Daily Archives: February 8, 2020

TANZANIA IMEISHAURI ETHIOPIA KUTAFUTA KIINI CHA RAIA WAKE KUKIMBIA NCHINI HUMO

 

Tanzania imeishauri Ethiopia kutafuta kiini cha Raia wake kukimbia Nchini humo ambapo mpaka sasa Raia elfu moja na Mia tatu  wa Ethiopia wanashikiliwa katika Magereza ya Tanzania.

Tanzania imeishauri Nchi ya Ethiopia kuchukua hatua ya kuchunguza kiini cha Raia wake kuondoka Nchini humo kinyume na utaratibu na kwa njia zisizo halali jambo linalosababisha   mrundikano wa Wafungwa ambao wanakamatwa katika Nchi wanazopita kama Wahamiaji Haramu ikiwemo Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba  Kabudi ametoa ushauri huo Addis Ababa Ethiopia katika  Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Kando ya Mkutano huo Dkt. Workneh Gebeyehu na  kuchukua hatua za kudhibiti idadi ya Raia wake wanaondoka Nchini humo na kukamatwa katika Mataifa mengine ikiwemo Tanzania.

Prof. Kabudi amesema mpaka sasa takribani Raia zaidi ya 1,300 wanashikiliwa katika Magereza mbalimbali Nchini Tanzania huku idadi ya wanaoendelea kukamatwa ikiongezeka jambo linalosababisha mrundikano wa Wafungwa katika Magereza .

Ameongeza kuwa katika mazungumzo hayo Tanzania na Ethiopia zimekubaliana kuchukua hatua za pamoja zitakazowezesha kurejeshwa Wafungwa na Wahamiaji Haramu Wa nchi hiyo wanaoshikliwa Tanzania kwa utaratibu utakaokubalika baada ya majadiliano ya kina na kitaalamu.

Akizungumza kupitia kwa Msemaji Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh Gebeyehu amekiri kuwepo kwa tatizo la Vijana wa  Nchi hiyo kuondoka Nchini humo kinyume cha utaratibu na kuitumia Tanzania kama mapito wakielekea katika Nchi za Kusini mwa Afrika na Ulaya na kuongeza kuwa Serikali ya Nchi hiyo itachukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo.

 

 

WANANCHI WA KIJIJI CHA OLE WAMETAKIWA KUSOMA SHERIA ILI KUEPUKA KUCHUKUA HATUA MIKONONI MWAO

Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Nd Mattar Zahor amewataka Wananchi wa Ole kujifunza na kusoma Sheria ambapo itawasaidia kuepuka kuchukuwa hatua mikononi mwao pindi inapotokezea migogoro katika jamii.

Nd,Mattar ametowa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi na Wanafunzi   huko katika Skuli ya Msingi Ole  ikiwa ni shamra  shamra za wiki wa msaada wa kisharia na siku ya sheria duniani.

Nae Kamimu Mkurugenzi  kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Chake Chake  ,Maalim Mohammed  Hassan  Abdalla  amesema dhamira ya Jumuia  ni kuona   Wananchi  wamekuwa na uwelewa wa kisheria  ili kuona yale makossa ambayo yamo ndani ya Jamii  yanapunguwa  ili kupata Jamii iliyobora.

Pia  Nd,Seif Mohammed Khamis  ambae ni Wakili wa Serikali  wakati akijibu  baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Wanachi  amesema tatizo la ucheleweshaji wa utolewaji wa hukumu au kuharibika kwa Kesi za udhalilishaji  inatokana na baadhi ya vitendo hivyo kuchelewa kuripotiwa.

 

error: Content is protected !!