Daily Archives: December 6, 2019

MH.MJAWIRI AMESISITIZA KUTEKELEZWA KWA VITENDO SUALA LA UHIFADHI WA WANYAMA PORI

Waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi Mh Mmanga Mjengo Mjawiri amesisitiza kutekelezwa kwa vitendo suala la uhifadhi wa wanyama pori kwa maslahi ya Taifa.

amesema utajiri wa Zanzibar wa kipaumbele ni pamoja na kuwepo wanyama hao na makaazi yao wanaohifadhiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za uhifadhi nchini.

Waziri mjawiri ameeleza hayo katika uzinduzi wa kanuni ya mazizi ya wanyama pori zanzibar ambapo viongozi wa idara ya misitu na maliasili zisizorejesheka wamesema idara hiyo haitasita kumchukulia hatua mmiliki wa zizi la wanyama asifuata sheria.

 

WALIMU VITUO VYA ELIMU MBADALA WAMETAKIWA KUTUMIA MBINU ZA KITAALAMU KATIKA UFUNDISHAJI

Walimu wanaofundisha vituo vya elimu mbadala na watu wazima wametakiwa kutumia mbinu za kitaalamu katika ufundishaji ili vijana wanaomaliza mafunzo hayo waweze kujitegemea.

Wito huo umetolewa skuli ya maandalizi Madungu na katibu tawala Mkoa wa Kusini Pemba Abdalla Rashid  wakati akifungua mafunzo ya mbinu za ufundishaji kwa walimu wa kituo cha elimu mbadala na watu wazima cha Wingwi.

Amesema vituo hivyo vimeamzishwa kuwawezesha vijana kujitegemea katika nyanja tofauti na kwamba ni tofauti kubwa na vijana wanaomaliza vyuo vikuu.

Mapema akielezea lengo la mafunzo hayo, Mkurugenzi wa idara ya elimu mbadala na watu wazima Mashavu Ahmada Fakih amesema yapo mapungufu kwa walimu wanaofundisha vitu hivyo.

Nao washiriki wa mafunzo hayo, wamekiri kukosa mbinu za ufundishaji kama inavyotakiwa.

 

MAMLAKA YA VIWANJWA VYA NDEGE ZANZIBAR KUTOA ELIMU KWA MASHEHA

Mamlaka ya viwanjwa vya ndege Zanzibar imeanza mkakati wa kutoa elimu kwa Masheha juu ya usalama wa wafanyakazi na utendaji mamlaka hiyo.

Mpango huo ni katika kuhakikisha watendaji wanaoomba ajira  katika mamlaka hiyo wanakuwa waaminifu ili kuepusha  uhalifu hasa katika maeneo ya viwanja vya ndege ambavyo ni njia kuu ya kuingia wageni mbalimbali Zanzibar.

Baadhi ya maafisa wa mamlaka ya viwanjwa vya ndege Zanzibar wakizungumza na   baadhi ya Masheha wa Mkoa wa Kusini Unguja  wamesema suala la usalama katika viwanja vya ndege ni muhimu  kwani uhalifu wowote utakaotokezea inaweza kuijenegea sifa mbaya Zanzibar  inayotegemea pato lake kwa sekta ya utalii.

Baadhi ya Masheha hao wamesema elimu hiyo imewaidia kufahamu mbinu za kuhakiki wakaazi hasa katika kubaliana na watu wasiofuata taratibu za kisheria  za kuomba kazi.

 

error: Content is protected !!