Daily Archives: December 11, 2019

DKT. SHEIN AZINDUA NYUMBA YA MAKAAZI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dkt. Ali mohamed shein amezindua nyumba ya makaazi ya mkuu wa mkoa wa mwanza na kupongeza juhudi kubwa zilizochukuliwa katika ujenzi wa nyumba hiyo.

Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hafla fupi ya uzinduzi wa nyumba ya makaazi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza iliopo, Isamilo Jijini Mwanza.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alisema kuwa ujenzi huo wa nyumba ya makaazi ya Mkuu wa Mkoa huo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha makaazi ya kiongozi huyo yanakuwa bora zaidi.

Alieleza kuwa juhudi hizo zilizochukuliwa katika ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa pia, itasaida kwa wageni watakaomtembelea Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza pamoja na yeye mwenyewe kuishi na familia yake.

Rais Dk. Shein alipongeza juhudi zilizochukuliwa katika kuhakikisha nyumba ya Mkuu wa Mkoa iliyokuwa hapo kabla kwenye mtaa wa Machemba, Isamilo hivi sasa imegeuzwa Ikulu Ndogo.

Hivyo, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Mwanza kwa kupata Ikulu Ndogo kwenye nyumba hiyo ambayo kwa maelezo ya Rais Dk. Shein ina historia kubwa.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alitoa pongezi kwa uongozi wa Mkoa huo pamoja na Mkandarasi wa nyumba hiyo.

Mapema Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo alimueleza Rais Dk. Shein kuwa mradi wa ujenzi huo ulianza kutekelezwa katika bajeti ya mwaka 2017/2018 baada ya nyumba aliyokuwa akiishi Mkuu wa Mkoa huo kubadilishwa matimizi na kuwa sehemu ya Ikulu Ndogo.

Aidha, alisema kuwa Mkataba wa ujenzi ulisainiwa tarehe 13 Juni, 2017 kati ya Mkandarasi Wakala wa Majengo (TBA) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa gharama ya TZS Milioni 660.

Aliongeza kuwa Mkataba wa ujenzi huo ulihusisha ujenzi wa nyumba kuu, nyumba ya wasaidizi, ujenzi wa uzio pamoja na kibanda cha walinzi.

Katibu Tawala huyo alieleza kuwa Mkandarasi alianza ujenzi mwezi Septemba 2017 baada ya malipo ya awali ya kiasi cha fedha TZS milioni 150 zilizokuwa zimepangwa  kwa ajili ya ukarabati wa iliyokuwa nyumba ya Mkuu wa Mkoa na kubadilishwa kuwa Ikulu Ndogo.

Hata hivyo, kwa maelezo ya Katibu Tawala huyo baada ya ongezeko la gharama za vifaa vya ujenzi Mkandarasi aliongezewa kiasi cha fedha TZS milioni 50 kukamilisha shughuli za ujenzi wa uzio na ununuzi wa baadhi ya vifaa.

Sambamba na hayo Katibu Kadio alieleza eleza kuwa kwa sasa ujenzi wa mradi huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 99 ambapo kazi ya ujenzi wa kibanda cha walinzi bado haujakamilika na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dk. Severine Mathias Lalika kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo alimpongeza Rais Dk. Shein kwa kuwazinduliwa jingo lao hilo na kusema kuwa ujio wake umewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha ujenzi huo unakwenda kwa kasi na kufikia malengo yaliokusudiwa.

Hafla hiyo pia, ni miongoni mwa shamrashamra za sherehe za kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri Tanzania Bara.

WANANCHI WAMESISITIZWA KUTODHARAU USALAMA WA AFYA ZA WATOTO NA KUWAPATIA CHANJO

Wananchi wa Wilaya ya kaskazini B wamesisitizwa kutodharau usalama wa afya za watoto na kuwapatia chanjo mbalimbali za  kuwalinda na maradhi.

Katibu tawala wilaya ya kaskazini B Makame Machano Haji amesemaiwapo wazazi watalitilia umuhimu  chanjo watapunguza vifo vya watoto kwa asilimia 23.

Ameeleza hayo katika utoaji wa matone ya vitamin a na dawa za minyoo kwa watoto   kuanzia umri wa miezi sita hadi miezi 59 wa wilaya ya kaskazini B huku akisisitiza suala la lishe bora kwa watoto ili kuwa nusuru pia na utapiamlo.

Daktari dhamana wa halmashauri wilaya ya kaskazini B Dr.Daniel Fransis Pius amesema lengo la halmashauri hiyo ni kuhakikisha wanawakinga watoto ili kuwa na afya njema.

Baadhi ya wazazi wa watoto waliopatiwa matone ya vitamin A na dawa za minyoo wamesema wamenufaika kujua mbinu bora za afya za watoto wao na vyakula vinavyohitajika kupewa katika ukuwaji wao.

MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA ENEO LA KINAZINI

Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imekabidhi zaidi ya tani tano za mchanga na matofali yaliyotengenezwa bila ya kibali kwa idara ya misitu na rasilimali zisizorejesheka katika ziara ya kushtukiza katika eneo la Kinazini.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Hassan Khatib Hassan amechukua hatua hiyo katika ziara ya kushtukiza katika eneo la Kinazini na kubaini kuwepo shughuli za upigaji wa matofali na uchimbaji wa mchanga kinyume na utaratibu.

Amesema kumekuwa na vitendo vya uharibifu wa uchimbaji wa mchanga katika maeneo ya bahari na koko kinyume cha sheria na kusababisha  uharibifu wa mazingira na kuutaka  uongozi wa idara ya misitu na rasilimali zisizorejesheka kuimarisha doria za mara kwa mara katika maeneo hayo.

Katika hatua nyengine katika ziara hiyo uongozi wa Serikaali ya mkoa mjini kwa kushirikiana jeshi la polisi na kikosi maalum cha ulinzi cha idara ya misifu imewakamata vijana wawili walitajwa kwa majina mzee ali mussa miaka 25 na isaa sharifu issa 30 wakaazi wa kwamtipura kwa kujihusisha na ukataji wa miti kinyume na utaratibu.

 

ZANZIBAR IMENUFAIKA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO LA MUHOGO

Zanzibar imenufaika kuongeza uzalishaji wa zao la muhogo kufuatia utekelezji wa mradi wa utafiti wa muhogo na viazi kwa nchi za Afrika .

Naibu katibu mkuu Wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi anaeshuhulikia kilimo na maliasi Masura Mossi Kasim amesema utafiti huo umewezesha uzalishaji wa zao hilo kufikia tani zaidi ya laki moja kwa mwaka.

alikuwa akifungua mkutano wa mkutano wa mwaka wa watafiti zao la muhogo kutokanchi kumi na mbili duniani.

Mkuu wa utafiti wa zao la muhogo Tanzania Mwombeki Winston amesema lengo la mkutano huo ni kuendelea kuwawezesha wakulima  kulima kibiashara na kupata faida zaidi.

 

error: Content is protected !!