Monthly Archives: February 2020

MAMA SAMIA SULUHU HASSANTAYARI AMEHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ameitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuhakikisha Wananchi wote wenye sifa ya Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanapewa nafasi hiyo ili waweze kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.

Mhe.Samia akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuhakikiwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura huko Skuli ya SOS Mombasa amesema Kujiandikisha katika Daftari hilo ni haki ya kila Mzanzibari mwenye sifa na kuwataka Wananchi kufika katika Vituo vya Kujiandikisha wakiwa na vielelezo vinavyohitajika.

Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar Thabit Idarous Faina amesema Tume itafanya Tathmini baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya kuhakiki na kuandikisha Wapiga Kura Wapya katika Daftari la Kudumu na kurudia tena zoezi hilo ili kutoa fursa kwa waliokosa Kujiandikisha katika Awamu hii.

Wananchi waliojitokeza katika Kituo hicho wamesifu utaratibu uliowekwa na Tume katika kuhakiki na Kujiandikisha hali inayowawezesha kukamilisha zoezi hilo kwa Muda mfupi.

Zoezi la kuhakiki na Kuandikisha Wapiga Kura Wapya linaendelea katika Wilaya ya Magharibi ‘b’ ambapo likimalizika katika Wilaya hiyo linategemewa kuingia katika Wilaya ya Mjini.

MHE. SIMAI AMESEMA FANI YA UALIMU INAHITAJI UJUZI NA VITENDO ZAIDI KULIKO MAELEZO

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Mohamed Said amesema fani ya Ualimu inahitaji ujuzi na vitendo zaidi ya kutoa maelezo ili kuleta ukombozi wa Elimu kwa Taifa.

Amesema kwa kutumia vitendo kunawafanya Wanafunzi kuelewa haraka na Masomo wanayofundishwa kukaa kwenye kumbukumbu hali itakayowasaidia kupata ufaulu mzuri.

Mhe. Simai amesema hayo katika Maonyesho ya sita ya dhana za Kufundishia na Kujifunzia ya Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA

Mhadhiri Msaidizi katika Skuli hiyo Said Ali amefahamisha kuwa dhana hizo za kufundishia ndio wanaoutumia katika Skuli hiyo hivyo ni vyema kutumiwa  kuwafundishia Wanafunzi   katika Skuli watakazokwenda kusomesha.

Skuli ya Elimu ya SUZA inaandaa Maonesho hayo kila Mwaka  kuonesha dhana zinazoweza kutumiwa na Walimu Darasani kwa ajili ya kurahisha Ufahamu wa Mwanafunzi.

MH. PAULO MAKONDA KUWEKA MIKAKATI NA MAZINGIRA MAZURI YA KIBIASHARA NA UWEKEZAJI KATIKA MKOA WA DAR

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam Mh. Paulo Makonda amesema wanaweka mikakati na mazingira mazuri ya Kibiashara na uwekezaji katika Mkoa wa huo ili uwe kitovu  kuu cha Biashara cha Kimataifa.

Mh. Makonda ameyasema hayo  katika  kikao cha kamati ya Ushauri wa Mkoa huo kilichofanyikaJijini Dar es salam amesema tayari wameshaweka mipango  madhubuti ya Kiusalama ili kuona shughuli za Kibiashara zinafanyika kwa masaa 24 kuanzia mwezi wa Ramadhani katika Maduka ya Kariakoo.

Amesema katika Bajeti ya Mwaka 2020/2021 Mkoa huo inakadiria  kutenga kiasi cha shilingi  billioni 685   kwa ajili ya kutekeleza  Miradi ya Maendeleo iliyopo katika Mkoa wa Dar es salaam pamoja na kujenga vituo  viwili vya Afya katika maeneo ya Kawe na Bunju A lengo ni kurahishisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa Wananchi.

Nao Wakuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Ubungo,Ilala ,Temeke na Kigamboni wakitowa taarifa za kamati za ushauri za Wilaya zao wamesema wataendelea kuweka mikakati mizuri kwa ajili ya kukusanya Mapato  ili kusaidia kutekeleza Miradi ya kimkakati ya maendeleo  iliyopo katika  Wilaya zao.

Akifunga kikao hicho Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Mh. Mussa Azzan Zungu amesema serikali ya Tanzania imeshakubaliana na Serikali ya Uholanzi kutowa pesa milioni 75 ambazo zitatumika kuimarisha Jaa la Pugu utoaji wa  Magari 20 ya Taka kwa Mkoa wa Dar es salaam pia amesisitiza Wananchi kutunza Mazingira ambapo amesema  bila ya Mazingira salama Taifa litapotea.

Kikao hicho kilichawashirikisha Wakuuu wa Wilaya zote za Dar es salaam , Viongozi  wa Dini, Vyama vya Siasa  ,Vyombo vya Ulinzi na Usalama ,Meya wa Jiji la Dar es salam pamoja na Watendaji mbali mbali wa Serikali.

error: Content is protected !!