Daily Archives: February 1, 2020

DK.ALI MOHAMED SHEIN ANATARJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADDHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein anatarjiwa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Sheria Zanzibar .

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu amesema maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na uwekekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Mahakama Kuu liliopo Tunguu.

Amesema mbali na uwekaji wa jiwe la msingi pia kutakuwa na maonesho ya mambo ya sheria ambayo yatafanyika katika Viwanja vya Maisara kuanzia febuari 7 ambapo taasisi zinazosimamia masuala ya sheria zitashiriki na kuweza kutoa elimu kwa Wananchi.

Jaji Makungu amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni dumisha utawala wa sheria na demokrasia katika uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo kauli mbiu hiyo itaenda sambamba na kuelekea uchaguzi  katika kudumisha Amani.

Aidha Mh. Makungu amewataka Wananchi kushiriki kwa wingi katika maonesho hayo ili kuweza kupata ufahamu juu ya masuala ya sheria na kuweza kupatiwa ufumbuzi katika mambo mbali mbali.

JUMLA YA TANI ZA UJAZO LAKI TATU NA ELFU SABINI ZA MAFUTA ZINATARAJIWA KUINGIZWA NCHINI

 

Jumla ya Tani za ujazo laki tatu na elfu sabini za Mafuta zinatarajiwa kuingizwa Nchini kwa ajili ya matumizi ya Ndani na Nje ya Nchi katika kipindi cha mwezi wa Machi mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa pamoja (PBPA) Nd.  Erasto Simon Mlokozi wakati akitangaza tenda kwa ajili ya uagizaji wa Mafuta kwa mwezi Machi Mwaka huu.

Amesema asilimia 51 ya Mafuta hayo yatakuwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya Nchi na asilimia 49 zitakuwa kwa ajili ya Nchi zinazopitisha mafuta katika Bandari ya Dar es salaam.

Aidha Mlokozi amesema ushiriki wa Kampuni za ndani katika uagizaji wa Mafuta bado ni ndogo licha ya kuzipa kipaumbele katika zabuni.

error: Content is protected !!