Daily Archives: January 27, 2020

MAKATIBU WA UENEZI WA MIKOA YOTE YA ZANZIBAR WAMESEMA WATAENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM

Makatibu wa Uenezi Majimbo,  Wilaya na Mikoa yote ya Unguja na Pemba wamesema wataendelea kulinda miradi  yote iliyozinduliwa katikakipindi cha  Sherehe za mikaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuhakikisha inadumu kwa muda mrefu bila ya kuharibiwa  na watu wasiopenda maendeleo  Nchi  ili kuweka kumbukumbukwa Vizazi vya sasa na vijavyo .

Wakizungumza katika Kikao Maalum  kilichofanyika  Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi Kiswandui Makatibu hao wa Majimbo yoye hamsini na  nne ya Unguja na Pemba wamesema miradi hiyo imegharimu fedha nyingi  kwa Serikali kutekeleza ilani ya Chama  kwa kuweza kutatua matatizo mbali mbali yaliyokuwepo

Wamesema watashirikia vyema na Wananchi pamoja na Viongozi kuhakikisha miradi hiyo inalidwa kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa wakihujumu kwa makusudi maendeleo yanayopatikana kwa faida ya taifa na wananchi.

Katibu wa Kamati maalum ya NEC  Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Bi Catherina  Peter  Nao amelani vikali tukio waliofanyiwa Wanachama wa CCM  hivi karibuni kuchomwa moto Nyumba za Watu watatu na   Watu wasiojulikana   waliochomewa Nyumba zao ni    Ndugu  Nasra Said , Ali Hemed , na Saleh Rashid ambao wanaishi  katika kijiji cha  Wingwi Mapofu  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba  na Watu wasiojulikana

Aidha Bi Caterine ameliomba Jeshi la Polisi  kuchunguzakwa makini  Watu waliofanya tukio hilo na baadae kuchukuliwa hatua kali za Kisheria ili kukomesha vitendo hivyo visiendelee tena kutokea hapa nchini.

BODI ZA MAPATO TRA NA ZRB ZIMETAKIWA KUANDAA MFUMO UTAKAORAHISISHA KUKUSANYA MAPATO NCHINI

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi                       Mhe. Mohammed Ahmada amezishauri Bodi ya Mapato ya Zanzibar ZRB  na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA  kuandaa mfumo utakaorahisisha kukusanya mapato kwa Wageni wanaoingia Nchini.

Ushauri huo ameutowa  baada ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano  ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilipotembelea Kituo cha  Kuhifadhia Kumbukumbu cha Taifa  (Data Center )kilichopo Jijini Dare s salam amesema kuwepo kwa mifumo itakayowiyana  itaweza kusaidia  kujua Takwimu za ukweli ya Wageni wanaoingi  Nchini kwa lengo la kukusanya Mapato yaliyosahihi.

Makamo Mwenyekiti wa Kamati  ya Ardhi na Mawasiliano ya Zanzibar Mh Suleiman Farahani  amesema lengo la  Ziara hiyo ni kuongeza mashirikiano yaliyopo baina ya Taasisi za Tanzania Bara na Zanzibar na  amefurahishwa  kuona Taasisi hizo zinaendeshwa na Wataalum wengi ni Watanzania wenyewe.

Nae Mkuu wa Kituo  cha kuhifadhi Kumbukumbu ya Taifa Cuthbert Simalengo amesema Kituo chake  kipo tayari kufanya kazi kwa pamoja na kituo cha kuhifadhi Kumbukumbu za Zanzibar   kushirikia katika  nyanja mbali mbali ikiwemo kubadilisha mifumo ,kubadilisha uzoefu pamoja na kujifunza kwa pande zote mbili  kwa lengo la kuzisaidia Serikali zote mbili  kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kamati Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi iliendelea na Ziara yake katika Mkoa wa Mtwara ambapo itatembelea Bandari ya Mtwara  na kuangalia Miradi ya gesi iliyopo Mkoani humo.

 

DK.SHEIN AMEWASISITIZA VIJANA KUENDELEA KUWA NA UZALENDO KATIKA JENZI NA ULINZI WA TAIFA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amewasisitiza Vijana kuendelea kuwa na uzalendo katika harakati za ujenzi na ulinzi wa Taifa.

Akitoa shukrani kwa kwa niaba ya Rais wa Zanzibar katika hafla ya chakula cha mchana kwa Vijana wa halaiki na wahamasishaji walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi kutimia miaka hamsini na sita Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Haji Ussi Gavu amesema hatua ya Vijana hao kushirikiana katika sherehe hizo inadhihirisha Uzalendo wao kwa Nchi yao.

Amesema hatua ya Rais ya kula pamoja chakula cha mchana na Vijana hao ni muendelezo wa utamaduni wake wa kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya katika sherehe za Mapinduzi na sherehe nyengine  za  Kitaifa

Akitoa shukrani kwa Rais katibu wa halaiki na hamasa Nd.Ali Mohammed Baraka amesema  Vijana hao wapo tayari kushirikiana katika kazi mbali mbali za ujenzi wa Taifa kwani wameandaliwa kiuzalendo zaidi  na  wako tayari  kulitumikia  Taifa  lao.

 

error: Content is protected !!