Daily Archives: March 9, 2020

MALENGO YA WANAWAKE HAYATAWEZA KUFIKIWA IWAPO BADO WANAWAKE WATAENDELEA KUDHALILISHWA

Naibu  Spika  wa  Baraza  la  Wawakilishi   Mh,  Mgeni Hassn  Juma  ame3sema  juhudi  za  kuleta  usawa  wa  jinsia katika  Jamii  zinakwaza  na  kuwepo  kwa  mitazamo  hasi  inayoendelea   dhidi ya  Wanawake   na  vitendo  vya  udhalilishaji.

Amesema  ndoto  na  malengo  ya  Wanawake  hazitaweza  kufikiwa  iwapo  bado  Wanawake  wataendelea  kudhalilishwa na  kufanyiwa  vitendo  vya  kikatili   pamoja  na  kunyimwa  fursa  na  haki  zao  za  msingi   .

Naibu  Spika  Mgeni  ametoa   tamko  hillo  wakati  akifungua  kongamano  la  Siku  ya  Wanawake  Duniani  na  tathimini  ya   ya  utekelezaji wa  Azimio  la  Beijing  amewataka  wanawake   licha  ya  changamoto  hizo  kutokata  tamaa na  kuungana  pamoja  kufanya utetezi  juu  ya  haki  hususanni  katika  masuala  ya  kiuchumi , elimu , afya  na  mapambano  dhidi ya  udhalilishaji.

Akizungumza  katika  Kongamano  hilo  Waziri  wa  Kazi, Uwezeshaji ,  Wazee, Wanawake  na  Watoto   Dr  Maudline  Cyrus  Castico amesema Serikali  itaendelea kusimamia  utekelezaji  wa  Sera  na  sheria  zinazo walinda Wanawake   na  kuwasisitiza  kufanya  kazi  kwa  bidii   ili waweze  kuijitegemea

Mwakilishi  wa   UN Women  hapa  Nchini  Bibi  Jullian  Bosset ameeleza kufarijika  na  hatua zinazo chukuliwa  na  SMZ  katika  kuimarisha Ustawi  wa  Wanawake   na utekezaji  wa  Maazimio  ya Beijing  pamoja  na  kuwa  na  Sera  na  sheria  bora  za   kuwalinda  Wanawake na kuahidi  kuendelea  kuunga  mkono  juhudi hizo.

Siku  ya  Wanawake  Duniani  huadhimishwa  kila  Machi  nane  ya  kila  Mwaka  tangu  ilipoasoisiwa  na Umoja  wa  Mataifa  Mwaka  1975  ambapo  kauli  mbiu  ya  mwaka  huu  inasema  "Endeleza  vuguvugu  la  usawa zingatia haki   na  maendeleo   ya  Wanawake.

error: Content is protected !!