Daily Archives: January 29, 2020

ZEC IMESEMA KUWA ZOEZI LA UANDIKISHAJI TAARIFA ZA WAPIGA KURA LITAENDESHWA KWA TARATIBU ZA KISHERIA

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imewahakikishia Wananchi kuwa zoezi la uandikishaji na uhakiki wa Taarifa za Wapiga Kura litaendeshwa kwa misingi na Taratibu za kisheria zilizopo ili kila mwenye sifa  atapata haki ya kuandikishwa katika Daftari la kudumu la Wapiga kura

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  Nd.Suleiman Hassan Haji  wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “a” uliofanyika katika Kituo cha Walimu Mkwajuni ambao umewashirikisha Viongozi wa Serikali,Viongozi wa Dini, Vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na Asasi za Kiraia

Amesema, zoezi la uandikishaji linamuhusu kila Mtu aliyetimiza sifa hivyo, ni wajibu wa kila Mwananchi kuzingatia maelekezo na Elimu inayotolewa na Tume kwa kuhamasisha na kushiriki katika zoezi hilo linalotarajiwa kuanza tarehe 9/2/2020 kwa Wilaya  hiyo na Shehia za Jimbo la Donge .

Wakitoa Muongozo na Utaratibu wa Uandikishaji wa Daftari Maafisa Uchaguzi wa Wilaya wamesema utaratibu  ulioandaliwa  na  Tume  unatoa  fursa  pana  kwa  Wananchi  kutumia  haki  yao ya  Kidemokrasia  na kuwataka  kujitokeza  kwa  Wingi  kujiandikisha.

Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wameishauri Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuendelea kushirikiana na Wakala wa Usajili wa matukio ya Kijamii ili kurahisisha upatikanaji wa Vitambulisho vipya vya Mzanzibar Mkaazi sambamba na kuzingatia ushiriki wa Watu wenye mahitaji maalum kwa  kuwandalia  mazingira Rafiki .

 

MH HAMAD RASHID AMEZITAKA TAASISI ZA DINI, KUSAIDIA KUIHAMASISHA JAMII UMUHIMU WA KULINDA AFYA.

Waziri wa Afya Mh .Hamad Rashid amezitaka Taasisi za  Dini, kusaidia kuihamasisha Jamii umuhimu wa kulinda Afya.

Amesema iwapo Viongozi hao watafikisha Ujumbe huo kwa kutumia mbinu mbalimbali hasa kwa Watoto juu kuosha mikono wanapomaliza shughuli zao kutawasaidia kuwa na tabia ya kujilinda na Afya.

Akifungua  mkutano wa Viongozi wa Dini mbalimbali wa Tanzania Mh.Rashid amesema Maradhi yanapoingia Nchini hayachaguwi Dini wala Siasa hivyo ni vyema Viongozi kushirikiana na watendaji wa Sekta ya Afya na mazingira ili kuhimiza usafi kwa jamii.

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Interfath Partneship Saud Msumi amesema  Taasisi hiyo inalenga kuwaunganisha viongozi wa Dini zote kushiriki katika masuala muhimu ya Kisiasa Kiuchumi na Kijamii.

Katibu wa Mfuti za Zanzibar Nd.Khalid Mfaume pamoja na Viongizi wa Dini walioshiriki mkutano huo wamesema Dini zote zimehimiza usafi wa aina zote hivyo Wananchi wanapaswa kushirkiana kusimamia hilo.

VIJANA NCHINI WAMESHAURIWA KUJITOA KUSAIDIA JAMII KWA HIARI KATIKA KUKABILIANA NA MAAFA

Vijana Nchini wameshauriwa kujitoa kusaidia Jamii kwa hiari katika kukabiliana na Maafa mbalimbali yanayotokea Nchini.

Mwenyekiti wa Vijana Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross Tanzania  Nd.Rahim Khamis  Kalyango amesema suala hilo litawajenga kuwa wazalendo wenye kuthamini haki za Watu wote.

Akizungumza na Mabaraza ya Vijana ya Mkoa wa Mjini Magharibi amesema  amewaomba kujiunga na Taasisi hiyo ili kupata fursa hizo za kujitolea kwa Jamii pale inapokutwa na

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar  Nd. Khamis Rashid  Kheir amewaomba Vijana kutuma fursa zinazotolewa na wadau mbalimbali ili kuendeleza kielimu na kujiinua kiuchumi.

WIZARA YA ELIMU IMEOMBWA KULIPATIA UFUMBUZI TATIZO LA KUTOLEWA KWA UFAULU WA SOMO LA DINI

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imeombwa kulipatia ufumbuzi wa haraka  tatizo la kutolewa kwa ufaulu wa somo la Dini kwa Wanafunzi ili waweze kuendelea  na masomo yao.

Imeelezwa kuwa tatizo hilo limekuwa likiathiri watu wengi hususan Vijana wa Kizanzibari kutokana na kukosa fursa ya kuendelea na masomo yao baada ya kuondolewa kwa ufaulu wa somo hilo katika idadi ya masomo manne.

Akizungumza na Wakuu wa Vyuo Vikuu mbali mbali vya Zanzibar katika Ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pembe Juma ameahidi kuzungumza na Wizara ya Elimu ya Tanzania Bara ili kuweza kuipatia ufumbuzi wa haraka kero hiyo ambayo inakwamisha mustakbali wa kitaaluma kwa  Vijana wengi.

Mh. Riziki pia amewataka Wakuu hao wa Vyuo Vikuu kutoanzisha program za masomo ambazo hazijasajiliwa jambo ambalo huwasababisha usumbufu mkubwa kwa Wanafunzi wao baadae wanapokuja kuhitaji vyeti vyao au wanapotaka kuingia katika Soko la Ajira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Utalii SUZA  Dr. Alley Soud Nassor amesema ipo haja kwa Nacte kuweka utaratibu mzuri na kuishirikisha Serikali wanapofanya maamuzi yao ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza hasa kwa upande wa Zanzibar.

Nae Mkurugenzi wa Chuo Cha Afya Bi Aziza Hamid ameiomba Wizara ya Elimu kuzungumza na Nacte ili kuwepo wajumbe kwa upande watakaotoka Zambao watakwenda kusimamia changamoto za Elimu kwa upande wa Zanzibar katika vikao vya Nacte.

 

error: Content is protected !!