Daily Archives: November 27, 2019

ANGOZA IMEANDAA TAMASHA MAALUM LA KUWASHAJIHISHA WANAWAKE

Mwanvuli wa Asasi za kiraia Zanzibar  ANGOZA  umeandaa  tamasha maalum  lenye  lengo  la  kuwashajihisha  wanawake  kutumia  fursa  ziliomo  katika  uchaguzi  mkuu  wa  mwaka  2020.

Tamko  hilo  limetolewa  na  Mwenyekiti wa ANGOZA  Asha  Aboud ambapo amesema  imebainika  kuwa  bado  kuna  kundi  kubwa  la  wanawake  ambao  wanakosa  kutumia  fursa  ziliopo  katika uchaguzi  kutokana  na  mambo toafuti lakini  zaidi   ni  kukosa  uelewa  wa  namna  ya  kuingia  katika  nyanja  za  uchaguzi .

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari   amesema katika tamasha hilo mada tatu zitawasilishwa ikiwemo uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu ambapo asasi za kiraia na sekta binafsi zitapata nafasi ya kutoa uelewa wao.

Mkurugenzi mtendaji waANGOZA Mw. Hassan Khamis amesema dhamira ya kufanya tamsaha hilo  ni kuutambulisha umma jinsi ya kazi zinazofanywa na angoza katika kuleta  mabadiliko  chanya na  kuleta  maendeleo katika jamii  na Taifa.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili likiwashirikisha washiriki wapatao 130 likiwa na kauli mbiu nafasi ya asasi za kiraia katika kukuza democrasia na maendeleo Zanzibar.

 

error: Content is protected !!