Daily Archives: January 19, 2020

MH.RAJAB AMEWATAKA WALIMU KUSHIRIKIANA KATIKA KUFUNDISHA ILI KUWEZA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU

Kiwango cha Ufaulu kwa Wanafunzi wa Kidato cha nne kwa Skuli za Wilaya ya Kaskazini b kimeongezeka kutoka wanafunzi 12 kwa mwaka 2018/2019 na kufikia idadi ya Wanafunzi 60 kwa mwaka 219/2020 kati ya Wanafunzi 918 waliofanya mtihani mwaka jana.

Kiwango hicho cha Ufaulu kimeongezeka kutokana na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Walimu pamoja na Uongozi wa Wilaya hiyo kwa kuwa karibu na Walimu pamoja na Wanafunzi kwa kufuatilia kwa kina baadhi ya matatizo na kuyatafutia ufumbuzi  wa haraka.

Akizungumza na Walimu wakuu  na wenyeviti wa kamati za Skuli za Wilaya ya Kaskazini b  .Nd. Rajab Ali Rajab katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kinduni  ambacho kilikuwa na lengo la  kujadili matokeo hayo pamoja na kuandaa mikakati madhubuti kwa Wanafunzi wa Kidato cha nne wanaotarajiwa kufanya mtihani wa taifa mwaka huu.

Amesema ili kiwango cha ufaulu kiongezeke ni vyema kwa Walimu kushirikiana pamoja katika ufundishaji,mkuwa  Pamoja na mitihani ya mara kwa mara  , na kufanya mchujo kwa Wanafunzi  ili kupata Darasa Moja la Wanafunzi wanaoonekana kuwa na uelewa mzuri Darasani

Aidha Nd.Rajab  amezitaka kamati za Skuli kujitathmini katika utendaji wao wa kazi kwani bado jamii imekuwa ikishindwa kutoa ushirikiano kwa Walimu hasa pale wanapotaka kuzungumza matatizo ya Wanafunzi.

Msaidizi Mkurugenzi  elimu Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini  b  Nd.Juma  Haji amesema licha ya kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu lakini bado Walimu Wakuu wanatakiwa kusimamia vyema majukumu yao  kwa kuhakikisha Walimu wanamaliza silabasi zao kwa wakati.

Nao baadhi ya Walimu Wakuu wamesema katika Skuli zao bado kuna matatizo ambayo yanarudisha nyuma jitihada za ufundishaji hasa pale wanapowarudisha  Wanafunzi wenye uelewa mdogo wazazi  wanaenda Skuli na kuwataka kuwapeleka Kidato cha nne hali ambayo inasababisha kuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi waliofeli

JAMII IMETAKIWA KUENDELEA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU

Jamii imetakiwa kuendelea na utamaduni wa kuchangia damu ili kuwasaidia watu wanaohitaji kuongezewa pamoja na kuepuka madhara ya kuwa na damu nyingi mwilini.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa shirikisho la familia kwa ajili ya amani duniani (FFWP) Stylos Leo Simbamwene wakati shirikisho hilo lilipoenda kuchangia damu katika Taasisi ya MMifupa Muhimbili (MOI). ambapo amesema jamii inatakiwa kupatiwa Elimu juu ya faida za kutoa damu kifya na kijamii.

Nae Meneja Mahusiano wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Nd. Patrick Mvungi amesema kwa siku taasisi hiyo inatumia chupa 15 hadi 26 za damu.

Nao baadhi ya wachangiji wa damu wameiomba jamii kuto ogopa kuchangia damu kwani hakuna madhara anayoweza kupata mtu kutokana na kuchangia damu.

Hatu ya taasisi hiyo kwenda kuchangia damu ni mwendelezo wa wadau mbalimbali kuchangia damu katika taasisi ya moi ili kupunguza uhaba wa damu katiaka taasisi hiyo, ambapo  kwa leo zaidi ya watu mia tano wamejitokeza.

 

CCM IMEKEMEA TABIA YA BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA HICHO KUWAANDAA WATU WA KUGOMBEA NAFASI YA UONGOZI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk. Abdallah   Juma Sadala amekemea tabia ya baadhi ya Viongozi wa Jumuiya za Chama hicho kuwaandaa watu wa kugombea nafasi ya Uongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Amesema tabia hiyo  imekuwa inasababisha kuibuka mifarakano fitina na majungu ndani ya Chama hali na kuleta  usumbufu katika utekelezaji wa  kazi zake.

Akizungumza katika kongamano la Mafunzo la kujenga uwezo wa kujua kanuni za maadili kwa Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mjini Zanzibar Dk.Sadala  Amesisitiza umakini na uadilifu katika utendaji kazi kwa vile hakuna mwanachama alie juu ya katiba  ya Chama Cha Mapinduzi.

Aidha ameuomba umoja huo kuendelea kuijenga jamii hasa katika mapambano ya kupiga vita vitendo vya udhalilihsjai ambavyo ni tishio kwa taifa la baadae.

Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi Mkoa wa Mjini Nd. Ali  Othuman Said  pamoja na Katibu wa Jumuiya hiyo Nd. Shemsa Saimon Himbula wamesema jumuia inatambua  juhudi  zinazochukuliwa na Chama Cha Mapinduzi  kupitia ilani yake katika  kuimarisha  maendeleo kwa wananchi wake.

 

 

MTAALA WA ELIMU YA MAANDALIZI NA MSINGI KUREKEBISHWA ILI MTOTO KUWEZA KUPATA ELIMU BORA

Aafisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Mohamed Nassor amesema mtaala wa Elimu ya Maandalizi na Msingi unafanyiwa marekebisho ili kumuwezesha Mtoto kuwa na mazingira mazuri ya kupata elimu.

Amesema hayo huko katika kituo cha Walimu TC  Michakaeni wakati alipokuwa akifungua Semina ya  siku moja ya uwasilishaji wa muundo wa mtaala mpya wa Skuli  za Maandalizi  kwa wadau mbali mbali Kisiwani Pemba.

Amesema Wizara  ina adhma ya kutoa  mtaala ambao utaendana na mfumo  wa sasa wa Elimu  ya Dunia, hivyo amewataka  wadaau hao kushirikiana kwa pamoja katika kuazimisha adhma hio.

Wakiwasilisha muundo wa mtaala huo  Nd. Patima Kheiri Kombo Afisa Mkuza Mitaala  na  Nd.Hafsa Aboud Talib  Mkuu wa Seksheni ya mafunzo   Taasisi ya Elimu Zanzibar  , wamewataka wadau huo kuupitia vyema mtaala  huo na kutoa maoni  ili kuiboresha dhana ya Elimu kwa Watoto wa Kizanzibari.

 

error: Content is protected !!