Daily Archives: December 2, 2019

SERIKALI YAPANGA MIKAKATI KUTOKOMEZA MARADHI YA UKIMWI IFIKAPO 2030

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh: Mihayo Juma Nh’unga ameitaka jamii     kuendeleza mapambano ya ukimwi kwa kunusuru maambukizi mapya ili lengo la Serikali la kutokomeza maradhi hayo ifikapo mwaka 2030 liweze kufikiwa.

Mh: Nunga ametoa kauli hiyo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani  huko viwanja vya Mpika Tango Mkoani. Kutojisahau kutokana na kupungua kwa kasi ya maambukizi ya Ukimwi Zanzibar na  badala yake

Akitoa taarifa ya hali ya Ukimwi Zanzibara mwenyekiti wa bodi ya tume ya ukumwi Dk Salhiya Muhsin amesema  hadi kufikia mwezi september  mwaka huu juhudi kubwa zimefanywa kutoa elimu , kuhamasishwa wananchi kupima vvu  na kutambua afya zao  na kuleta mafanikio .

akitoa salamu kutoka kwa washirika wa maendeleao mwakilishi kutoka shirika la umoja wa mataifa kitengo cha ukimwi  kanda ya Zanzibar  George Lay ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk Shein kwa mafanikio yaliyopatikana na kuiwezesha Zanzibar  kubaki asilimia ndogo ya kutokomeza maradhi ya Ukimwi ikilinganishwa na nchi  yengine za Afrika.

Katika risala ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi iliyosomwa na Zahira Salim wameelezea wasiwasi wao baada ya wafadhili wao kumaliza muda wao huku wakiimba Serikali kubeba jukumu la kuwapatia mahitaji yao.

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh:  Hemed Suleiman Abdalla amesema hali  halisi ya takwimu za ukimwi zinaonyesha bado ipo haja kwa jamii kujenga utamaduni kwa kupima na kujua afya zao.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Issa Juma Ali ametumia maadhimisho hayo kutoa tahadhari kwa watoto wa kike na akinamama kujiepusha na vitendo vya udhalilishaji katika msimu huu wa uchumaji wa zao    karafuu.

Maadhimisho hayo yalianzia kwa  shamra shamra mabali mbali pia   wananchi wameshiriki katika kupima afya zao,kuchangia damu kwa hiari ambapo ujumbe wa mwaka huu ni jamii ndio msingi wa mabadiliko dhidi ya Ukimwi.

 

 

WAZAZI NA WALEZI WAMESHAURIWA KUFUATILIA NYENDO NA TABIA ZA WATOTO WAO.

Wazazi na walezi wameshauriwa kufuatilia nyendo na tabia za watoto wao ili  wakue katika maadili mema na kuwaepusha na wimbi la udhalilishaji linaloiathiri jamii.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mama Asha Suleiman Iddi alisema hayo katika shughuli ya maghafali ya kwanza ya skuli ya Fat-hi International Community iliopo Shangani  ilioambatana na zoezi la kuwakabidhi vyeti na kuwapongeza wanafunzi  waliomaliza ngazi ya maandalizi  { kg-ii}.

Mama Asha alitumia fursa hiyo kwa kuwashajiisha na kuwasisitiza wazazi kutenga muda wao kwa kuchunguza tabia za watoto wao zitakazowasaidia kugundua mabadiliko yoyote  mabaya yaliyowazunguuka na kwa haraka  kuyapatia ufumbuzi unaostahiki.

Aliwaeleza wazazi na walezi kuwa elimu ina mchango mkubwa katika kujenga mustakabali wa maisha ya watoto. Hivyo kuna kila sababu kwa wazazi kutumia jitihada zao zote katika kuwarithisha elimu watoto wao ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.

Mke huyo wa Makamu wa Pili wa Rais aliwapongeza waanzishi  wa skuli binafsi nchini kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  katika kuinua kiwango cha elimu bila ya kujali ukubwa wa gharama wanazozitoa kwa lengo la kuwafinyanga watoto.

Akisoma risala mwalimu wa skuli ya Fat,hi International Community  ndg. Sheha Ngweshani alisema skuli hiyo  imepata mafanikio makubwa kutokana na watoto wanaosoma katika skuli hiyo wana uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuhesabu sambamba na kuwajenga wanafunzi katika silka na desturi za mzanzibari.

Mwalimu Sheha Ngweshani alimueleza mama Asha kuwa ingawaje yapo mafanikio yaliofikiwa lakini bado inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo kukosekana kwa vifaa kama vile fotokopi na kompyuta vifaa ambavyo vinakwenda sambamba na ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia.

Nae naibu katibu mkuu taaluma kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar  ndg. Madina Mjaka Mwinyi alisema  ushirikiano unahitajika baina ya wazazi, walezi na walimu katika kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira wezeshi kwani kufanya hivyo ndio njia pekee ya kuwajenga watoto wakiwa katika hatua ya awali.

Alifafanua kwamba Serekali ya Mapinduzi  Zanzibar itaendelea kutoa elimu kuanzia ngazi maandalizi, msingi na sekondari,  hivyo skuli binafsi nazo zina wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo.

Katika shughuli hiyo ya maghafali mama asha aliahadi kuchangia vifaa kama vile kopyut na printa ili kutatua miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wanaosoma katika skuli hiyo ya fat-hi international comuunity.

 

 

 

 

error: Content is protected !!