Daily Archives: December 12, 2019

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KUTOA HUDUMA BORA NA ENDELEVU KWA MASLAHI YA NCHI NA WANANCHI.

Wizara ya fedha na mipango imesema itaendelea watendaji wa Wizara hiyo katika utendaji wao wa kazi kulingana na mkataba ya huduma kwa wateja ili kutoa huduma bora na endelevu kwa maslahi ya nchi na wananchi wake.

Mkurugenzi uendeshaji na utumiashi wa wizara hiyo Ali Bakar Is-haka akifungua mkutano wa mapitio ya mkataba wa utoaji huduma kwa umma amesema mkataba huo umeweka wazi majukumu wajibu na haki katika kuwahudumia wananchi hivyo utekelezaji wa majukumu kupitia mkataba huo kutasaidia kuondoa malalamiko kwa wananchi.

Akiwasisha mada juu ya umuhimu wa mkataba wa huduma kwa wateja afisa uchambuzi kazi mwandamizi kutoka ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala bora Othman Simba Makame amezishauri taasisi za Serikali kufanya mapitio ya mikataba yao kila mwaka ili kuboresha mapungufu yanayojitokeza katika utoaji wa huduma.

Washiriki wa mkutano huo wamesema licha ya elimu waliyoipata bado kuna umuhimu mkubwa wa kuufikisha mkataba huo kwa wananchi ili ili kuwajengea uwezo wa kujenga hoja katika katika kutetea haki zao pale wanaponyimwa huduma wanazostahiki.

 

RIPOTI YA UMASIKINI WA WATOTO KUZINDULIWA ZANZIBAR

Ofisi ya mtakwimu mkuu wa Serikali Zanzibar imezindua ripoti ya umasikini wa watoto inayoonesha watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 katika meneo ya vijijini bado wanaishi katika hali ya umasikini zaidi.

Ripoti hiyo inayotokana na taarifa ya utafiti wa mapato na mtumizi ya kaya ya mwaka 2014/2015 imeangalia viashiria vya afya, chakula, elimu, maji, makaazi na upatikanaji wa habari kwa watoto ambapo kaya zinazoongozwa na wanawake ni masikini zaidi kulinganishwa na zile zinazoongozwa na wanaume.

Akizundua ripoti hiyo naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha na mipango Iddi Haji amesemamatokeo hayo yatasaidia sekta husika kutathmini utekelezaji wa mipango kuhusu upatikanaji wa huduma bora kwa makundi yote ya jamii.

Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa ripoti hiyo mtakwimu mkuu wa Serikali Bi Mayasa Mahfoudh amesema taarifa hizoza hali ya umasikini wa watoto umetokana na mahitaji ya uchambuzi wa taarifa zilizokuwemo katika  ripoti ya jumla ya utafiti huowa mapato na mtumizi ya kaya ya mwaka 2014/2015.

Mwakilishi wa shirika laUNICEF walisaidia kuandaliwa kwa ripoti hiyo Bi Maha Damaj amesema utafiti umebaini kiwango cha umasikini unatofautiana kwa mujibu wa umri wa watoto.

Bohari kuu ya dawa zanzibar imeandaa mafunzo maalum ya lugha za alama kwa wafanyakazi wake

Katika kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinapatikana katika sekta zote bohari kuu ya dawa zanzibar imeandaa mafunzo maalum ya lugha za alama kwa wafanyakazi wake ili viziwi wapate haki zao za msingi katika taasisi hiyo.

Katika ufunguzi wa mafunzo hayo katibu mkuu Wizara ya afya Bi Asha Ali Abdalla amesema wafanyakazi wanapaswa kufahamu tofauti zinazowakwaza watu wa makundi mbali mbali katika kupata huduma muhimu kama zile za afya na mawasiliano ya kawaida ili kupata jamii jumuishi.

Mkurugenzi bohari ya dawa Nd. Zahran Ali Hamad amesema mafunzo hayo yana lengo la  kupunguza matatizo yanayowakumba viziwi katika kupata muhimu ya afya na kuendeleza utumishi na utawala bora nchini.

Mwenyekiti wa chama cha viziwi CHAVITA Bi Asha Ali wameishukuru taasisi hiyo kwa kufanya mafunzo hayo na kusema ana matumaini kwa taasisi na jumuiya nyengine kufanya mafunzo hayo kwa watendaji wao ili kupunguza matatizo kwa viziwi wanapotaka huduma muhimu

 

VIJANA WALIOPATIWA MIKOPO YA ELIMU YA JUU WATAKIWA KUREJESHA FEDHA HIZO KWA WAKATI

Afisa mdhamini Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Mohamed Nassor amewataka vijana waliopata mikopo ya elimu ya juu kurejesha fedha hizo ili ziwanufaishe wanafunzi wengine.

Akifungua mafunzo mkutano wa kujadili mikakati ya urejeshaji wa mikopo kwa maafisa utumishi na wahasibu katika ukumbi wa Baraza la mji Chake Chake, mdhamini Mohamed amesema marejesho ya mikopo hiyo  hayaridhishi.

Kwa upande wake mratibu wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu Zanzibar ofisi ya Pemba Ahmada Omar Juma amesema mashirikiano yanahitajika kwa kila taasisi ili wanaodaiwa warejeshe fedha hizo kwa wakati.

Akiwasilisha mada ya marejesho ya mikopo, meneja wa mikopo Abudu Issa Khamis amesema wadaiwa 2,648 wanafuatiliwa ili waanze marejesho ya mikopo yao.

Nao washiriki wa mkutano huo wameishauri bodi ya mikopo kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara maofisini na wasisubiri kupelekewa taarifa ofisini kwao.

 

 

error: Content is protected !!