Daily Archives: March 6, 2020

MH.SAMIA AMESEMA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA NI CHANGAMOTO YA KIDUNIA

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amesema ukosefu wa Ajira kwa Vijana ni changamoto ya kidunia hivyo amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kuweka mikakakati thabiti ya kupambana na tatizo hilo.

Mh. Samia ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua Mkutano  wa Mawaziri wa Sekta ya Kazi na Ajira na Wadau wa utatu wa Jumuiya  ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC uliyofanyika katika Ukumbi wa  Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam amesema kwa mijubu wa takwimu  za Shirika la Kazi Duniani kuhusu mwenendo wa Ajira kwa mwaka 2020 zaidi ya Watu Milioni 187.7sawa na asilimia 5.4  Duniania hawana kazi .

Mh. Samia amewataka Washiriki wa Mkutano huo kuweka Mikakakti ya kuimarisha   Sekta ya Kazi na Ajira  kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo katika Sekta hiyo  pamoja kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Maendeleo endelevu SADC ya namba 8 yanayohimiza  kuongezeka kwa fursa za ajira zenye staha .

BARAZA LA NNE LA BIASHARA LA ZANZIBAR LINATARAJIWA KUFANYIKA MACHI 7 KATIKA UKUMBI WA SHEIKH IDRISA ABDULWAKIL.

Waziri  wa Biashara na Viwanda  Balozi Amina Salum Ali amesema Baraza la nne la Biashara la Zanzibar linatarajiwa kufanyika Machi 7 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari  Balozi Amina amesema Baraza hilo litajadili shughuli za Biashara na uwekezaji Nchini ambapo mada mbalimbali kutoka Serikalini na  Wafanyabiashara zitawasilishwa.

Aidha amesema pia kutakuwa na mada ya ushirikiano baina ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma pamoja na uhusiano na wajibu wa Wawekezaji katika kuishirikisha jamii.

Katika mkutano huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi.

error: Content is protected !!