Daily Archives: January 15, 2020

TIMU YA MTIBWA IMETWAA UBINGWA WA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI YA 56 KWA KUICHAPA SIMBA 1-0

 

Mtibwa Sugar imetwaa ubingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi ya 56 kwa kuichapa Simba kwa bao moja kwa bila mchezo uliopingwa Uwanja wa Aman saa 2:15 usiku wa jana.

John Bocco, pamoja na kiongozi wa Simba Nahodha wa timu ya Simba amesema haikuwa bahati yao kushinda kombe la Mapinduzi mbele ya Mtibwa Sugar.

Kocha wa Mtibwa na Nahodha wa Kikosi hicho wamesema haikuwa rahisi kuifunga Simba katika hatu hiyo ya Fainali.

 

TIMU YA WILAYA YA MJINI IMEBEBA KOMBE KATIKA MASHINDANO YA ZBC WATOTO MAPINDUZI CUP 2019/2020

 

Timu ya Wilaya ya Mjini imebeba Kombe katika  Mashindano ya ZBC Watoto Mapinduzi Cup 2019/2020 kwa kuifunga timu ya Wilaya ya Kusini kwa mabao  2 – 0.

Mchezaji Moh’d Salum  alikuwa ndie kinara wa mchezo huo kwa kufunga magoli yote mawili  ambapo bao la kwanza aliliweka wavuni  dakika ya 43 na la pili   dakika ya 89, mtanange uliopigwa kwenye kiwanja cha Mao ze Doung.

Mashindano ya ZBC  Watoto Mapinduzi Cup yamezishirikisha timu 11, timu 4 kutoka Pemba na timu saba za Unguja.

MHE. MWANTATU AMESISITIZA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI KUFUATA SHERIA ZA KAZI ILI KUEPUKA MIGOGORO

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Mhe. Mwantatu Mbarak Khamis Amesisitiza Waajiri na Wafanyakazi kufuata sheria za kazi ili kuepuka migogoro katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza mara baada ya kupokea ripoti ya utekelezaji ya Kamisheni ya Kazi, kwa kipindi cha Julai hadi Disember 2019 amesema Serikali imeweka Sheria hizo kwa taasisi za Serikali na Binafsi  ili kuweka taratibu na kanuni za utekelezaji wake.

Mapema Kamishna wa kazi Zanzibar Fatma Iddi Ali  akiwasilisha ripoti kwa kamati hiyo amesema Kamisheni imekagua taasisi 195 binafsi kufuatilia ulipaji wa kima kipya  cha mshahara ambapo taasisi 165 zinaendelea kulipa kima hicho, 30 zimepelekewa amri ya utekelezaji ambapo 23 zimetii amri, na saba zitapelekwa Mahakamani baada ya utaratibu wa sheria kukamilika.

Kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na ada ya vibali kwa wafanyakazi wa kigeni kwa mwezi wa Julai hadi Disember 2019 Bi Fatma amesema zaidi ya Shilingi Milioni mia mbili sabini na nane zimekusanywa

 

VIONGOZI NA WANACHAMA WA SACCOS NCHINI WAMETAKIWA KUFANYAKAZI KWA USHIRIKIANO NA UADILIFU

 

Viongozi na Wanachama wa vyama vya Akiba na mikopo (Saccos) nchini wametakiwa kufanyakazi kwa ushirikiano na uadilifu    ili vyama hivyo viweze kuwa endelevu     na kufikia malengo yake.

Hayo ameyaeleza   Mwenyekiti  wa kamati ya Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi  Mhe. Mwantatu Mbarak wakati kamati hiyo   ilipotembelea taasisi ya fedha ya Wanaushirika ya Faraja Union Limeted iliopo Kisiwandui   Mjini Zanzibar.

Amesema taasisi hizo za fedha ni chombo muhimu hivyo masuala hayo ni ya kuzingatia pamoja na kuwa na lugha nzuri katika utoaji wa huduma .

Naye Katibu  wa Faraja Union Limeted Omar Juma Said amesema taasisi  yake ina wanachama 16 ambao ni Saccos na vyama vya ushirika kutoka unguja na pemba.

Amesema lengo la taasisi  hiyo  ni kupata nguvu ya pamoja ili kutowa mikopo itayoelekeza kwenye uwekezaji wa kati ,kilimo na uvuvi kwa wanachama wake . Faraja Union Limited imezinduliwa tarehe  7/1/2020.

 

 

error: Content is protected !!