Daily Archives: November 15, 2019

WAGONJWA WA SUKARI WATAKIWA KUFUATA UTARATIBU WA VYAKULA WANAOPEWA NA WATAALAMU WA AFYA.

Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amewaka wagonjwa wasukari kufuata utaratibu wa vyakula wanaopewa na wataamu wa afya ili kulinda afya zao.

Akizungumaza katika maadhimisho ya siku ya ugonjwa sukari Mhe. Mahmoud  amesema serikali kupitia wizara ya afya imeweka utaratibu wa kuwapatia huduma ya afya wagonjwa wa maradhi hayo ikiwemo kuwapatia dawa na maelekezo ya utumiaji wa vyakula jambo litasaidia kuimarisha afya zao.

Mratibu wa umoja wa wagonjwa wa sukari Bi Mkasi Mohamed amesema umefika wakati kwa Wananchi hasa Wazee kuitikia wito katika kupata huduma za matibabu zinazotolewa bure katika shehia zao.

Wananchi Mzee Juma Ali na Bi Asya Shaban wameiomba Serikali kuendelea kuwasaidia Wazee kwa kuwapa huduma mbali mbali huku wakiwashauri wananchi kuwa na tabia ya kuchunguza afya zao ili kupata matibabu mapema.

 

ZBS KUANZISHA UKAGUZI NA UTOAJI WA ALAMA ZA UBORA WA VIWANGO KWA VIFAA VYA UJENZI.

Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya viwango Zanzibar ZBS Bi Khamisa Mmanga Makame amesema taasisi hiyo itaanzisha ukaguzi na utoaji wa alama za ubora wa viwango kwa vifaa vya ujenzi vinavyoingia na vinavyotengenezwa Visiwani  humu ili  kuimarisha sekta ya ujenzi

Akizungumza katika Semina ya mafunzo ya utengenezaji wa Matofali kwa Wakandarasi na Wamiliki wa Viwanda Bi Khamisa amesema kutokana na kukua kwa sekta ya ujenzi  taasisi hiyo imeamua kuelekeza nguvu zake katika sekta hiyo ili kuwa na Majengo imara.

Mkurugenzi wa ZBS amesema wameanza kuimarisha mifumo yao ya ukaguzi na utoaji wa viwango kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya Zanzibar ili ziweze kushindana katika soko la Kimataifa.

Washiriki wa semina hiyo wameitaka ZBS kushirikiana na Idara ya Misitu, Mazingira na wadau wa ujenzi katika kutatua matatizo katika sekta ya ujenzi ikiwemo upatikanaji wa Mchanga.

Muezeshaji katika semina hiyo Mhandisi Danford Semwenda amewataka wamiliki wa Viwanda vya matofali kuchukua tahadhari kwa wafanyakazi wao kwa kuwapa vifaa vya kinga kuepusha majanga.

 

KUWEPO KWA CHANGAMOTO KATIKA UPATIKANAJI WA TAKWIMU.

Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali imesema inakabiliwa na changamoto kubwa katika upatikanani wa Takwimu zilizo rasmini  katika  kutathmini mipango mbali mbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Mkurugenzi huduma za jamii  Khadija Khamis Khatibu alisema hayo katika mafunzo ya utoaji na utumiaji wa takwimu  kwa watendaji wa Serikali amesema  mbali na juhudi zinazochukuliwa na Ofisi hiyo  katika kupanga mipango yake lakini kuna baadhi ya tasisi za Serikali zimekuwa hazitowi ushirikiano katika upatikana wa takwimu zilizo rasmin.

Akiwakilisha mada juu ya upatikanai wa Takwimu rasmini afisa kutoka takwimu Asia Hassan Mussa kuwepo vitengo vya Takwimu katika tasisi za Serikali kutawezesha Ofisi ya Takwimu kuweza kukusanya Takwimu  kwa urahisi .

Wakichangia baadhi ya washiriki wamesema kumekuwa na tafauti katika upatikanaji wa Takwimu katika tasisi za Serikali na mtakwimu mkuu hivyo ni vyema kuwepo na mfumo umoja ambao utaziozesha takwimu zote  ziwe sahihi.

Mafunzo hayo ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho  siku ya Takwimu Afrika ambapo ujumbe wa mwaka huu takwimu zenye ubora ni muhimu katika kuhakikisha usimamizi mzuri wa uhamaji wa lazima ktika bara la Afrika.

WIZARA YA KAZI INA MIPANGO WA KUWAPATIA AJIRA ZA STAHA KWA VIJANA.

Wizara ya Kazi, uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto imesema mipango na jitihada za taasisi za serikali na binafsi katika kuwapatia  ajira za staha vijana wengi zaidi nchini zinaleta matunda kufuatia utendaji mzuri wa kamati za ajira za wilaya nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia masuala ya Kazi na uwezeshaji Bi Maua Makame Rajab akifungua mkutano wa kamati za kisekta za uzalishaji ajira za Wilaya tatu (3) za Mkoa wa Mjini Magharibi amesema hali hiyo imehamasisha vijana kuondoa vikwazo vinavyowakabili  kufikia malengo yao

Amefamisha kuwa wizara  kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeweka mikakati ya kupambana na changamoto hiyo ya ajira kwa vijana ikiwemo kuimarisha mafunzo ya kazi za Amali nchini.

Mapema mkurugenzi wa idara ya ajira  Ali Suleiman Ameir  amesema  sera  ya ajira ya mwaka 2009 imeweka fursa ya kujadili, changamoto na utendaji wa wadau kuhusuiana na  ajira kwa vijana nchini.

Wakiwasilisha matokeo ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi sita ya mwezi  wa april hadi octoba, 2019 wanakamati wa kuzalisha ajira wa wilaya 3 za mkoa wa mjini magharibi  wamesema zaidi ya ajira elfu sita na mia tano (6500)zimezalishwa katika sekta za serikali na binafsi kipindi hicho.

Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa na idara ya ajira na kuwashirikisha wadau kutoka Wizara za kilimo, Mifugo, Uvuvi, Baraza la vijana, ZSSF, Mazingira.

error: Content is protected !!