Daily Archives: January 20, 2020

VIJANA WAMETAKIWA KUENDELEA KUBUNI MIRADI INAYOTEKELEZEKA NA KUWEZA KUIRUDISHA MIKOPO KWA WAKATI

Vijana wamesisitizwa kuendelea kubuni miradi inayotekelezeka itakayowawezesha kupata mikopo na kuweza kuirudisha kwa wakati.

Wakitoa maoni yao katika mafunzo maalum yaliyoandaliwa na jumuiya ya kuwawezesha vijana kiuchumi ZAFAYCO wadau kutoka sekta mbali mbali za vijana wamesema fursa nyingi hazijafikiwa zikiwemo za kilimo na uvuvi ambazo vijana wanaweza kuzitumia kwa kushirikiana na taasisi za Serikali kupata mikopo  ili kujiinua  kiuchumi.

Muwezeshaji wa mafunzo hayo mshauri wa miradi ya SUZA  Omar Jecha amesema watajitahidi kuishauri Serikali njia zaidi za kupata nyenzo au mifuko zaidi ya kuwainua kiuchumi vijana itakayosaidia kupunguza utegemezi kwa vijana.

SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA JONSON LIMESEMA LITAENDELEA KUSAIDIA MAENDELEO YA NDANI YA NCHI

Shilrika lisilokuwa la Kiserikali la Jonson ik lenye makao Makuu yake Marekani limesema limeamua  kuendelea  kusaidia  maendeleao ya ndani ya Nchi  na kuhakikisha  kila mwananchi anapata  mahitayi  muhimu  kwa kila nsiki

Mkururugenzi  wa shirika  hilo Bibi akizungumza    wakati  wafanyakazi wa Shirika hilo  kuamua kujitolea kusaidia  kituo cha kulelea  watoto mayatima  wanaoishi  Mazizini baada ya kukabidhi uwongozi  wa Mkoa  kutoa msaada wa kituo hicho msaada huo unatokana na mchango wa wafanyakazi.

Amesema lengo la kutoa msaada huo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanatambuliwa la kupata huduma stahiki ikiwemo afya elimu ulinzi na ustawi wa jamii.

Mkuu wa kituo hicho cha kulelea watoto  hao mayatima  Pili Sadala Mussa  amesema msaada  huo  utawasaidia  watoto  hao kulinganisha na mahitaji yao na kuwapongeza wafanyakazi hao kwa uwamuzi huo sambamba na kuyataka mashirikiano mengine  kuiga mfano kama huo.

Baadhi ya wafanyakazi wamesema wataendelea  kushirikiana na wafanyakazi na  Jumuiya  ambazo zimejikita  kusaidia watoto .

 

WADAU WA MAPAMBANO VITENDO UDHALILISHAJI WAMETAKIWA KUBUNI MBINU ZA KUONDOA TATIZO HILO

Wajumbe kati ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi wameviomba Vyombo vya Sheria, Serikali na Wadau wa mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na  udhalilishaji wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto  kubuni mbinu mbadala  za kulimaliza tatizo hili baya Nchini.

Wakizungumza na Uongozi na Wafanyakazi wa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wizara ya Kazi,Uwezeshaji, Wazee,Wanawake na Watoto katika ukumbi wa Afisi hiyo Miembeni wakati wa ziara ya kikazi Afisini hapo wamesema hukumu zinazotolewa na Mahakama ni ndogo na kuwafanya wakorofi wafanyaji wa vitendo hivyo kutoacha na kulifanya janga hili kuendelea kwa kasi kubwa nchini.

Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa chini ya Uongozi wa makamo mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Mussa Haji Foum wamesema sheria ziliopo sasa dhidi ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji hazitotufikisha mbali katika kuondoa kadhia hii.

Mapema akiwasilisha taarifa ya kesi za udhalilishaji kwa kipindi cha mwezi julai hadi disemba, 2019 katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mashtaka Nd. Ibrahim Mzee Ibrahim amesema katika kipindi hicho Afisi imepokea majalada 426 na kuyafanyia kazi majadala 400 kati ya hayo.

Wakieleza mikakati ya wWzara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto viongozi na watendaji wa Wizara hiyo wakiongozwa na Naibu Waziri wake Mhe. Shadya Mohammed Suleiman amesema Wizara inajikita zaidi katika kukinga kuliko kutibu matatizo baada ya matukio.

 

error: Content is protected !!