Daily Archives: February 2, 2020

SERIKALI YA TANZANIA NA CHINA ZIMETOA TAMKO LA PAMOJA KUHUSU HALI ZA WATANZANIA WALIOKO NCHINI CHINA

Serikali yaTtanzania na China zimetoa Tamko la pamoja kuhusu hali za Watanzania walioko Nchini China na hatua zinazochukuliwa na Nchi hiyo kukabiliana na Virusi vya Corona.

Akizungumza katika Kikao cha pamoja kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba John Kabudi na Balozi wa China aliyekuwepo Nchini na Waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amesema mpaka sasa hakuna Mtanzania yeyote au Raia wa Kigeni aliyethibitika kuwa na Virusi hivyo.

Hata hivyo Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki na za dharura ikiwemo kuwapima Watu wote Wanaowasili Nchini kupitia Viwanja vya Ndege na aina nyingine za Usafiri.

Nae Prof.Palamagamba Kabudi Amefahamisha kuwa Ubalozi wa China umeomba fursa ya kukutana na Serikali ya Tanzania kwa nia ya kueleza hali ilivyo Nchini China, hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Nchi hiyo katika kukabiliana na Maradhi hayo na hali ilivyo kwa Watanzania Wanaoishi Nchini China.

Balozi wa China Nchini Wu Ke amewaondoa wasiwasi Watanzania kwa kusema kuwa zaidi ya Wanafunzi 4000 waliokuwepo Nchini China hasa katika Mji wa Wuhan ambao imeathirika na Virusi vya Corona wapo salama na hakuna aliyeathiriwa.

MAHAKAMA ZANZIBAR IMESEMA IPO KATIKA MPANGO WA KUANDAA MFUMO WA KUPUNGUZA KESI KATIKA MAHAKAMA ZAKE

Idara ya Mahakama Zanzibar imesema ipo katika mpango wa kuanda Mfumo Maalumu wa kupunguza mrundikano wa Kesi katika Mahakama.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Hakimu wa Wilaya ya Mwanakwerekwe Mohamed Subeti wakati wa Uzinduzi wa wiki ya Sheria kwa Kanda ya Dar es salaam ambapo amesema kwa sasa wapo katika mchakato kuanda mifumo hiyo kwa kila Mkoa ili kuondoa mrundikano wa Kesi Mahakama.

Awali Akizundua wiki ya Sheria Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mh.Paul Makonda ameiomba Taasisi ya Mahakama Nchini kuendelea kutoa Haki kwa wakati ili kuondoa malalamiko kutoka kwa Wananchi juu ya Taasisi hiyo.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kanda ya Dar es salaam Lameck Maiko Mlachi Amesema wiki ya Sheria itatoa fursa ya Wananchi kutoa mrejesho juu wa mpango mkakati wa miaka ya mitano wa Mahakama ulianza kutekelezwa mwaka 2015/2020

Uzinduzi wa wiki ya Sheria, Kanda ya Dar es salaam ulikwenda sambamba na matembezi ya yaliyoanzia Mahakama ya Kisutu hadi Viwanjwa vya Mnazi Mmoja Jijini humo ambapo Wizara ya Sheria na Katiba Zanzibar nayo ilishiriki katika matembezi hayo.

Ikumbukwe kuwa wiki ya Sheria kwa Tanznaia Bara imeanza leo february  mosi 2020 na inatarajiwa kuhitimishwa february sita mwaka huu Jijini Dar es salaam.

JAMII WAMETAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUSOMA VIATBU VYA KISWAHILI ILI KUWEZA KUPATA TAALUMA YA JUU

Wanajamii na Wapenzi wa Lugha ya Kiswahili wametakiwa kuwa na Utamaduni wa Kusoma Viatbu vya kiswahili ili kuweza kupata Taaluma juu ya mambo mbali mabli.

Akisoma Risala Mwenyekiti wa Klabu ya kusoma Vitabu Bi. Maryam Hamdan Amesema lengo la kuanzisa Klabu hiyo ni kuhuisha na kuwahamasisha Wanafunzi na Wanajamii kurejesha Utamaduni wa zamani wa Kusoma Vitabu ambao kwasasa umepotea kutokana na utandawazi.

Bi. Maryam amesema Klabu yao pia inajihusisha na kufanya uhakiki wa Vitabu mbali mbali vikiwemo vilivyomo katika Mitaala ya Wanafunzi  ili kuweza kuwasaidia na kuwajenga Wanafunzi kuwa na Utamaduni wa kupenda kusoma vitabu na kuweza kupata Ufaulu Mzuri katika Masomo yao.

Akizinduwa  Klabu hiyo ya Kusoma Vitabu katika Ukumbi wa Maktaba Kuu Maisara Mjini Magharib Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pembe Juma amesema Wizara ya Elimu inaiunga Mkono Klabu hiyo kwani ni njia moja itakayowawezesha Wanafunzi kutumia muda wao mwingi katika kujishughulisha kutafuta Elimu na kuachana na kushiriki katika mambo maovu.

Mh. Riziki pia amewataka Wanaklabu hao kutumia Vyombo vya Habari katika kuwahamasisha zaidi Wananchi kurejesha Utamaduni wa Kusoma Vitabu ili waweze kuamka zaidi na kuona umuhimu wa kujifunza mengi yatakayoijenga Jamii Kiuchumi, Kiutamaduni na Kijamiii kupitia Vitabu.

Kwa upande wao Wanafunzi walioshiriki katika hafla hiyo wamesema miongoni mwa mambo waliojifunza kupitia uhamasishaji huo ni pamoja na kujenga tabia ya kutumia vizuri muda wao katika kutafuta Taaluma  kupitia vitabu ili waweze  kuchambuwa mambo kwa ufasaha.

error: Content is protected !!