Daily Archives: January 17, 2020

WAWEKEZAJI NCHINI WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOWEKWA NA SEREKALI

 

Wawekezaji Nchini wametakiwa  kufuata  sheria na miongozo iliyowekwa na Serekali  ili kujiepusha kuingia katika  makosa ya uvunjifu wa sheria.

Akizungumza na baadha ya Wawekezaji wa Hoteli katika ziara maalumu ,Wilaya ya Kaskazini ‘a’  Afisa uhusiano ZIPA  Abdulla Khamis  Amesema  kuna mamalalamiko kuwa baadhi wawawekezaji wamekuwa vinara wa kutofuata sheria.

Amesema kutokana na tatizo hilo Serikali imeagiza kufanywa Ziara hiyo ili  kuwakumbusha Wawekezaji kuhusu kufuata miongozo ya Nchi.

Akizungumza kwa niaba ya wawekezaji wa Mahaoteli Nd. Devid  kutoka Hoteli ya Oceanic Bell  Amesema kuwa  vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa Mahoteli  sio vizuri na kuwataka  waache tabia hizo kwani   nikuenda kinyume  na sheria.

Baadhi ya Wananchi wa Kijijin i hapo wamekiri kuwepo kwa matatizo hayo kwa baadhi ya wamiliki wa Mahoteli na wameiomba Serikali kutolifumbia macho suala hilo.

Ziara hiyo imefanywa katika  Hoteli za Kijiji cha Matemwe

 

WANAFUNZI WA SKULI ZA SEKONDARI WATAKIWA KUTHAMINI JUHUDI ZINAZOFANYWA KATIKA KUIMARISHA SEKTA HIYO

Wanafunzi wa Skuli za Sekondari watakiwa kuthamini juhudi zinazofanywa na Wadau wa Elimu katika kuimarisha sekta hiyo kwa lengo la kuengeza viwango vya Ufaulu katika mitihani yao.

Sheha wa Shehia ya Mtopepo  Nd.Issa  Ahmada  Akizungumza katika ghafla ya kugawa vitabu kwa Wanafunzi wa Skuli ya Mtopepo Sekondari amesema juhudi mbali mbali za kuimarisha miundombinu ya elimu zinafanywa lakini bado ufaulu wa Wanafunzi hauridhishi hivyo umefika wakati Wanafunzi kujitambua na kuzitumia fursa walizonazo ili waweze kufaulu katika madaraja ya juu.

Mratibu wa mradi wa (RAA )Bi .Bigrit Mitawi amesema lengo la kugawa vitabu hivyo ni kuwawezesha Wanafunzi kuwa nyenzo za kusomea wanaporudi nyumbani na kuwataka kuvitumia vizuri ili lengo liweze kufikiwa.

Mwalimu mlezi wa Skuli hiyo Nd. Khalfan Musaa amesema mradi huo unaojulikana kama “MOBILE LIBRARY ” utamuwezesha Wanafunzi kuazimwa vitabu kwa kipindi cha mwaka mmoja chini ya uangalizi maalumu na kuvirejesha katika kipindi cha mwisho wa mwaka ili waweze kupewa wengine.

Wanafunzi waliopata vitabu hivyo wameahidi kuvitunza na kuvitumia vizuri na kusema vitawasaisdia katika kufanya vyema kwenye mitihani yao.

Katika hafla hiyo jumla ya vitabu 138 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni vimegaiwa kwa wanafunzi 23 wa Skuli ya Sekondari Mtopepo ikiwa ni mkakati maalumu wa kuengeza viwango vya ufaulu katika Skuli hiyo.

UWT MKOA WA KUSINI IMEWATAKA WANWAKE KUJITAMBUA NA KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI.

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania  (UWT)  Mkoa wa Kusini Unguja imewasisitiza Wanwake kujitambua na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi.

Akifungua Mkutano mkuu wa  UWT  ngazi ya Mkoa   Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Kusini Unguja   Nd.Shemsa  Abdalla Ali Amesema kundi halipaswi kuwa nyuma kwavile wana uwezo wa kulisaidia maendeleo ya Taifa.

Amefahamisha kuwa hatua  hiyo itasaidia kujenga  udhubutu kwa  Wanawake kushikilia nafasi mbali mbali za Uongozi ndani ya Chama  na maeneo mengine muhimu ya maamuzi.

Wakisoma Risala ya Jumuiya hiyo wamesma wanakabiliwa na changamoto ya ulipwaji wa ada kwa baadhi ya Wanachama pamoja na uhaba wa vitendea kazi.

Nao Wajumbe hao wameihakikishia Jumuiya hiyo kuwa hawatasita  kutoa ushirikiano kwa Chama  na  Jumuiya  pamoja na kuomba   kutatuliwa baadhi ya masuala yanayowakabil Wanawake ikiwemo   huduma bora za Uzazi .

WALIMU WA SKULI YA MKOTE WAMEIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA MAJI SAFI PAMOJA NA HUDUMA ZA VYOO

 

Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Mkote Wilaya ya Wete wameiomba Serikali na wafadhili kuwasaidia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma za vyoo ili kuwanusuru na maradhi ya mripuko yanayoweza kutokea kutokana na  ukosefu wa huduma hizo.

Wakizungumza na ZBC mara baada ya kufika  skulini  hapo Wanafunzi hao wamesema hivi sasa wamekuwa wakikabiliwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama  sambamba na  huduma ya matundu ya vyoo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Baraza la Mji Wete Amesema changamoto hizo si kwa Skuli ya Mkote tu bali kuna skuli nyengine kadhaa ambazo zinakabiliwa na changamoto kama hizo lakini Baraza linajitahidi kuzitatua Awamu kwa  Awamu.

Skuli ya Mkote ambayo imeanzishwa  mnamo mwaka 2009 ambayo ina Wanafunzi zaidi ya   mia sita  inatumiwa na Watoto  kutoka  Vijiji visivyopungua sita kama vile Buyuni, Madaniwa na Utaani.

 

error: Content is protected !!