Monthly Archives: November 2019

DKT BASHIRU AELEZA AMANI NA UTULIVU ILIYOCHANGIA MAENDELEO YA TAIFA KATIKA NYUMBA ZA IBADA.

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi taifa Dkt .Bashiru Ali kakurwa ameelezea umuhimu wa kuwakumbusha waumini historia ya waasisi wa amani na utulivu iliyochangia maendeleo ya taifa katika nyumba za ibada.

Akizungumza na waumini wa dini ya kiislam wa kijiji cha Tumbatu katika sherehe ya maulid ya kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.) mkakati huo utawajenga waumini kulinda amani ya nchi.

Dkt Bashiru ameiomba jamii kuungana katika kuimarisha maendeleo ya jamii na taifa ili yaweze kuleta manufaa kwa pande zote katika jamii.

Mwakilishi wa Tumbatu Haji  Omar Kheri amesema maulid hayo katika kijiji cha Tumbatu ni sehemu ya utamaduni  unaolenga kuwaunganisha na kuimarisha umoja wao na kujenga uzalendo na utamaduni wa Watumbatu.

ZECO KUHAKIKISHA KUTATUA KERO YA HUDUMA YA UMEME

Shirika la umeme Zanzibar ZECO limesema litahakikisha kutatua kero ya huduma ya umeme mdogo wanaopata wananchi katika maeneo mbalimbali wanaopata wananchi.

Mkuu wa idara ya mawasiliano na huduma kwa jamii ZECO Salum Abdalla Hassan amesema shirika hilo limesha yaorodhesha maeneo yote yenye tatizo hilo likiwemo la Shakani ambalo limeshawekewa tranforma kwa ajili ya kuongeza kiwango cha umeme.

amewaomba wananchi kutumia huduma hiyo kwa umakini na kutoa taarifa mara wanapoona hitilafu.

Baadhi ya wananchi wameishukuru zeco kuwatatulia tatizo la kupata umeme mdogo uliokuwa unawasumbua kufanya shughuli zao za kujiongezea kiuchum

ANGOZA IMEANDAA TAMASHA MAALUM LA KUWASHAJIHISHA WANAWAKE

Mwanvuli wa Asasi za kiraia Zanzibar  ANGOZA  umeandaa  tamasha maalum  lenye  lengo  la  kuwashajihisha  wanawake  kutumia  fursa  ziliomo  katika  uchaguzi  mkuu  wa  mwaka  2020.

Tamko  hilo  limetolewa  na  Mwenyekiti wa ANGOZA  Asha  Aboud ambapo amesema  imebainika  kuwa  bado  kuna  kundi  kubwa  la  wanawake  ambao  wanakosa  kutumia  fursa  ziliopo  katika uchaguzi  kutokana  na  mambo toafuti lakini  zaidi   ni  kukosa  uelewa  wa  namna  ya  kuingia  katika  nyanja  za  uchaguzi .

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari   amesema katika tamasha hilo mada tatu zitawasilishwa ikiwemo uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu ambapo asasi za kiraia na sekta binafsi zitapata nafasi ya kutoa uelewa wao.

Mkurugenzi mtendaji waANGOZA Mw. Hassan Khamis amesema dhamira ya kufanya tamsaha hilo  ni kuutambulisha umma jinsi ya kazi zinazofanywa na angoza katika kuleta  mabadiliko  chanya na  kuleta  maendeleo katika jamii  na Taifa.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili likiwashirikisha washiriki wapatao 130 likiwa na kauli mbiu nafasi ya asasi za kiraia katika kukuza democrasia na maendeleo Zanzibar.

 

UNDP YAIPONGEZA ZANZIBAR KWA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania Christine Musisi wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

 

Katika mazungumzo hayo, Mwakilishi huyo Mkaazi wa (UNDP), alitoa pongezi hizo kwa Rais Dk. Shein na Serikali anayoiongoza kutokana na kasi kubwa ya ukuaji uchumi sambamba na hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa Zanzibar.

 

Mwakilishi huyo Mkaazi wa Umoja wa Mataifa alieleza kuwa Katika kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Shein Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeona mageuzi makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo sambamba na kuimarika kwa utawala Bora.

 

Aliongeza kuwa Shirika la Umoja wa Maifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP) litaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza na kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo ili Zanzibar izidi kupata mafanikio.

 

Aidha, Mwakilishi huyo Mkaazi wa (UNDP), alieleza kuwa katika uongozi wa Rais Dk. Shein Shirika hilo limeweza kushuhudia mafanikio makubwa ya kiimaendeleo ikiwa ni pamoja na juhudi za kupamba na umasikini na kukuza uchumi chini ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA) ukiwemo (MKUZA II) na kuahidi kuuunga mkono (MKUZAIII).

 

Alieleza kuwa huduma za kijamii zimezidi kuimarika zikiwemo huduma za afya, elimu, maji safi na salama pamoja na huduma nyenginezo sambamba na juhudi kubwa zilizofanyika katika kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

 

Hivyo, Kiongozi huyo alieleza kuwa (UNDP), iko tayari kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia vipaumbele vyote vilivyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Nae Rais Dk. Shein kwa upande wake alieleza kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP), ni miongoni mwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) ambalo limekuwa na mashirikiano na kuweza kuiunga mkono Zanzibar kwa muda mrefu.

 

Hivyo, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kulipongeza Shirika hilo na kueleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wake wanafarajika na juhudi kubwa inazozichukua Shirika hilo katika kuhakikisha Zanzibar inazidi kupata mafanikio ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

 

Rais Dk. Shein aliongeza kuwa uchumi wa Zanzibar umezidi kuimarika kutokana na mashirikiano makubwa kati ya uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wake bila ya kuwasahau washirika wa Maendeleo kama vile Shirika hilo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

 

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza juhudi na mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha na kukuza uchumi wake ikiwa ni pamoja na kuiimarisha sekta ya uwekezaji, viwanda sambamba na kuiendeleza na kuiimarisha sekta ya utalii ambayo inachangia kwa asilimia 27 ya Pato la Taifa la Zanzibar na asilimia 80 ya fedha za kigeni.

 

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein alieleza kuwa sekta ya utalii imeweza kuimarika kwa kiasi kikubwa ambapo pia, juhudi za makusudi zinaendelea kuchukuliwa katika kuiendeleza sekta hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hoteli kubwa za kitalii pamoja na kuviimarisha vivutio vlivyopo.

 

Kwa upande wa uwekezaji, Rais Dk. Shein alimueleza Mwakilsihi Mkaazi huyo wa (UNDP) kuwa Mamlaka ya Ukuzaji wa Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), imekuwa ikifanya kazi kubwa katika kuhakikisha maeneo huru ya Uchumi yanaimarika na yanafikia yale malengo yaliyowekwa ambapo kwa upande wa Unguja alieleza kuwa eneo la Fumba tayari limeanza kutumika kiuwekezaji huku juhudi zikichukuliwa kwa upande wa eneo la Micheweni huko Pemba.

 

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein alieleza kuwa huduma za  kijamii zimezidi kuimarika na miradi yote ya maendeleo imeendelea kupata mafanikio na kueleza kuwa huduma za afya kwa upande wa kupunguza vifo vya akina mama na watoto vimepungua kwa kiasi kikubwa.

 

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alisema kuwa juhudi za makusudi zinaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha Zanzibar inatekeleza azma ya Uchumi Bahari (Blue Economy), ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanda vidogo vidogo, kukuza sekta ya utalii, uvuvi pamoja na sekta nyenginezo.

error: Content is protected !!