Daily Archives: January 18, 2020

WALIMU WAMETAKIWA KUFUATA UTARATIBU WA KUWAGAIA WANAFUNZI MABUKU KAMA ILIVYOPANGWA NA SERIKALI.

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini " b"  Nd: Rajab Ali Rajab amewataka Walimu kufuata utaratibu wa kuwagaia Wanafunzi mabuku ya kuandikia kama ulivyopangwa na Serikali.

Akikabidhi mabuku ya kuandikia kwa Walimu wa Skuli hiyo kwa niaba ya Skuli zote za Kaskazini b amesema lengo ni kuondosha usumbufu na mzigo wa wazee kutumia gharama kubwa   kuwanunulia mabuku Watoto wao wanapoanza masomo.

Amesema katika mpango huo Walimu wanapaswa kugaia Wanafunzi kwa  awamu na ni marufuku maabuku hayo kuuuzwa.

Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi Upenja Nd:Hussein Jecha Ali akizungumza kwa niaba ya Walimu wenzake ameahidi kusimaimia Wanafunzi hao kuyatumia mabuku hayo kama yalivyokusudiwa.

 

TUME YA NGUVU ZA ATONIC TANZANIA IMESEMA IMERIDHISHWA NA USIMAMIZI MZURI WA MATUMIZI YA ATOMIC

Tume ya Nguvu za Atonic tanzania imesema imeridhishwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya Atomic kwa baadhi ya vituo vya Hospitali na vituo vya Afya vya Zanzibar.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano   Nd:Peter  Gaitan Ngamilo amesema imefanya ukaguzi katia vituo 24 vya Afya na Hospitali za Unguja na Pemba na kubaini Viwili tu vimeshindwa kufuata utaratibu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema  tume hiyo ina lengo la kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda umma wafanyakazi pamoja na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi.

Mtafiti mwandamizi Tume ya Atomic Tanzania Dr: Suleiman Ameir Suleiman amesema itaendeleza matumizi salama ya Teknolojia ya mionzi ili isiweze kuathiri Taifa.

 

TAASISI ZA UMMA ZIMESISITIZWA KUWEKA BAJETI ZA MASUALA YA UKATILI NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Bi. Fatma Gharib Bilal amesisitiza taasisi za umma kuweka bajeti maalum kuhusiana na masuala ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia zanzibar.

Akizungumza katika kikao cha kamati ya kitaalam ya kuratibu utekelezaji  wa mpango kazi wa kitaifa wa kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na Watoto amesema kufanya hivyo kutarahisisha utekelezaji wa mpango kazi wa masuala hayo.

Katika kikao hicho wajumbe wamepokea na kujadili taarifa za utekelezaji mpango kazi wa kitaifa wa  kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji  wa Wanawake na Watoto kuhusu mazingira wezeshi,kinga na huduma.

WIZARA YA KILIMO IMESEMA KUWA IMEJIPANGA KATIKA UZALISHAJI WA KUTUMIA MBEGU KIDOGO MAVUNO MENGI

 

Wizara ya Kilimo  Mali Asili Mifugo na Uvuvi Zanzibar  imesemesema  imejipanga katika kujiaandaa na  uzalishaji wa kilimo cha kisasa kwa kutumia  mbegu kidogo mavuno mengi ili kuiingia katika ushindani wa kilimo hai.

Akizungumza na  ujumbe wa Wabunge kutoka  Filand  waliokuja  Ofisini kwao kubalishana mawazo na kukagua miradi ilopo katika wirazara hiyo  Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mh: Mmanga  Mjengo Mjawiri  Amesema  umefika wakati wa Wazanzibari kuweza kubadilika katika suala zima la kilimo kwani ndio tui wa  mgongo kwa kila  Nchi.

Amesema jitihada hizo zitakuja  kutokana na kuondokana na changamoto zilizopo  ikiwemo mabadiliko ya tabia Nchi  utoaji wa elimu kwa Wanachi juu ya matumizi ya ukataji wa kuni  na jinsi ya kuondokana na  nzi wa matunda wanao wakabili baadhi ya maeneo  ya mashamba ambapo ufumbuzi wake watapatiwa  kwa njia za mzungumzo kati ya wabunge hao na wenyeji.

Kwa upande wake  mratibu wa mradi  Nd:Nuru Lamek Mtema  amesema ujio wa Wabunge hao kutoka  Filand imekuwa na umuhimu mkubwa kutokana na  kuwa  ukisaidia  jamii katika  masuala  yanayo wakabili.

error: Content is protected !!