Daily Archives: January 26, 2020

DK. SHEIN AMEUNGANA PAMOJA NA VIKOSI VYA ULINZI KATIKA CHAKULA MAALUM CHA MCHANA ALICHOWAANDALIA.

 

Rais waZzanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  ameungana pamoja na Wapiganaji wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki katika Maadhimisho ya Sherehe za kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Chakula maalum cha Mchana alichowaandalia.

Chakula hicho maalum cha Mchana aliwaandalia kutokana na ushiriki wao kwenye Sherehe hizo za miaka 56 ya Mapinduzi zilizofanyika Januari 12 mwaka huu 2020 huko katika Uwanja wa Amaan, Mjini Unguja.

Hafla hiyo ya Chakula maalum ilifanyika leo katika  Viwanja vya Polisi Ziwani Jijini Zanzibar, ambayo ilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.

Wengine ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Washauri wa Rais wa Zanzibar.

Aidha, viongozi wengine pamoja na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Maafisa na Wapiganaji na WanaHabari kutoka  vyombo mbali mbali vya Habari nao walihudhuria.

Katika shukurani zake Rais Dk. Shein kwa Wapiganaji hao zilizotolewa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mh.Issa Haji Ussi Gavu alitoa pongezi kwa Wapiganaji hao kwa kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo Adhimu za kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Waziri Gavu alimpongeza Rais Dk. Shein kwa Uongoziz wake madhubuti uliopelekea kuwepo kwa Salama, Amani, Umoja na Mshikakamno na Utulivu mkubwa ambao umezaa matunda ya maendeleo hapa Zanzibar.

Aliendelea kutoa shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa muendelezeo wake wa  kuwaandalia Chakula maalum cha Mchana ambao ni utamaduni aliouweka kila mwaka baada ya kumaliza Sherehe za Mapinduzi hatua ambayo inaonesha wazi jinsi alivyokuwa na upendo pamoja na imani kubwa na Wananchi wote anaowaongoza.

Alieleza matumaini makubwa yaliopo kuwa kila uchao Sherehe hizo zitaendelea kuwa nzuri na kuvishukuru Vikosi hivyo kwa kufanikisha Sherehe hizo huku akitumia fursa hiyo kuvipongeza kwa kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulinda Amani, Utulivu na Mshikamano uliopo.

Waziri Gavu alitoa shukurani za dhati kwa Vikosi hivyo kwa kuadhimisha kwa hali ya juu kilele cha miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Sambamba na hayo, Waziri Gavu alieleza kuwa Sherehe hizo za Januari 12, 2020 zilivutia sana ambazo zilikuwa ni kielelezo cha kutosha cha Mapinduzi ya Januari 12.1964 yaliyowakomboa Wazanzibari wote ambayo yataendelea kulindwa, kuenziwa na kutunzwa daima.

Nae Mkuu wa Brigedi ya Nyuk Zanzibari, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo  ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama alitoa shukurani na pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa kuendelea kuvijali na kuvithamini Vikosi vya Ulinzi na Usalama.

Alimpongeza Rais Dk. Shein kwa kuendeleza utamaduni wake huo aliouweka wa kila mwaka ambapo mara baada ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu huwandalia chakula maalum cha mchana Wapiganaji na Maafisa hao na kula nao pamoja.

Brigedia Jenerali Nondo alitumia fursa hiyo kumkaribisha Rais Dk. Shein pamoja na Viongozi na Wageni wote katika eneo hilo la Viwanja vya Polisi Ziwani na kueleza kuwa hatua hiyo anayoifanya Rais Dk. Shein  inawachochea kuwa na ari ya utekelezaji wa Ulinzi wa Nchi,  Wananchi wake pamoja na kuyalinda Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Pia, Bregedia Jenerali Nondo alieleza namna ya maandalizi ya Gwaride yalivyofanyika hadi kufanikisha Sherehe hizo na kutoa shukurani kwa Rais Dk. Shein pamoja na Serikali kwa kusaidia kufanikisha maandalizi yote ya Gwaride hilo na kutoa pongezi na shukurani kwa niaba ya Wapiganaji wote walioshiriki katika hafla hiyo adhimu.

Ni utamaduni aliouweka Rais Dk. Shein wa kuwaandalia chakula cha mchana Vikosi vya Ulinzi vinavyoshiriki katika gwaride la Sherehe za Mapinduzi pamoja na Vijana na Wanafunzi ambao hushiriki Sherehe hizo kwa kila mwaka.

Hapo kesho Rais Dk. Shein  amewaandalia chakula cha mchana Vijana na Wanafunzi  walioshiriki katika maadhimisho ya Sherehe za kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo hapo katika Viwanja vya  Polisi Ziwani Jijini Zanzibar.

Katika hafla hiyo pia, kikundi cha Taarab ‘Island Super Star’ Maarufu Wajelajela kutoka Kikosi cha Mafunzo kilitumbuiza kwa nyimbo zake mwanana zikiwemo zile za kuhamasisha kuyaenzi na kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 pamoja na Brassband ya Jeshi la Polisi ambayo nayo ilitumbuiza katika hafla hiyo.

VYAMA 10 VYA SIASA VYA UPINZANI VIMEIELEZEA HATUA YA MAENDELEO ILIOFIKIWA NCHINI

Vyama    Kumi   vya   Siasa   vya  Upinzani  vimeielezea   hatua  ya  maendeleo  iliofikiwa  ndani  ya  miaka  tisa    chini  ya  Uongozi  wa  Dr.Ali  Mohamed  Shein   kuwa   imeijengea  heshima  kubwa   Zanzibar   na  inapaswa  kuungwa  mkono  na  kila  mpenda  maendeleo.

Viongozi  wa   Vyama  hivyo  wakitoa  tamko  la  pamoja   la   kumpongeza  Rais  wa  Zanzibar   wakati  wakizungumza  na  Waandishi  wa   Habari wamesema   maendeleo  yaliofikiwa  katika  nyanja  tofauti  ikiwemo  Miundo Mbinu  ya Barabara  ,Uwanja wa  Ndege, na  Uimarishaji  wa  Makaazi  ya  Wananchi  yameonesha  kwa  vitendo  dhamira  ya  Dr.Shein  ya kutekeleza  malengo  ya  Mapinduzi  ya  Januaari  1964.

Wakiwasilisha  tamko  hilo  Viongoi  hao  wa amesisitiza  kuwa    mafankio  hayo  makubwa  hayakuja  kwa  kubahatisha   bali  yametokana  na Uongozi wa  Hekima wa     Dr.Shein  uliojikita  katika  kuimarisha  Amani  ya  Nchi na  kujali  maslahi  ya  Nchi , uimarishaji  wa  Uchumi  na  kusimamia  ukusanyaji  wa  mapato  ya  Serikali.

Wakizungumzia  kuhusu  uandikishaji  katika  Daftari  la  Kudumu  la  Wapiga  Kura  tamko  hilo  limewasisitiza  Wananchi  kutoyumbishwa  na  baadhi  ya  maneno  ya  baadhi  ya  Wanasiasa  na  kuwataka  kujitokeza  kwa  wingi  kujiandikisha   ili  kutumia  haki  yao  ya  Kidemokrasi  ili hatimae   waweze  kupiga  kura.

Vyama  kumi  vya  Siasa vilivyojumuika  kutoa  tamko  hilo  la  pamoja  la  kumpongeza  Rais Dr.Shein ni  TLP, NLD,Chama  Cha  Demokrasia  Makini , Ada Tadea . Dp  , Sau  , UNDP , AFP, ADC na NCCR  Mageuzi.

SERIKALI ITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA MAKAMPUNI MBALI MBALI KATIKA KUSAIDIA MAENDELEO YA NCHI

Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi,  amesema Kuwa Serikali   Itaendelea kuunga Mkono  na kushirikiana  na  Kampuni  na wadau wa maendeleo  wenye nia njema  katika kusaidia makundi maalum  ya Watu Wenye Ulemavu  kwa kuwapatia nyezo za kufanyiakazi ili kuondokana na dhana potofu  juu  watu wenye ulemavu kuwa ni ombaomba.

Hayo yamesemwa Katika Houtuba iliyo somwa kwa maniaba yake na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh.Mihayo Juma N’hunga, katika ghafla ya kukabidhi visaidizi  kwa watu wenye ulemavu katika Viwanjwa vya Mapinduzi Square.

Aidha alisema  kuwa Serikali itaendelea  kutoa fursa mabali mbali kwa Watu Wenye Ulemavu zikiwemo za Ajira na kutoa mafunzo mbali mbali kwa makundi hayo kwakuamini yatawapa manufaa makundi hayo ambayo  kwa kiasi kikubwa yatawasaidia  kwani  baadhi yao wamefanikiwa  sana katika maendeleo bila ya kujali hali walizo nazo.

Alisema  kuwa inatia moyo kuona   kuwa bado kuna Makupuni yenye moyo wa Kizalendo ambayo yanasaidia makundi haya bila ya kujali hali walizo nazo  kwa Walemavu kwakuamini Walemavu wana wenawez kufanyakazi  kama watapatiwa visaidizi.na

Katika hatua nyengine Balozi Seif aliendelea  kiishukuru  kampuni   ya  TCC  kwa kushirikiana   na Idara ya Watu Wenye Ulemavu  Zanzibar ambayo ipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili  wa Rais pamoja na Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu  SHIJIWAZA  kwa mchango wao walio utoa  kwa kuweza kutambua mahiutaji ya watu wenye ulemavu

Balozi Seif Ali amewasisitiza makundi hayo kuweza kuvitumia vizuri visaidizi hivyo katika shughuli zitakazo waletea maendelea kwa kuwasisitiza kuwa Ulemavu sio Umasikini na kwamba ukiwa nakifaa chakusaidia wanaweza kufanya kazi.

Nae Mkurugenzi wa Sheria wa  Kampuni ya TCC  Ndugu Godson Killiza,  akizungumza kwa niaba ya Meneja  Mkuu wa Kampuni hiyo alisema kuwa wamefarijika  na  mapokezi makubwa waliyoyapata   kutoka kwa Viogozi hao na kuahidi  kuendelea   kusaidia Watu Wenye Ulemavu hapa Zanzibar  kadiiri  watakapopata  nafasi kwani  imekuwa ni desturi yao  katika kusaidia Jamii ya Watu Wenye Ulemavu.

Mkurugenzi huyo wa TCC  alisema kuwa  utowaji huo wa Visadizi unaingia katika Awamu ya saba   kwa upande wa Zanzibar amabapo awamu nyenginze zilikuwa katika Mikoa ya Pwani ,Dar Esalam ,Dodoma ,Morogoro, Ruvuma pamja na Geita ambapo jumla ya  watu 1800 walipatiwa visaidizi hivyo,

Hata hiyo Mkurugenzi huyo aliwataka  Watu Wenye Ulemavu kuchangamkia fursa za   vifaa hivyo kwani vifaa hivyo vingi miongoni mwa vimetengenezwa  hapahapa Tanzania kupitia  miongoni mwa watu Wenye Ulemavu aliongeza kusema Mkurugenzi huyo.

Kwa Upande wake Mwenyekiti  wa Jumuiya Za watu Wenye Ulemavu Zanzbar, SHIJUWAZA Bi Mwandawa Khamis  Mohamed, amauomba Uongozi na Seirikali kwa Ujumla kuangalia Sheria ya Utoawaji wa   huduma  zinazohusu Kampuni kama hizo na kuzipitia tena  sharia hizo hasa kwa Watoto walio chini ya Umri wa miaka kumi na 18

Aidha Mwenyekiti huyo  aliushukuru Uongozi huo kwa kujali hali za Watu Wenye Ulemavu na kuziomba Kampuni nyengine  kuweza kuiga mfano wa Kampuni hiyo  katika kuwasaidia Watu Wenye Ulemavu.

Katika Makabidhiano hayo Jumla ya  Watu Wenye Ulemavu 210  wamekabidhiwa vifaa hivyo vikiwemo  Basikeli  za maringi matatu 50 ,viti mwendo 30, jozi za magongo 30 na fimbo 100 zimekabidhiwa kwawatu wenye ulemavu wamakundi mabalimbali.

 

WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU NCHINI WAMEHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ELIMU

Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini wamehimizwa kuchangamkia Fursa za Elimu, na Uchumi kutokana na umuhimu wa Sekta hizo katika maendeleo ya jamii.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery Bin Ally wakatiakifungua Semina ya Waqfu wa Sarafu (Cash Waqf) iliyoandaliwa na Benki ya Kiislamu ya Pbz ambapo amebainisha kuwa utafutaji wa Elimu ndio Agizo la kwanza alilopewa Mtume Muhammad (S.aw) na hivyo linapaswa kutekelezwa na Waumini hao kama Ibada nyengine.

Nae Muangalizi wa masuala ya Sheria katika Benki ya Kiislamu ya Pbz Nd.Ally  Sharif Maalim amesema huduma ya Waqfu Sarafu ni miongoni mwa mambo yatakayokuza uchumi wa Kiislamu ambao utasaidia kuikwamua jamii yenye mahitaji katika nyanja mbalimbali na hivyo kuisadia Serikali katika kuleta maendeleo ndani kwa kutatua matatizo ndani ya Jamii.

Akitoa Mada ya Uchumi wa Kiislamu katika Semina hiyo Mkurugenzi wa Huduma za Benki ya Kiislamu ya Pbz ameelezea umuhimu na wajibu wa kila Muimuni katika kujenga uchumi wa Kiislamu.

Semina hiyo ni mwendelezo wa utoaji wa Elimu juu ya huduma ya Waqfu Sarafu inayotolewa na Benki ya Kiislamu ya Pbz tayari ambapo wameshaitoa katika Mkoa wa Mtwara na Visiwa vya Pemba.

 

error: Content is protected !!