Daily Archives: January 21, 2020

MH. KASSIM MAJALIWA AMEWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUTOZIKATISHA NDOTO ZA WATOTO WAO WA KIKE

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amewataka Wazazi na Walezi kutozikatisha ndoto za Watoto wao hasa Watoto wa Kike kwa kuwakosesha  kwa lengo la kuwakomboa na utegemezi  katika maisha yao ya baadae.

Mh.Waziri Mkuu ameyasema hayo  huko katika Kiwanja cha Skuli ya Daya Mtambwe wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi  mara ya  kukaguwa maendeleo ya ujenzi wa  Chuo cha Amali kilichopo Daya Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema  ni vyema  kulinda ndoto za Watoto   hasa Watoto wa Kike  kwani mara nyingi ndoto  hizo  huwa hazikamiliki kutokana na kukosa Elimu jambo ambalo  linawafanya kuwa tegemezi  katika maisha yao.

Pia Mh.Waziri  Mkuu amesema Serikali inaendelea  kuimarisha  Sekta ya Elimu  kwa  kufanya  mapitio ya  mitaala pampoja na kuimarisha Tehama ili kuendana na  mabadiliko ya Sayansi na Teknologia.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka  Wananchi  kuendeleza Muungano pamoja na  kudumisha  hali ya Amani na utulivu iliyopo Nchini.

Nae  Naibu Katibu Mkuu  Taaluma Bi  Mwanaidi  Mjaka Mwinyi, amesema mradi huo unaojengwa  na  Campuni ya ZECON campaini limited ya tanzania  ulianza rasmi juni 2016   na badala yake ulisimama  kutokana na  kutofahamiana  baina ya  Mkandarasi na msimamizi wa ujenzi  ambae ndie aliyochora mchoro  huo.

 

 

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEANDAA MIKAKATI YA KUWAFUNDISHA WAKULIMA WA ZAO LA MWANI

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa mikakati maalumu ya kuwafundisha Wakulima wa zao la Mwani kutumia mbegu mpya ili kuongeza mapato na uhakika wa soko.

Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali amesema hatua hiyo itasaidia kuondokana na ukulima wa zamani uliokuwa hauna maslahi kwao.

Akifungua mkutano wa siku moja  wa tasisi inayoshughulikia utafiti na sera repoa Balozi Amina amefahamisha kuwa mbegu hiyo mpya ya Mwani awamu ya kwanza ya majaribio inatarajiwa kuvunwa  mwezi ujao.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi inayoshughulikia mambo ya utafiti na sera repoa Dr.Donald Mmari amesema lengo la mkutano huo ni kujadili uzalishaji wa bidhaa bora pamoja na kuuzika ndani ya soko na nje.

SERIKALI IMESEMA ITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO NA SHIRIKA LA MAENDELEO LA FINLAND

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imesema itaendelea  kutoa ushirikiano na Shirika la maendeleo la Finland FIDA  kufanikisha  miradi waliyokusudia kuitekeleza katika Mkoa Mjini Magharibi.

Mkuu wa Mkoa huo Mh Hassan Khatibu Hassan amesema kwa miaka mingi Nchi hiyo imekuwa na mahusiano mazuri na Zanzibar hivyo watahakikisha wanaendeleza uhusiano huo kwa masilahi ya pande zote mbili.

Akizingumza na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Finland na uongozi wa FIDA ameishukuru Nchi hiyo kwa uamuzi wake huo wa kuendeleza sekta muhimu kwa jamii ikiwemo kinamama na Watoto.

Mkuu wa mradi wa FIDA  Zanzibar Nd. Nuru mtema amesema kuwa kwa Zanzibar Shirika hilo litatekeleza miradi ya Elimu, Afya kilimo na kusaidia huduma nyengine muhimu na jamii.

Ujumbe huo upo Zanzibar kwa ziara ya siku tatu na imepata fursa ya kuona na Viongonzi wa skta mbalimbali wakiwa Nchini  ambapo pamoja na mabo mengine  wanangalia namna ya miradi inayotekelezwa na Nchi  hiyo .

 

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR WAMETAKIWA KUTUMIA FURSA ZA KIMASOMO WANAZOPATIWA

Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar kitengo cha ufundi wametakiwa  kutumia muda wao vyema  katika kujifunza masomo kwa kuuliza maswali  mbali mbali ili kuhakikisha wanaelewa kwa makini  ili waweze kutumia  elimu hiyo katika  kurekebisha mitambo ya ZBC

Mkurungenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar  Nd. Chande Omar amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa kitengo cha ufundi kwa kurusha matangazo  kwani Serikali  na wananchi wamekuwa wakitegemea  Shirika hilo kwa kuendesha vipindi mbali mbali .

Amesema Shirika hilo halina uwezo wa kuwasomesha  mafundi  wengi nje ya Nchi hvyo wameona ipo haja  kutafuta waalamu  kutoka China kuja kuwapatia mafunzo hayo kwa muda wa wiki mbili  ili kuweza kurekebisha pale panapo tokea hitilafu.

error: Content is protected !!