Daily Archives: November 12, 2019

JAMII IMETAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO KWA SERIKALI ILI KUZUWIYA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI .

Jamii imetakiwa kutoa mashirikiano ya pamoja na  tasisi za kirai na Serekali  ili kusaidia kuondoa unyanyapa na kupambana na mapukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi Nchi

Wito huo umetolewa Hassani Abdall Said kwa niaba ya ya mratibu wa jumuiya ya kuelimisha athari za dawa za kulevya ukimwi na mimba katika umri mdogo jukamkm,

Huko katika ukumbi wa Asamail Gombani wakati alipokuwa akizunguma na waelimishaji rika wa ukimwi na dawa za kulevya ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kutoa  uwelewa juu ya elimu ya ukimwi na kuondoa unyanyapa kwa watu wanoishi na Virusi vya Ukimwi uliyofadhiliwa na mfuko wa rais wa marekani wakupunguza Virusi vya Ukimwi

Mapema akiwasilisha mada juu ya hali ya ukimwi Zanzibar dr Abdalla Omar Hassani amesema kila mtu kwa nafasi yake anawajibu mkubwa wa kuhakikisaha anazuwia   mapukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Nao baadhi ya washirikia wa hao wamesema  bado ajmii inahitaji elimu ya kutosha ili kuondowa unyanyapaji kwa watu wanaishi na virusi vya ukimwi na  dawa za kulevya .

 

WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE PEMBA WAJUMUIKA KATIKA ZOEZI LA KUPIMA AFYA ZAO .

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadidi Rashid  amejumuika na wafanyakazi wa mamlaka ya Viwanja vya Ndege Pemba katika zoezi la kupima afya zao lililofanywa na madaktari bingwa wa kichina kutoka hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani.

Akifungua zoezi hilo Mkuu huyo wa Wilaya amesema ni muhimu   wafanyakazi wa mamlaka hiyo  kupima afya zao hasa  ukizingatia mazingira ya kazi zao. Ikiwa ni pamoja na kukutana na watu wa aina tofauti, kuendesha mashine mbali mbaliambazo mionzi yake mara nyingi huathiri kiafya  .

Mapema Meneja  Mamlaka ya Viwanja vya ndege Fadhil Juma Ali  amewashukuru madaktari hao kwa uamuzi wao wa kuwafanyia vipimo,  baada ya  kufurahishwa na utoaji wa huduma zao wakati wanapotumia kiwanja hicho .

Nao mmoja wa madaktari hao dk Chuu amesema wameamua kufanya zoezi hilo baada ya kuona  watu wengi huenda Hospitali kuchunguza afya zao katika hatua za mwisho za maradhi na kuwa tayari wameshaathirika.

Baadhi ya wafanyakazi hao Khamis Mgau Kombo na Naima Hamad Bakari wamesema  zoezi hilo limewsaidia kwani mfanyakazi  anapokuwa na afya  huwajibika  ipasavyo

Wafanyakazi hao walichekiwa afya zao kwa kupatiwa vipimo vya maradhi mbali mbali  kama vile homa, presha, moyo , mishipa , koo, masikio  na macho .

 

error: Content is protected !!