Daily Archives: November 14, 2019

MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI WA MAJI SAFI NA SALAMA

 

Mamlaka ya Maji Zanzibar, imekusudia kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa maji safi na salama ili kupunguza upotevu wa maji unaotokana na uchakavu wa miundombinu hiyo katika baadhi ya maeneo.

Meneja wa mradi wa maji wa mamlaka hiyo Nd Maulid Hassan Khamis ameyasema hayo katika ziara ya kamati ya bajeti ya baraza la wawakilishi iliyotembelea ujenzi wa matangi ya maji Saateni na Migombani.

Amesema mamlaka hiyo imepanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni 33 katika ujenzi wa matangi hayo pamoja na kubadilisha mabomba chakavu ambapo itasaidia kupatikana kwa maji safi ndani ya mji wa Zanzibar.

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya baraza la wawakilishi Dk Mohamed Said ameitaka mamlaka hiyo kushirikiana na taasisi nyengine za serikali zinazohusika na uimarishaji wa miundombinu na utoaji huduma kwa wananchi ili kuepusha kero na gharama zisizotarajiwa kwa wananchi na Serikali.

Mradi wa maji safi na salama mjini Zanzibar unajengwa na  kampuni ya Stecol kutoka China kwa kusimamiwa na zawa na unategemewa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu ambapo zaidi ya wakaazi laki tano wa Mji Mkongwe na Ng’ambo watafaidika na mradi huo.

 

WANANCHI PEMBA WATAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO NA MTATHIMINI MKUU WA SEREKALI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mh.  Mohammed Abudu Mohammed amewataka wanachi  ambayo wamo katika utanuzi wa ujenzi wa Kiwanja cha  Ndege kisiwani Pemba  kutoa mashirikiano yapamoja na Mtadhimini mkuu wa Serekali wakati wa kufanya tadhimini kwa nyumba na vipando vyao ili waweze kulipwa fidia kila moja anavyostahiki bila ya kudhulumiwa mtu.

Wito huo ameutoa katika kikao cha pamoja na  Waheshimiwa Mawaziri na wanachi wa waliyofikiwa na utaanuzi wa ujenzi wa kiwanja hicho huko furaha wilaya ya chake chake Pemba.

Mapema Waziri wa ujenzi  mawasilianio na usafirishaji Mh Sira Ubwa Mamboya amesema utanuzi wa ujenzi wa kiwanja hicho  utaendana na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Unguja nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh Hemed Suleiman Abdalla amewataka wanachi hao kuwacha kusikiliza taarifa yoyote isiyo kuwa  rasmi na badala yake kusikiliza tarifa sahihi inaotolewa na Serekali .

 

error: Content is protected !!