Monthly Archives: March 2020

OPERESHENI KUFUATILIA TAARIFA ZA UINGIAJI WA RAIA WA KIGENI KUPITIA BANDARI ZISIZO RASMI IMEFANYIKA

Serikali ya Mkoa wa Kusini  Pemba kwa kushirikiana na Wizar ya Afya umefanya Opresheni Maalum ya kufuatilia taarifa za uingiaji wa Raia wa Kigeni  kupitia Bandari zisizo rasmi  huko katika Kijiji cha Tundaua Chakechake.

Akizungumza katika operesheni hiyo Waziri wa Afya Mh.Hamad Rashid amesema kumekua tabia ya baadhi ya Raia kutoka Nchi jirani kuingia Nchini kinyume na sheria, ni lazima kufuatwa  Sheria za kuingia Nchini hasa katika kipindi hichi cha kujikinga na Maradhi ya Corona.

Amewapongeza Wananchi wa Kijiji hicho cha Tundaua Wilaya ya Chakechake kwa kutoa Taarifa hizo na kuwaomba Wananchi wa maeneo mengine kuiga Mfano huo.

Baadhi ya Raia waliongia Kisiwani Pemba kupitia Bandari ya Wesha ambao Baada ya Kuchunguzwa Afya zao wamesema walifuata taratibu Sahihi za kuingia Nchini.

 

HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA MTU YEYOTE ATAKAYETUPA TAKA KWENYE MTARO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo Wapili wa Rais Mhe.Mohamed Aboud amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitosita kumchukulia hatua Mtu yoyote  atakaebaini kuchafua au kutupa taka kwa makusudi  katika Mitaro ya kupitishia Maji Taka .

Kauli hiyoameitoa wakati alipofanya Ziara ya kutembelea Mitaro ya Maji Taka katika Maeneo ya Kilimani ,Sebleni,Mwanakwerekwe na Mikunguni amesema Serikali imetumia fedha nyingi katika kujenga Mitaro hiyo hivo haitakuwa tayari kuona Mwananchi anaharibu Mitaro hiyo kwa makusudi.

Hata hivyo  alisema  kwa wale waliojenga karibu wa Mitaro hiyo watahamishwa kwa mujibu wa Sheria na kuwataka Wananchi kutojenga karibu ya Mitaro hiyo kwani Serikali haitokuwa tayari kumlipa Mwananchi  yoyote ambae atakiuka agizo la Serikali.

Aidha  amewapongeza Wakandarasi hao kwa kazi nzuri waliyo ifanya na kuwataka  kujitajidi katika kumaliza kazi hiyo kwa wakati uliopangwa hasa ukizingatia kipindi kichokuja ni cha Mvua za Masika .

Mratibu wa Mradi huo Makame Ali amesema   mradi huo unakiasi cha kilomita 21 Elfu na umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 49  Fedha amabzo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mkadarasi anasimamia Ujenzi huo kutoka Kampuni ya CRJE ya China Nd.John Nyakoroe amesema tayari kazi ya kumaliza mradi huo imefikia asimia 95 ambo inatarajiwa kumalizika Mwanzoni mwa Mwezi   wa  Mei.

WIZARA YA KILIMO IMESEMA HAITOMVUMILIA MTU YEYOTE ATAKAYEHAMISHA RASILIMALI KINYUME CHA SHERIA

Wizara   ya Kilimo Maliasili Mifugo na  Uvuvi   imesema  haito mvumilia Mtu yoyote atakae  bainika  anahamisha Rasilimali yoyote isiorejesheka  kinyume  na sheria .

Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi  Mh.Mmanga  Mjengo Mjawiri amesma hayo wakati alipo kuwa akiangalia  Gari zilizo kamatwa  zilizokuwa zinasafirisha Mchanga  na mbuyu  kinyume na  sheria Maruhubi Mjini  Zanzibar.

Mh.Mmanga amesema  bado kuna baadhi ya Watu wasiokuwa na imani  wanajaribu  kufanya  uhujumu wa Rasilimali  zisizo rejesheka  kwa  kukeuka utaratibu wa  ulioekwa na Idara husika  ambapo amesema watachukuliwa hatua kali za Kisheria  pindi watakapo bainika .

Msimamizi wa Sheia za Misitu Nd.Haji wa Haji Hassan   na   Mkurugenzi wa  Idara ya Misitu Nd.Sudi  Muhamed Juma wamesema  kukamatwa kwa dari hizo ni kufuatia  doria wanazo zifanya  baada ya kutialia  wasaiwasi juu ya eneo hilo la Mkwajuni.

Gari hizo tatu za Mchanaga na moja ya ambayo imebeba  Mbuyu  ambao ulikuwa unasafirichwa kinyume na  Sheria zimehifandhiwa idara ya Misitu Maruhubi baada ya  Wahusika kukimbia    kisiko julikana .

 

 

DKT SHEIN AMEONGOZA WANANCHI NA VIONGOZI KATIKA MAZISHI YA WAZIRI KIONGOZI WA KWANZA WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameongoza Mamia ya Wananchi, Viongozi  wa Serikali  na  Vyama vya Siasa  katika Mazishi ya aliyekuwa Waziri Kiongozi wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Ramadhan Haji Faki yaliyofanyika Kijijini kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Marehemu amesaliwa katika Msikiti Mkuu wa Mwembeshauri na Sala kuongozwa na  Mufti Mkuu wa Zanzibar.

Nd. Ramadhan Haji Faki  amezaliwa mwaka 1930  na amefariki jana Jijini Dar es salaam akiwa na umri wa miaka 99

Marehemu Faki ambae alikuwa Mjumbe wa Kamati ya watu 14 ya Chama cha ASP iliyoongoza Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 alishika wadhifa wa Waziri Kiongozi Mwaka 1983 hadi 1984.

Katika uhai wake Marehemu Faki alitumikia Jeshi la polisi kwa muda wa miaka 14 akipitia vyeo mbali mbali na mwaka 1966 alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania na kutunukiwa vyeo kuanzia Kapteni hadi Brigedia Jeneral na pia alishiriki Vita vya Kagera.

Kabla ya kuwa Waziri Kiongozi mwaka 1980 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Baraza la Mapinduzi na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi mwaka 1964 hadi 1984.

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohamed Aboud ameongoza ujumbe wa Serikali kutoa Rambi rambi  kwa  Familia ya Marehemu.

error: Content is protected !!