Daily Archives: January 23, 2020

BALOZI SEIF AMEZITAKA TAASISI NYENGINE HAPA NCHINI KUENDELEA KUWASAIDIA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema  uamuzi wa Kampuni ya Sigara Tanzania {TCC} wa kuwa karibu na watu wenye mahitaji maalum unapaswa kuendelea kuungwa mkono na taasisi nyengine hapa nchini.

Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati wa mazungumzo yake na uongozi wa ngazi ya juu wa Kampuni ya Sigara Tanzania ambao upo Zanzibar kujitayarisha kutoa msaada wa vifaa tofauti kwa watu wenye ulemavu Visiwani Zanzibar.

Amesema zipo taasisi na Makampuni mengi ndani na nje ya nchi yenye uwezo na fursa kubwa ya kusaidia kundi hilo maalum lakini matokeo yake ni machache mno yanayotenga muda wa kujitolea kufanya hivyo kwa watu hao wenye haki ya kupata huduma kama yalivyo makundi mengine

Balozi Seif aliushukuru na kuupongeza uongozi wa Kampuni ya Sigara Tanzania kwa uamuzi na moyo wake wa kizalendo uliopelekea kuliona kundi hilo la watu wenye mahitaji maalum na hatimae kulisaidia kwa vifaa pamoja na uwezeshaji wa kiuchumi.

Aliueleza uongozi huo wa TCC kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini jitihada za Kampuni hiyo na itajitahidi kuunga mkono katika kuona changamoto zinazoikwaza kampuni hiyo katika harakati zao za kusaidia jamii zinaondoka.

Mapema Mkurugenzi wa Sheria na mahusiano wa Kampuni ya Sigara Tanzania {TCC}

Nd.Godson Kiliza alisema uamuzi wa kampuni hiyo wa kuanzisha mradi wa kusaidia kundi la watu wenye mahitaji maalum ni kurejesha mafidha kwa jamii.

Nd. Godson alisema mradi huo ulioanza kwa takriban mwaka mmoja sasa kwa kushirikiana na serikali kupitia shirikisho la jumuiya ya walemavu nchini umekuwa ukiwapatia vifaa tofauti watu wenye ulemavu.

Alisema vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na Baskeli za Walemavu, Magongo na Fimbo hutolewa sambamba na kuwapatia baadhi ya watu wenye ulemavu vibanda kwa lengo la kuendesha biashara ndogo ndogo ili kukidhi matihaji yao ya msingi.

Alieleza kwamba bajeti yao ya mradi huo kwa mwaka 2019 ambayo ni endelevu inamalizia katika Visiwa vya Zanzibar ambapo jumla ya watu wenye mahitaji maalum wapatao 210 kutoka Unguja na Pemba wanatarajiwa kupata msaada wa baskeli, magongo pamoja na fimbo.

Amesema katika kuunga mkono jitihada za kuuendeleza mradi huo maalum kwa jamii nd.Godson Kiliza alizihamasisha taasisi na Jumuiya za kiufundi zilizopo Zanzibar kuchangamkia tenda ya utengenezaji wa vifaa kwa ajili ya kundi hilo maalum kupitia uwezeshaji wa Kampuni hiyo.

 

 

 

WAFANYA BIASHARA WA SOKO LA KWEREKWE WAMETAKIWA KUTOWA USHIRIKIANO KATIKA KUDUMISHA USAFI

Mkuu wa Soko la mwanakwerekwe Nd. Mcha Ussi Mcha amewataka wafanyabiashara wa Soko hilo kutowa ushirikiano katika kudumisha usafi ili kulifanya Soko  liwe safi na lenye mandhari nzuri.

Akizungumza na ZBC ofisini kwake Mwanakwerekwe Nd. Mcha amesema suala la kudumisha usafi si la Manispaa pekee hivyo kila mfanya biashara anapaswa kuyatunza mazingira katika eneo lake la kazi na kuepuka kuyachafua kwa makusudi kwa kisingizio cha tozo hafifu wanalotoa.

Akielezea suala la miundo mbinu za Soko  hilo ikiwemo mitaro ya kupitishia maji amesema hali ilioko sasa hairidhishi na kuwataka Wananchi kuwa wastahamilivu kwani Serikali iko katika mikakati ya kuliboresha Soko hilo  liwe la kisasa.

Kwa upande wake mfanya biashara wa Soko hilo Nd. Suleiman Salum Suleiman amesema kupanda kwa bidhaa mbali mbali inatokana na upungufu wa bidhaa hizo na pindi zinapokuwa nyingi bei hizo hupunguwa hivyo amewata Wananchi kukubaliana na hali iliopo kwa muda hadi biadhaa hizo zitakapopatikana kwa wingi.

Nae mama lishe anaepika chakula katika Soko hilo Nd. Aisha Ramadhan amesema kupanda kwa tungule, mbatata, vitunguu maji na karoti kunapelekea ugumu katika manunuzi ya viungo hivyo kwa ajili ya shughuli za mapishi na kupelekea kukosa faida kwani huwabidi kuuza chakula chao kwa bei  ya kawaida.

 

MPANGO MKAKATI WA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI NA UDHALILISHAJI KUANDALIWA

 

Wizara ya kazi uwezeshaji  Wazee, Wanawake na Watoto Pemba  imeanda mpango  mkakati ya kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji  unao endelea katika maeneo mbalimbali  Kisiwani Pemba

Akizungumuza na wadau wa vikundi kazi kutoka tasisi na ngos  Kisiwani Pemba, Afisa mdhamini  Wizaraya kazi uwezeshaji  Wazee, Wanawakena Watoto Nd.  Hakimu Vuai Sheni katika ukumbi wa  Wizara hiyo  uliopo Gombani  Chakechake Pemba.

Amesema  kuwa Wizara hiyo imeandaa kamati za kupambana  ukatili na udhalilishaji wa Wanawake  na Watoto, katika maeneo mbali mbali Kisiwani Pemba .

Akizungumuzia lengo lampango kazi huo, Afisa mpango  Wizara ya Kazi uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto ambae pia  ni mratibu wa mradi wa usawa wa kijinsia Nd. Halima Masheko Ali amesema kuwa  dhamira yao  ni kuwapatia   uwelewa wanavikundi kazi,  wa kukabilina na masuala mazima  ya udhalilishaji  katika maeneo yao ya kazi

Kwa upande wao washirikiki wa mafunzo hayo,  wamesema  mipango kazi  ikikamilika itakiwa njia ya kupambana na matendo hayo, ambayo yamekuwa yakiendelea siku hadi siku.

SERIKALI IMETUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MBILI KUWAWEZESHA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUSOMA

Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni Mbili kuwawezesha Wanafunzi wa Elimu ya juu kusoma ndani na Nje ya Nchi

Akisoma ripoti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali   Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Simai Mohammed Said katika kikao cha Uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Elimu kwa robo ya pili ya mwaka 2019/2020 kwa kamati ya Ustawi wa jamii ya Baraza la Wawakilishi amesema fedha hizo zimejumuisha Ada na gharama za Safari ambapo Wanafunzi hao wamefungishwa mikataba maalum ya kurejesha fedha hizo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Mhe. Mwanaasha Khamis ameitaka Wizara hiyo kusimamia Majengo yaliyowekewa Mawe ya msingi katika Shamra Shamra za Sherehe za Mapinduzi ili kuondosha uhaba wa Madarasa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd.Madina Mjaka amewataka Wazazi wa Skuli za Vijijini kuwasimamia Watoto wao katika Masomo na kutowaruhusu kushiriki katika Shughuli Uvuvi na Utalii ambazo zitawakosesha Fursa muhimu ya kupata Elimu.

 

 

 

 

error: Content is protected !!