Daily Archives: November 11, 2019

SERIKALI INAENDELEA NA JUHUDI ZA KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA KWA WAJASIRIAMALI HASA VIJANA

Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na juhudi za kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa wajasiriamali hasa vijana wanaojishughulisha na kazi mbali mbali kwa kuwatafutia soko la ndani na nje ya nchi.

Balozi Seifa Ali  hotuba yake imesomwa na Naibu waziri wa Wizara ya kazi, uwezeshaji wazee wanawake na watoto mh shadiya  mohamed suleiman  katika ufunguzi wa kongamano la pili la wanawake  chakarika amesema  Idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza masomo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na kusababisha ugumu wa ajira  hivyo Serikali imekuwa ikiwapatia vijana elimu ya ujasirimali na kuwataka vijana hao kutumia fursa zinazotelewa na kuacha kutegemea ajira kutoka Serikalini.

Aidha  amewataka kinamama hao kuacha muhali  pale wanapokamatwa  watuhumiwa wanaowafanyia   vitendo vya udhalilishaji  kuwa mstari wa mbele kujitokeza kutoa ushirikiano   navyombo vya ulinzi  kwa kutoa ushahidi mahakamani  ili wahalifu hao watiwe  hatiani na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria .

Mkuu  wa wilaya ya kusini ndugu Idrisa Mustafa Kitwana  amewaomba vijana kuchangamkia fursa hizo wanazopitapa  za ujasiria mali kwani zimekuwa zikiwapatia ujuzi na tija kwa kujipangia muda wao wenyewe .

Katika risala yao taasisi ya mwanamke chakarika iliyosomwa na   rukia juma wamesema licha ya kupata maendeleo katika tasisi hivyo  bado wanakabiliwa na ukosefu wa ofisi za kudumu na  vifaa vya kufanyia kazi  hivyo wameomba kusaidiwa ili kudidi kufanya kazi. Kuondokana na utegemezi.

 

TIMU YA MAMLAKA YA MANUNUZI YAICHAPA TIMU YA WIZARA YA KILIMO KWA MIKWAJU YA MATUTA 5 -4

 

Timu ya Mamlaka ya Manunuzi imefanikiwa kuichapa timu ya Wizara ya Kilimo kwa mikwaju ya matuta 5 -4 timu ya Wizara ya Kilimo,  mchezo uliopigwa katika kiwanja cha Mao Ze Doung.

Mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute ambapo hadi dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake hali iliyopelekea kuingia katika hatua ya matuta.

Kwa ushindi huo timu ya Mamlaka ya Kilimo inaingia katika mechi ya fainali siku ya jumatatu kuelekea maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika.

 

 

TABIA YA BAADHI YA WANANCHI KUTUPA TAKA OVYO YANACHANGIA UHARIBIFU WA MIONDO MBINU YA BARABARA

Tabia ya baadhi ya wananchi kutupa taka  ovyo na  kulima migomba bila ya kufuata taratibu katika eneo la mto wa mtoni kidatu kunasababisha mafuriko katika eneo hilo wakati wa msimu wa mvua kubwa.

Mhandisi wa barabara Zanzibar Cosmas Masolwa amesema matazo hayo pia yanachangia uharibifu mkubwa wa miondo mbinu ya barabara na makaazi ya wananchi.

Ameeleza hayo katika ziara ya ukaguzi wa barabara pamoja na kuangalia athari za miundombinuya barabara iliyofanywa na bodi ya mfuko wa barabara Zanzibar.

Wakielezea tatizo hilo wakaazi wa Mtoni Kidatu tatizo hilo wameiomba Serikali kuwajengea daraja ili kuepukana na athari za  zinazoweza kutokea.

Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa barabara  Mwalimu Haji Ameir amesema jitihada zinafanyika za kuziba mashimo yaliyojitokeza katika barabara mbalimbali yaliyosababishwa na mvua.

Ziara  hiyoya bodi ya mfuko wa barabara Zanzibar imetembelea barabara ya Bububu kwa nyanya na barabara ya kwa Boko, Kibanda maiti iliyochimbika kutokana na ongezeko la magari baada ya barabara ya Mikunguni kufungwa kutokana na ujenzi wa mtaro unaoendelea.

error: Content is protected !!