tamimu Hamadi Saidi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja Nd.Hassan Mcha Hassan wamesema ni vyema kwa Wanavikundi wengine kuiga mfano wa Wajasiriamali wa uzalishaji wa Umeme wa Jua na Ushonaji cha  (Beafoot) cha Kinyasini kwa kushiriki shughuli mbali mbali za Kitaifa.

Meneja wa (Beafoot) Nd.Pendo Yaled Daud amesema Usafi ni njia kuu moja wapo ya kumueka katika hali ya usalama Mgongwa na kumfanya apone haraka.

MAKADHI WAMETAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA USAJILI.

Makadhi  na  Mashekh  wanaosimamia  usajili  wa  Ndoa  na  Talaka  katika Mkoa wa  Kusini  wametakiwa  kufanya  kazi  zao  kwa  kufuata  Sheria  na  taratibu  za usajili zinavyowaelekeza  ili  kuepuka  matatizo  mbali  mbali  yanayoweza  kujitokeza  katika Jamii.

Akizungumza kwa niaba  ya Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mkuu wa Wila  ya Kusini   Bwana  Iddrissa Kitwana  Mustafa  wakati akifungua mafunzo  elekezi  kwa  Mashekh  na Makadhi   juu ya utaratibu wa  usimamizi   wa ujazaji  wa Madaftari  ya  uasjili   wa  Ndoa  na  Talaka  huko Tunguu.

Amesema    hatua  hiyo  ya kufuata  Sheria  na  Taratibu  za usajili   itaiwezesha  Serekali  kupata kujua  idadi  sahihi   ya  Wajane  na wenye Ndoa   na kuweza  kupanga   vyema  mipango ya maendeleo   hivyo ni vyema  wakawa  makini   ili kuona kwamba  lengo  lilikusudiwa  linafikiwa .

Nae  Naibu  Mkurugenzi  wa  Wakala wa  Usajili  wa  Vizazi ,Vifo ,Ndoa,na Talaka  Nd. Shaban Ramadhan  Abdalla  amesema  lengo  la kutolewa  mafunzo  hayo  ni kuwajengea  uwezo  wasimamzi  hao ili  waweze  kufanya  Kazi zao  kwa  ufanisi .

Nao  Mashekh  hao na Makadhi  wameishukuri  Idara  hiyo kwa kuwapatia  Mafunzo  hayo  kwani  wataweza   kufanya kazi zao  kwa uhakika  na kuepuka  na  kasoro mbali mbali ambazo  zilikua zikijitokeza .

Katika  mafunzo hayo mada mbili ziliwasilishwa  ikiwemo  utaratibu  na usimamizi  wa  ya Madaftari ndoa na Talaka  na  Taratibu za  usimamizi wa  Madaftari ya  Usajili .

error: Content is protected !!