Daily Archives: February 6, 2020

WIZARA YA AFYA IMEZINDUA MPANGO WA AFYA YA JAMII UTAKAOTOA HUDUMA ZA AFYA KWA HATUA ZA AWALI

Wizara ya Afya imezindua mpango waAfya ya Jamii utakaotoa huduma za Afya kwa hatua za awali kwa Mtu mmoja mmoja katika ngazi ya Shehia ambao utarahisisha mfumo wa kutoa huduma bora za Afya kwa Wananchi

Mpango huo umezinduliwa na Waziri wa Biashara naViwanda Balozi Amina Salum Ali katika Mkutano wa Mwaka wa Wizara hiyo uliowakutanisha Wadau wa Sekta ya Afya, Taasisi naWashirika wa Maendeleo.

Wakizungumza katika Mkutano huo Balozi Amina na Waziri wa AfyaMh. Hamad Rashid Mohamed wamesema mpango huo ni  kutimiza Sera ya Serikali ya kutoa huduma za Afya bure ambapo Zanzibar ipo katika nafasi nzuri kwa Nchi nyingi za Afrika kuwafikia Wananchi wengi hasa wa Vijijini.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay amesema Wizara ya Afya inapaswa kufanya juhudi za kukabiliana na matatizo ya vifo vya Mama na Mtoto na maradhi yasiyoambukiza na pia kutoa huduma bora za Afya zinazoendana na Sera za WHO

Mkutano huo wa 15 wa kutathmini utoaji wa huduma, matatizo na mapendekezo kwa Mwaka ujayo umeelezea mafanikio yaliyofikiwa na Wizara hiyo ikiwemo kuongeza idadi ya Madaktari kutoka Daktari mmoja kwa Wagonjwa 31, 838 Mwaka 2010 hadi kufikia Daktari 1 kwa Wagonjwa 6,276 2019.

MASHEHA WAMETAKIWA KUTOA USHIRIKIANO NA TAASISI MBALI MBALI ZA SERIKALI

Ofisi ya Mtathmini Mkuu wa Serikali imewaomba Masheha kuwa tayari kutoa ushirikiano na Taasisi hiyo wanapotekeleza majukumu  yao.

Akizungumuza naViongozi hao pamoja na Watendaji wa Wilaya ya Kaskazini “A” ikiwa ni muendelezo wa kuitambulisha Ofisi hiyo kwa Wananchi Afisa Mipango Nd.Suleiman Faki Khamis amesema kazi kuu wanayoifanya ni kukagau Ripoti ya thamani sahihi ya kitu au malipo mbalimbali kwa mujibu wa Sheria.

Kaimu Katibu Tawala Nd.Khatibu Habibu Ali ameishukuru Serikili ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuanzisha Taasisi hiyo kuzingatia uadilifu  ili kuepusha migogoro isiyokuwa na tija.

Baadhi yaWashiriki wa Mkutano huo wamesema Taasisi itasaidia kujua ukweli wa thamani ya kitu kinachouzwa au kununuliwa hali itakayondosha Wananchi kudhulumiwa haki zao.

Ofisi ya Mtathmini Mkuu wa Serikali imeanzishwa tangu Mwaka 2015 ambapo kwa sasa naaendelea kutoa Elimu kwa Jamii kuitambuaTaasisi hiyo pamoja na majukumu yake kwa Jamii.

MAWAKILI WASIO NA SIFA AMBAO WANAITIA DOSARI SEKTA YA SHERIA NCHINI KUDHIBITIWA

Waziri wa Katiba na Sheria Mh Khamis Juma Mwalim amesema Serikali inakusudia kuwadhibiti Mawakili wasio na sifa ambao wanaitia dosari Sekta ya Sheria Nchini.

Akiwasilisha Mswaada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Mawakili sura ya 28 na kutunga Sheria ya Mawakili na Wakuu wa Viapo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mh Mwalimu amesema Zanzibar imekuwa na idadi kubwa ya Mawakili lakini hawatambuliki Kisheria.

Amefahamisha kuwa lengo la Serikali ni kuondosha kasoro katika utekelezaji wa Sheria hiyo pamoja na kuimarisha uadilifu na utawala wa Sheria katika utekelezaji wa majukumu mbali mbali.

Akiwasilisha maoni ya kamati ya Sheria Utawala bora na Idara Maalum Makamo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Zulfa Mmaka Omar amesema kuumarishwa kwa Mswaada huo kutaiwezesha Jumuiya ya Mawakili Zanzibar kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi..

Wajumbe wa Baraza hilo wameujadili pamoja na kuupitisha Mswaada huo kwa hatua nyengine ili uwe Sheria kamili.

 

UWT ITAENDELEZA KASI YA KUTAFUTA WANACHAMA WAPYA ILI KUIMARISHA JUMUIYA HIYO

Naibu Katibu Mkuu wa UWT  Zanzibar Nd.Tunu Juma Kondo amesema Jumuiya hiyo itaendeleza kasi ya kutafuta Wanachama wapya ili kuimarisha Jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na Wanachama wa UWT  Mkoa wa Kusini Unguja huko Dunga pamoja na kukabidi kadi Wanachama wapya Nd.Tunu amesema Jumuiya za Chama ni chachu za kuimarisha CCM  hivyo hazitasita kuandikisha Wanachama wapya  ili kukipa nguvu zaidi.

Amesema UWT  itaendeleza juhudi za malezi bora ya Watoto  wa Tanzania wakuwe katika maadili mazuri ili baadae wawe Viongozi waadilifu.

Mwakilishi wa viti maalum Mkoa wa Kusini Unguja Mh.Wanu Hafidh Ameir amesema Viongozi wa Mkoa huo wataongeza juhudi za kuwawezesha Vijana kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo vyarahani ili waweze  kujikwamue na umasikini .

Katibu wa CCM  Jimbo la Tunguu Nd.Sharifa Maabad Othaman amesema Jumuiya ya UWT  Mkoa  Kusini imefanikiwa kutekeleza kazi zake vizuri lakini pia inakabiliwa na tatizo la Wanachama kutolipa ada sambamba  na vikiundi vya Kinamama kuwa na mitaji midogo ya kuendesha miradi yao.

Mkutano huo ni sehemu ya maadhimisho ya kutimia miaka arobaini na tatu ya kuanzishwa Chama Cha Mapinduzi

 

error: Content is protected !!