Daily Archives: January 28, 2020

DK.MAGUFULI AMEWAAPISHA MAWAZIRI PAMOJA NA MABOLOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Januari, 2020 amewaapisha Mawaziri 2 na Mabalozi 3 aliowateua hivi Karibuni.

Mawaziri walioapishwa ni Mhe. George Boniface Mwataguluvala Simbachawene aliyeapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mhe. Mussa Azzan Zungu aliyeapishwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Mabalozi walioapishwa ni Mhe. Maimuna Kibenga Tarishi aliyeapishwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva – Uswisi, Mhe. Hussein Athuman Kattanga aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Tokyo – Japan na Mhe. Prof. Kennedy Godfrey Gastorn aliyeapishwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa New York Marekani.

Akizungumza baada ya kuwaapisha na kushuhudia wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi hao kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uchapakazi, kutanguliza maslahi ya Tanzania pamoja na kushirikiana vizuri na viongozi na watendaji wengine katika wizara zao.

Amemtaka Mhe. Waziri Simbachawene kushughulikia dosari zilizopo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwemo kuhakikisha watendaji na viongozi ambao ni kikwazo katika ufanisi wa wizara wanaondolewa, pamoja na kushughulikia makubaliano yaliyotiwa saini na viongozi wakuu wa wizara waliopita kuhusu mkataba wa ununuzi wa vifaa vya zimamoto (vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 1) katika mazingira yasiyokuwa na uadilifu na bila kujali maslahi ya Taifa.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

ZOEZI LA UHAKIKI NA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA LA ENDELEA WILAYA YA WETE NA CHAKE CHAKE

Wananchi wa Wilaya ya Wete  na Majimbo matatu  ya Wilaya ya Chake Chake likiwemo Jimbo la Ziwani, Ole na Chake Chake  yanayoendelea  na zoezi la uhakiki  na uandikishaji wa daftari la Wapiga kura wamesema wameridhishwa  na hatua zilizochukuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar  ya uhakiki wa Daftari hilo.

Wakizungumza na ZBC  baadhi ya  Wananchi  hao wamesema wameridhishwa na hatua ya zoezi hilo  kutokana na upatikanaji wa  haki bila ya tatizo lolote .

Nao Mawakala wa Vyama vya siasa wamesema zoezi hilo linakwenda kwa Mashirikiano makubwa  baina yao na  Maafisa wa Tume ili kuona  lengo la zoezi hilo linafikiwa.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake  Nd.Rashid  Hadid Rashid  amewataka Wananchi kuendeleza  amani na utulivu iliyopo  na kuhakikisha Wananchi wote wenyesifa  ya kuhakiki na kujiandikisha  wanafanya hivyo.

WAKAAZI WA KIJIJI CHA PAJE WAMEPATIWA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO NA KUPATIWA MIWANI BILA YA MALIPO

Katika kuhakikisha huduma za afya zinawafikia Watu wa Vijijini kitengo cha Macho cha Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa kushirikiana na Shirika la Specsavers la Uingereza limetoa huduma ya upimaji macho na kutoa miwani bila ya malipo kwa wakaazi wa kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini.

Akizungumza katika zoezi hilo la upimaji Macho Katibu Tawala Nd. kibibi mwinyi Hassan na Daktari dhamana wa Wilaya ya Kusini Nd.Maulid Abdalla wamewasisitiza wakaazi wa Paje na Vijiji jirani kuitumia fursa hiyo ili kujua matatizo ya macho yanayowasumbua ambayo yanaweza kuwagharimu fedha nyingi.

Mratibu wa shirika la Specsaver Happiness urassa amesema huduma hizo wanazitoa katika Nchi nyingi duniani kusaidia Serikali na Wananchi wenye matatizo ya macho hivyo wameomba kupatwa ushirikiano ili kufanikisha kazi hiyo.

Nao Wananchi waliopatiwa huduma hiyo wameishukuru Serikali na Shirika hilo kwa kuwapatia huduma hiyo ambayo wengi wao wanakuwa na uzito wa kupima afya zao zikiwemo hizo za macho.

WAZEE WENGI WAMEKUWA WAKIISHI MAZINGIRA BORA KUTOKANA NA SERIKALI KUWALIPA PENCHENI KILA MWEZI

Waziri wa Kazi  Uwezeshaji  Wazee  Wanawake na Watoto Mh .Moudline Cyrus Castico amesema  Wazee wengi hivi sasa wamekuwa wakiishi katika mazingira  mazuri  kutokana na kudhaminiwa na Serikali  kwa kulipwa Pencheni kila mwezi na kuwekewa mazingira mazuri katika kupatiwa huduma za msingi.

Mh Castico ameyasema hayo  katika Mkutano wa ushajihishaji wa mswada wa sheria ya Wazee kwa Wajumbe wa Baraza la Wakilishi uliofanyika katika Ofisi ya Takwimu amesema   mswada  huo uliojadiliwa na Wajumbe wa Baraza la Wakilishi utawasaidia  wazee hao kutatua matatizo yao walinayo na hivi sasa wamekuwa wakiishi kwa matumaini  bila ya kuwa na hofu ya kimaisha kutokanaSserikal kuwawekea mazingira bora

Baadhi ya Wazee na  Mwanasheria wa Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto wamesema  mswada huo utawasaidia kupata haki zao za msingi ili waishi katika mazingira bora  kwani kuna baadhi ya Wazee wamekuwa hawapati  haki zao za msingi hivyo kupitishwa kwa  msaada huo ndani ya Baraza la Wakilishi utawasaidia Wazee hao kupata mahitaji yao ya lazima kwa ajili ya maisha yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii [B.L.W]  Mh Mwanatatu  Khamis amesema wapo  tayari kupokea mswada huokwa kufanyia kazi  na kuwaomba Wazee hao  kukusanya mawazo  mengine  kabla ya kupitishwa Barazani ili kuwakomboa Wazee hao  kwa kupata haki zao za msingi.

error: Content is protected !!