Daily Archives: November 13, 2019

MABADILIKO YA UTENDAJI WA KAZI KATIKA SEKTA ZA UMMA

Wizara ya Nchi ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala bora imesema nafasi kubwa ya  kuleta mabadiliko ya utendaji  katika sehemu  za kazi  katika  sekta  za  ummaa   itafanikiwa iwapo  watumishi wenyewe watakuwa tayari  Kubadilia  na  kuacha  mazoea.

Kauli  hiyo imetolewa na Mkurugenzi  idara ya miundo ya taasisi , Utumishi na maslahi ya watumishi kutoka wizara hiyo, Nd. Shaibu Ali wakati akifunga mafunzo ya siku tatu juu  ya  kujenga  kwa  Watumishi  wapya  ambapo amesema dhamira ya Serikali ni kuona Watumishi wanafuata  sheria  za  kazi  na  miongozo  ya  Utumishi  wa  umma.

Mkurugenzi wa chuo cha utawala wa umma ipa dr.mwinyi talib amesema ni vyema kwa watumishi wenyewe kuyafanyia kazi kwa vitendo  mafunzo wanayopatiwa kwa kutoa huduma bora kwa jamii, pamoja na kuwasisitiza viongozi wa taasisi kutekeleza matakwa ya kisheria ya kuwapeleka watumishi wapya katika   mafunzo ili lengo la serikali lifikiwe.

Baadhi  ya  wafanyakazi waliopatiwa  mafunzo  hayo  wameyaelezea  mafunzio  hayo  kuwa  ni  muongozo  muhimu  kwa  waajiriwa  wapya  kwa  wanaingia  kazini  huku  wakijua wajibu  wao.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SERIKALI IMEWEZA KUTUNGA SHERIA ZINAZOWEZA KUTOA ULINZI KWA RAIA NA MALI ZAO

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa umma na utawala bora Mh Haroun Ali Suleiman amesema Serikali imeweza kutunga sheria mbali mbali zinazoweza kutoa ulinzi kwa raia na mali zao kwa kuzingatia kanuni za utawala bora.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa mwisho wa mwaka kwa wahusika wa sekta ya haki jinai juu ya utekelezaji wa kazi zao amesema ni vyema kubainisha na kuyajadili matatizo yanayojitokeza katika sekta hiyo ili kuleta mafanikio katika kutoa na kusimamia haki jinai.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Nd Muumin Khamis Kombo akielezea hali halisi ya utekelezaji wa sekta za haki jinai amefahamisha kuwa matatizo yaliyojitokeza ni njia mojawapo ya kujipima ili kupatikana kwa dira ya mwelekeo wa mafanikio ya mwaka ujao.

 

error: Content is protected !!