Daily Archives: January 22, 2020

MAMLAKA YA ANGA TANZANIA NA MAMALAKA YA VIWANJA VYA NDEGE ZANZIBAR KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Mh. Hamza Hassan Juma  amewataka watendaji wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) na Mamalaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kutatua changamoto zinazojitokeza katika masuala yanayohusu wa usafiri Anga kwa lengo kuleta tija kwa pande zote mbili.

Wito huo  umetowa na Mwenyekiti  wa Kamati hiyo wakati walipoitembelea Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) na kuzungumzia juu ya utekelezaji wa suala zima la mapato yatokanayo na uendeshaji  wa Anga kwa upande wa Zanzibar na maendeleo yake amesema ni vyema kwa  mamlaka hizo zikafanya kazi    kwa pamoja  na kuangalia mahitaji halisi  kwa ajili ya utekelezaji wa  miradi mbali mbali unayohusiana na masuala ya usafiri wa anga kwa  maslaahi  ya Taifa.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Nd. Hamza Johari akizungumzia kuhusiana na ufungaji wa rada   amesema ufungaji  huo  umekuja baada ya kufanyika kwa utafiti kwa lengo la kufikia maeneo yote ya Nchi  ambapo rada hizo zimefungwa   katika maeneo ya  Kilimanjaro,  Mwanza, Dare s salaam na Mbeya kwa ajili ya kuimarisha  usalama wa  Anga.

Mkurugenzi   Mkuu wa  Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Zanzibar  Kapteni  Said Ndumbogani  amesema Zanzibar inahitaji  chombo maalum cha kusimamia  usalama wa Anga .

Kamati  ya Ardhi na mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar  ilipata nafasi ya kuitembelea rada  pamaoja na kupokea taarifa juu ya maendeleo  ya rada  hilo iliyopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa  vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es salaam ambapo kamati hiyo uliambatama na watendaji wa Wizara ya Ujenzi Usafirishaji  na Mawasiliano ya Zanzibar.

KAMATI YA MAENDELEO YA WANAWAKE HABARI NA UTALII IMEELEZEA KURIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA WIZARA

Kamati ya maendeleo ya wanawake habari na utalii imeelezea kuridhishwa na utendaji wa Kamisheni ya Utalii, Shirika la Magazeti ya Serikali na Shirika la Wakala wa Uchapaji kwa utekelezaji mzuri wa shughuli zao.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe, Mwantatu Mbaraka Khamis wakati kamati hiyo ilipotembelea mashirika hayo.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar  Nd. Abdallah Juma amesema kwa kipindi cha mwaka 2019 uingizaji wa  wageni umeongezeka  hadi kufikia milioni mia tatu na sabiini ukilinganisha na mwaka 2018.

Kaimu Mkurugenzi wa  idara ya mipango na utawala wa wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar  Nd. Salum Khamis amesema katika  mwaka 2018 hadi 2019 wametekeleza vyema majuku yao pamoja na kuajiri wafanyakazi wapya ishirini na tatu.

Mkurugenzi wa Shirika la Magazeti Zanzibar Nd. Yussuf Khamis amesema  Shirika limefanikiwa kuongeza vifaa mbalimbali ikiwemo computa ,camera na gari ili kuongeza ufanisi kufuatia kuanzishwa kwa Magazeti ya Zanzibar mail na Zaspoti.

 

MABANDA YA WAFANYABIASHARA YALIYOJENGWA BILA YA UTARATIBU KATIKA SOKO LA MWANAKWEREKWE KUVUNJWA

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Hassan Khatib Hassan ametoa muda wa wiki moja kwa Baraza la Manispaa Mjini na Baraza la Manispaa Maghribi ‘B’ kuvunja mabanda ya wafanyabiashara yaliyojengwa bila ya utaratibu katika soko la Mwanakwerekwe na kuliondoa jaa liliopo mbele ya Soko hilo.

Akizungumza katika ziara ya kuangalia ufanyaji biashara katika Soko hilo Mhe. Khatibu amesema kufanywa biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuzagaa kwa taka inaleta usumbufu kwa watumiaji wa soko na kuhatarisha afya za watu.

Amesema iwapo mabaraza hayo yatashindwa kuendesha   masoko Serikali ya Mkoa itasimamia uendeshaji wa Masoko hayo.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa Magharibi “B’ Ali Abdala Natepe wameahidi kuyafanyia kazi maagizo hayo na kuwataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano pale mabanda hayo yatakapovunjwa.

Wafanyabiashara wa Soko hilo wamesisitiza kuwepo kwa usimamizi mzuri wa Soko ili waweze kuendesha biashara zao vizuri.

 

 

 

 

JUMUIYA YA MUZDALIFA IMESEMA ITAENDELEA KUWASAIDIA WANANCHI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Muzdalifa Shekh Farouk Hamad amesema Jumuiya yao itaendelea kuwasaidia  Wananchi wanaoishi katika Mazingira magumu wakiwemo Watoto ili wajisikie kuwa  hawako sawa na Watu wengine.

Akikabidhi Sabuni na Nguo kwa Wananchi wa Shehiya nne (4) za Jimbo la Amaani        Shekh Farouk  s  amesema katika  kufanikisha Azma hiyo  watashirikiana na  Wafadhili na Mashirika mbali mbali likiwemo  la Helping Hand la Marekani.

Amesema Jumuiya yake inaamini kuwa msaada walioutoa utawasaidia kwa kiasi kikubwa Wananchi hao katika kupunguza shida zinazowakabili.

Mkurugenzi  wa Shirika la kujitolea la Helping Hand  Bi Nadia Zeshan  akizungumza na Wananchi wa Shehiya hizo amesema Shirika lake linaridhishwa na namna ya misaada yao inavyotumika.

Baadhi ya Watu walionufaika na msaada huo wameelezera  kufurahishwa na msaada huo.

Shehia zilizopewa misaada ni Shehia ya Wazee, Sebleni, Kilimahewa na shehia ya Amani.

 

error: Content is protected !!