Daily Archives: January 23, 2020

ZBC NA AZAM MEDIA WAMETAKIWA KUKAA PAMOJA KUJADILI NAMNA YA KUTEKELEZA MKATABA WA MASHIRIKIANO

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Mh.Mwantatu Mbaraka Khamis amelishauri Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kukaa pamoja na Kampuni ya Azam Media kujadili namna ya kutekeleza Mkataba   wa Mashirikiano ili kuleta manufaa ya pande zote mbili.

Mh. Mwantatu ameyasema hayo wakati kamati hiyo ilipofanya  Ziara ya kutembelea  Ofisini za  Azam  Media Jijini  Dar es salaam  kwa lengo la  kujifunza na kubadilisha uzoefu katika utendaji wa shughuli   wa  Vyombo hivyo  amesema ni vyema masharti ya mikataba kwa pande  zote mbili yakazingatiwa pamoja na kuangalia utaratibu  wa kubadilishana uzoefu kwa Wataalamu ili lengo la ushirikiano liweze kufikiwa.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mh. Mahamoud Thabiti Kombo ameishukuru Azam Media kwa Mashirikiano yao mazuri kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utoaji wa Taarifa zao kwa Serikali.

Wakati huohuo Mtendaji Mkuu wa Azam Media  Nd.Tido  Muhando amesema  wamekuwa karibu sana na Serikali zote mbili na kuwapa  Mashirikiano mazuri kwa Serikali na kwa upande wa  ZBC  wamekuwa wakifanya kazi kwa kubadilishana vipindi pamoja na kubadilisha Wafanyakazi pale panapo hitajika kwa lengo la kuongeza Ufanisi

Nae  Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Dkt.Salehe Yussuf  Mnemo  amesema kunahitajika muda zaidi  kwa  Azam Media kuongeza kutoa Taalamu kwa Watendaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar  ZBC   ili lengo lililokusudiwa la kutoa huduma bora iliweze  kufikiwa.

Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii na Watendaji wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale ilipata nafasi ya kutembelea Studio mbalimbali zilizopo Azam Media na kuweza kujifunza kwa vitendo jinsi Studio hizo zinavyoweza kurusha matangazo yake.

 

 

WAKULIMA NCHINI WAMETAKIWA KUBADILISHA MFUMO WA KILIMO

Wakulima Nchini wametakiwa kubadilisha mfumo Kulima na kufuga kwa mazoea na badala yake waaze Kulima na Kufuga kisasa.

Hayo ameyasema  Dk. Ibrahim Mussa wakati wa kuwasilisha mada juu ya changamoto mbali mbali zinazowakabili Wakulima na Wafugaji Nchini  hapo katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Migombani.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa kuwaendeleza Wakulima na Wafugaji kutoka Mamlaka ya Mafunzo ya Amali  Zanzibar  Nd. Abdalla Hambal  Amesema bado wanaendelea kuandaa Mafunzo ambayo yatasaididia kutatua changamoto zinazowakabili makundi ya Wakulima na Wafugaji hapa Zanzibar.

Kwa upande wao Washiriki wa Mafunzo hayo kutoka Taasisi za Wakulima na Wafugaji waliishauri Mamlaka ya Mafunzo ya Mali na Serikali kwamba bado makundi hayo mawili yanahitaji kuangaliwa kwa ukaribu na kushauriwa namna wanavyoweza kubadilisha Kilimo na Mifugo ili kuuondokana na utaratibu wa zamani wa Kufuga na Kulima.

Mafunzo hayo ya siku mbili ya Kilimo Biashara( Agribuisness) na Wabuniufu wa Viwanda ( Creative Industry ) yanasimamiwa na mradi wa pamoja kati ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Science na Elimu  UNESCO

 

 

WATENDAJI WA BARAZA LA MJI PEMBA WAMETAKIWA KUUPITIA KWA MAKINI MWONGOZO WA UFANYAJI BAJETI

Afisa Mdhamini Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Nd. Juma Nyasa Amewataka Watendaji wa Mabaraza Mji na Halmashauri Kisiwani Pemba kuuupitia kwa makini  muongozo  wa ufanyaji wa Bajet  uliopangwa   ili  kufkia vyema malengo ya kupeleka Madaraka kwa Wananchi.

Ameyasema hayo mara baada ya Ufunguzi wa  Mkutano wa siku moja wakujadili muongozo wa ufanyaji wa Bajeti wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka katika ngazi ya Shehia huko Ukumbi wa Baraza la Mji ChakeChake Pemba.

Nae Wakili wa Serikali kutoka  Ofisi ya Rais Tawala  za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Nd.Zainab Khamis Kibwana amewataka watendaji hao kujadili kitaalam muongoz huo sambamba kutoa maoni yao ili kuwasaidia wananchi kuwa na uwelewa katika jamii .

Kwa upande wao watendaji walioshiriki mkutano huo wamesema muongozo huo utakapokamilika utasaidia kurahisisha utekelezaji wa shughuli zao na kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii.

 

 

error: Content is protected !!