Monthly Archives: October 2019

ZANZIBAR KUJIFUNZA KOTOKA NCHI ZILIZOFANIKIWA NA UWEPO WA NISHATI YA MAFUTA NA GESI

Zanzibar ikiwa imo katika mchakato wa utafutaji wa nishati ya mafuta na gesi inatakiwa kujipanga kwa kujifunza na kuandaa wataalamu  kupitia nchi ambazo tayari zimefanikiwa na uwepo wa nishati hizo.

Akitoa ufafanuzi wakati wa uwasilishaji mada ya faida na changamoto zitokanazo na uwepo wa   mafuta na gesi nchi mwalimu wa chuo kikuu Dar-es-salaam Profesa Evelyn Mbende ameeleza kuwa ni vyema zanzibar ikaweka mikakati maalum juu ya swala hili kwa lengo la kuendelea kuilinda amani iliopo baada ya upatikanaji wa nishati hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi zanzibar (ZATUC)  Khamis Mwinyi Mohammed amesema kuwepo kwa sera maalum ya kuwalinda wafanyakazi ambao watakuwepo kwenyemchakato huo wa utafutaji wa mafuta na gesi kutaepusaha migogoro kati ya waajiri na waajiriwa

Wakizungumza kwa niaba ya taasisi zao wajumbe waliopatiwa mafuzo hayo  kwa  upande wa wizara ya kazi uwezesahaji wazee wanawake na wtoto wameelezea mikakati ambayo wamejiwekea wakati wa upatikani wa nishati hiyo hapa nchini

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliondaliwa na shirikisho la vyama vya wafanyakazi zanzibar ZATUC  na  shirikr la fes  la amrkani amabayo imewashirikisha wajumbe kutoka tasisi malimbali iliwemo za serikali na binafsi

CUBA ITAENDELEZA USHIRIKIANO NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Cuba imesema itaendeleza ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta ya kilimo na utalii ili kuimarisha uchu

Wajumbe kutoka cuba wameeleza hayo walipokuwa na mazungumzo na viongozi wa wizara ya habari utalii na mambo ya kale katika ukumbi wa wizara ya habari.

Wamesema pia watabadilishana uzoefu na kupeana elimu kuhusu sekta hizo ili kuzifanya endelevu na zenye tija kwa mataifa hayo mi wa nchi mbili hizo.

Katibu mkuu wizara ya habari utalii na mambo ya Kalebi Khadija Bakari amesema sekta ya utalii inazidi kuimarika hivyo   watatoa mafunzo ambayo yatasaidia kukua zaidi kwa sekta hizo.

Mkurugenzi wa shirika la utangazaji zanzibar Chande Omari   na katibu mtendaji wa kamisheni ya utalii ndug Abdala Muhamed wamesema kufutia ujio wa ujumbe huo  watatayarisha vipindi ambavyo vitatoa elimu kwa jamii kujua umuhimu wa sekta ya utalii nchini

error: Content is protected !!