Daily Archives: February 4, 2020

DK. MAGUFULI AMEWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI WA WIZARA, MAHAKAMA, MIKOA NA WAKUU WA MAJESHI

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.   Dk. John Pombe  Magufuli  amewaapisha Viongozi  mbalimbali wa Wizara, Mahakama, Mikoa na Wakuu wa Majeshi aliowateuwa hivi karibuni katika nyadhifa mbalimbali.

Hafla hiyo ya Uapisho imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali   akiwemo  Jaji Mkuu wa Tanzania Pro. Ibrahim Juma na Viongozi wa vyama na Serikali, Viongozi wa Dini Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi   na Usalama .

Mapema akiwaapisha Viongozi hao Mh.Rais Magufuli amewataka Wateule hao kufanya kazi kwa Mashirikiano na uadilifu pamoja na kuweka mbele uzalendo kwa maslahi ya Taifa.

Rais Magufuli amesema wote waliowachagulia ni kutokana na sifa za utendaji wao katika nafasi walizotumikia hapo awali ambapo kwa kila mmoja alizitaja sifa na ufanisi wa kazi yake  na hapa anaeleza.

Nae Jaji Mkuu wa Tanzania Pro. Ibrahimu Juma amemshukuru  Rais kwa kuweza kuwajazia safu ya Mahakama kwa kuwapa Viongozi ambao ndio wanahimili kazi za kila siku za Mahakama.

Miongoni mwa Walioapishwa ni pamoja ni Kamishna  Jenerali wa Magereza  Brigedia Generali Suleiman Mungiya Mzee, mwengine ni Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji DCP.Johm William Hausunga.

Wengine   walioapa  ni Msajili Mkuu wa Mahakama Bw. Wilbert  Chuma, Bw. Kelvin Mhina kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani na Shamira Sarwat kuwa Msajili wa Mahakama Kuu.

Pia amewaapisha Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama akiwemo Jaji Dkt. Gerald, Wakili Julius Kalolo Bundala  na Wakili Genoveva Kato .

Kwa upande wa Makatibu Wakuu waliowapa ni Mary Gasper Makondo kuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Ardhi, Dkt.Hassan Abbas  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, Pro.Riziki Silas Shemdoe Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Zena Ahmed Said   Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Nd. Leonard Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati.

Pia Rais Dk.Magufuli Amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa ambapo Viongozi hao Walioteuliwa walikula Kiapo cha Uadilifu.

 

 

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MH. MWALIMU AMETOA TAARIFA YA MAADHIMISHO WIKI YA MSAADA WA KISHERIA

Waziri wa Katiba na Sheria  Mh.Khamis Juma Mwalimu Ametoa Taarifa juu ya  Maadhimisho ya wiki ya msaada wa Kisheria ambayo itaenda sambamba na siku ya Sheria kwa mwaka 2020 itakayo fanyika siku ya Ijumaa Tarehe 7 Mwezi huu.

Akizungumza  katika Mkutano na Waandishi  wa Habari  uliofanyika  katika Ukumbi wa Ofisi ya katiba na Sheria Mazizini  amesema maadhimisho hayo  yatajumuisha  shughuli mbalimbali  kwa Unguja na Pemba ikiwemo utoaji wa Elimu  kwa Wananchi kupitia Vyombo vya Habari ikiwemo Redio na Televisheni, Ziara katika Shehia mbali mbali ili kuwapatia Wananchi Elimu ya Msaada wa Sheria katika Maeneo yao.

Amesema lengo la kutoa Elimu hiyo ni kuwawezesha Wananchi kufahamu haki zao za sheria ambazo zitattua kero zinazo wakabili na kufikia mahitaji ya kuundwa kwa sheria hizo.

Maadhimisho hayo pia yataambatana na shughuli kuu mbili ambazo ni Uzinduzi  wa  usajili wawatoa Huduma za Msaada wa kisheria kwa njia ya Kielekroniki na pia Uzinduzi wa Sheria ya Msaada wa Kisheria kwa Lugha nyepesi.

Kauli  mbiu ya maadhimisho hayo ni upatikanaji wa msaada wa kisheria ni nguzo kwa Ustawi wa Jamii ikiwa lengo kuu ni kuona Ustawi wa Jamii unaimalika kupitia msaada huo wa Kisheria.

 

MKUTANO WA KUMI NA SABA WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR UNATARAJIWA KUANZA 05 /02/2020

Mkutano  wa kumi na saba wa  Baraza la tisa la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza Jumatano  ya Tarehe tano Febuari  Mwaka huu.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Nd.Raya Issa Msellem  akitoa Tarifa kwa Vyombo vya Habari  amesema kuwa Mkutano huo utajumuisha Shughuli   mbalimbali kiwemo maswali na majibu 112 ambayo yameratibiwa kwa ajili ya  kujibiwa kwenye Mkutano huo.

Aidha  amefahamisha kuwa katika  mMswada itakayojadiliwa ni pamoja na mswaada wa sheria ya kuweka masharti yanayohusiana na haki  na huduma za ustawi kwa Wazee na kuanzisha mpango wa Pensheni Jamii pamoja  na mambo mengine. .

UJENZI WA MTARO WA BARABARA YA MIKUNGUNI UNATARAJIWA KUKAMILIKA MWISHONI WA MWEZI WA TATU MWAKA HUU

Ujenzi wa Mtaro wa Barabara ya Mikunguni unaoendelea kujengwa   unatarajia kutumia kiasi cha Shilingi Bilioni 49 badala ya pesa za awali zilizotarajiwa kutumika Bilioni 23 na kukamilika  kwa Ujenzi huo ni  tarehe 31 mwezi wa tatu  Mwaka huu .

Akitoa Taarifa za Ujenzi wa Mtaro huo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya CRJE  Nd.John Yakuru  ameelezea hali ya Ujenzi  wa Mitaro ya Kilimani na Mikunguni amesema wako katika hatua nzuri nawatakamilisha kwa wakati uliopangiwa  na kuwataka Wananchi kuwa wastahamilivu .

Amesema   wapo katika hatua za mwisho katika Mtaro wa Mikunguni na baadae kurejesha hali ya Barabara kama ilivyokuwa  kwani Barabara hiyo ina kilomita 20  ambapo mradi huo  wa Mitaro unasimamiwa na ZUPS chini ya usimamizi Mkuu Wizara ya Fedha

kwa upande wa Wananchi wanaotumia  Barabara ya Mikunguni pamoja na Wafanya Biashara pembezoni mwa Barabara hiyo wameiomba Serikali kuwasimamia Wakandarasi  wa Ujenzi huo kumaliza kwa haraka ili kuendelea  na harakati zao za maisha  kwa vile  Barabara hiyo  imechukua muda mrefu Ujenzi wake .

Wamesema licha ya kuwa Ujenzi wa Barabara hiyo kuendelea lakini bado imekuwa ni kero kwao  na kuikosesha Serikali Kodi   pamoja na wao kukosa kufanya biashara zao vizuri kwa sababu wateja hawapiti njia hiyo   hivyo basi wameiomba Serikali kuliona hilo ili  kukamilika kwa ujenzi huo kutatoa fursa kwao na kuweza kuendesha  harakati zao za maisha

 

error: Content is protected !!