Daily Archives: January 24, 2020

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMEFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri.

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Nd. John Kijazi amesema uteuzi huo Dkt. Magufuli amemteuwa Mhe. Mussa Hassan Zungu kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira na Mhe. George Simbachawene anachukuwa nafasi ya  Kangi Lugola aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae nafasi yake imetenguliwa kuanzia leo.

Pia Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kamishna Jenereli wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias andengenye ambaye nafasi yake itajazwa baadae.

Pia Dk Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi watatu ambao wanawakilisha Tanzania katika Nchi mbali mbali ambapo Mabalozi hao wameteuliwa kutokana na Mabalozi waliokuwa katika vituo hivyo kumaliza muda wao.

Vituo vya Mabalozi hao watatu walioteuliwa vitatangazwa baadae.

Pia Dk. Magufuli ameitaka Takukuru kufanya uchunguzi  kuhusiana na Mkataba uliosainiwa na Kampuni kutoka Nje ya Nchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaogharimu zaidi ta Shilingi Trilioni Moja ambao unadaiwa hauna tija kwa Nchi.

UBOVU WA BARABARA ILIYOKUWA IKIWAKABILI WANANCHI WA VULENI WILAYA YA CHAKE CHAKE LIMEPATIWA UFUMBUZI

 

Tatizo la Usafiri la muda mrefu ambao unachangiwa na ubovu wa Barabara uliyokuwa ukiwakabili Wananchi wa Vuleni Wilaya ya Chake Chake limepatiwa uvumbuzi kwa kuanza ujenzi wa Barabara hiyo.

Wakizungumza katika Ujenzi wa Barabara hiyo baadhi ya Wananchi wamesema kujengwa kwa Barabara hiyo na Baraza la Mji Chake kutawasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na tatizo  hila kwani wmekuwa wakishindwa hata kusafirisha bidha zao.

Mapema Mhandisi wa Barabara hiyo Nd. Mohammed Mzee Mohammed amesema ujenzi wa Barabara hiyo utajengwa kwa kiwango cha kifusi ukiwa na urefu wa 250 na ukitarajiwa kumalizika ndani ya wiki moja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Mji Chake Chake Nd. Salma Abuu Hamad amesema ujenzi wa Barabara hiyo nikatika kuondoshea changamoto za Barabara zinazo wakabili Wananchi na kuwaletea maendeleo .

BARAZA LA MANISPAA MAGHARIB A LIMESEMA LITAENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Magharib "A"  Nd. Rashid Mohammed Mahmood amesema atashirkiana na watendaji wa Baraza hilo ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika Wilaya hiyo.

Akizungumza baada ya kuapisha kuwa Meya wa Halmashauri hiyo Mstahiki Meya huyo amesema nguvu za pamoja katika kutekeleza majukumu ya kila siku yatawezesha kufanikisha mipango wanayojiwekea.

Msahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Nd.  Saleh Juma Kinana  amesema yupo tayari kushirikiana pamoja na uongozi wa Wilaya hiyo kwa kuimarisha huduma za usafi katika Miji yote Nchini.

 

UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA NI JAMBO LINALOHITAJIKA KUSHUGHULIKIWA KWA NGUVU KUBWA

Wabunifu Nchini wametakiwa kutumia fursa ya kukutana na Watendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali ili waeleze changamoto mbali mbali zinazo wakabili katika kada hiyo kwa lengo la kuisadia Mamlaka hiyo kutayarisha Mitaala itakayoakisi mahitaji ya Soko la Ajira kwa Viwanda.

Akifungua Mkutano wa siku moja uliowashirikisha Wabunifu wa Viwanda hapa Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dr.Bakari Ali Silima alisema Jamii imekuwa na kilio cha namna ya kupambana na Soko la ajira huku Vijana wengi wakiendelea kulalamika kukosa kazi jambo ambalo linahitajikushughulikiwa kwa nguvu kubwa ili kupunguza na hatimae kuondosha kabisa kulio hicho.

Nae Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dr.Ibrahim Mussa Haroun kutoka Chuo cha South West cha China amesema zipo changamoto nyingi ambazo zinawakabili Wabunifu Nchini ikiwa ni pamoja na namna ya kuandaa filamu,matumizi mazuri ya Camera na hata kukosa hati miliki ya kazi wanazozifanya na kupelekea kutokufaidika na kazi wanazozifanya kwa maarifa yao.

Kwa upande wao Washiriki wa kikao hicho cha siku moja kilichojadili changamoto za Wabunifu walieleza changamoto zao kuwa ni pamoja na taasisi zilizopewa dhamana ya kusimamia ukuaji wa Wabunifu kuwa bado hazijawawezesha wao kufanya vizuri pamoja na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Wabunifu wenyewe ili kuboresha kazi zao.

Mamlaka ya Mafunzo ya Amali kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa linaloshughulikia Elimu na Science  UNESCO  inaendesha mradi wa pamoja wa kuwawezesha Wabunifu wa Viwanda ili waweze kuzalisha kazi ambazozitaleta tija kwa Wabunifu na Nchi kwa ujumla.ambapo kwa upande wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali itasadia kutayarisha Mitaala itakayoakisi mahitaji halisi ya Soko la Ajira.

 

error: Content is protected !!