Daily Archives: October 29, 2019

TIMU YA SKULI YA SOS IMETWAA KOMBE TUMBATU WALIBEBA KOMBE LA MCHEZO WA NAGE

Timu ya skuli ya sos imetwaa kombe la bonaza la michezo la kuibua vipaji na kuimarisha mashirikiano na jamii viliopo jirani na kijiji hicho baada ya kushinda kwa penant 7 – 6 timu ya skuli ya tumbatu jongowe .
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye kiwanja cha sos mombasa hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa nguvu sawa baada ya kushindwa kutambiana.
Ushindi wa sos ulipatikana baada ya mchezaji wa jongowe shuti lake kugonga mwamba wa pembeni na mpira kurudi uwanjani.
Katika bonaza hilo tumbatu walibeba kombe la ubingwa katika mchezo wa nage kwa kushinda chupa 7 – 3 dhidi ya sos.
Keptain wa timu hizo alisema mchezo ulikuwa mzuri…

Mchezo ya awali ilikuwa sos valicheza na kisauni katika mchezo wa nusu fainali na tumbatu jongowe walikipiga na sos villeg.
Michezo mingine iliyokuwa kivutio kiwanjani hapo ilikuwa ni riadha wadogo na wakubwa.
Akizungumzia michezo hiyo kwa niaba ya uongozi wa kijiji cha sos mratibu wa malezi mbadala nyezuma simai amesema michezo hiyo imebeba ujumbe wa mlindemtotona umpatie fursa sawa za elimu unaolenga mashirikiano.
Katibu mtendaji wa baraza la vijana khamis faraji mgeni rasmi katika bonaza hilo amesisitiza umuhimu wa michezo na fursa kwa vijana ambao wanahitaji kuandaliwa mapena na vipaji vikaendelezwa.

MAAFISA WENYE DHAMANA YA KUSIMAMIA MANUNUZI WAMETAKIWA KUUSIMAMIA SHUGHULI ZAO KWA KUZINGATIA SHERIA

Maafisa wenye dhamana ya kusimamia manunuzi wametakiwa kuusimamia shughuli zao kwa kuzingatia sheria na maadili ya kazi ili kuhakikisha fedha za serikali zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Hayo yamesemwa na katibu Tawala Mkoa wa Kusini Pemba Abdallah Rashid Abdallah kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, katika mafunzo ya sheria ya ununuzi na uondoaji wa mali za umma, sheria namba 11 ya mwaka 2016, kwa Maafisa masuuli na madiwani kisiwani pemba.
Akiwasilisha mada ya sheria hiyo, mkufunzi kutoka mamlaka ya Ununuzi na uondoshaji wa Mali za Umma, mohamed khamis said amesema maafisa wanapaswa kufanya manunuzi kutoka kampuni zilizosajiliwa na mamlaka yenye dhamana, ili kuepusha matatizo yasiyo ya lazima
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameiomba mamlaka hiyo kuimarisha mashirikiano baina ya maafisa manunuzi na maafisa mipango katika taasisi za serikali ili kuleta ufanisi katika utendaji wao.

TIMU YA MPIRA WA PETE YA WILAYA YA MAGHARIBI B IMEFANIKIWA KUIBUKA NA USHINDI WA MABAO 34-28

Timu ya mpira wa pete ya wilaya ya magharibi b imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 34-28 dhidi ya wenyeji wao timu nungwi mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa nungwi.
Katika mchezo huo magharibi b walionekana kuutawala mchezo licha ya timu ya nungwi kuwepo nyumbani kwao ambapo mgeni rasmi katika mchezo huo mkurugenzi msaidiz masuala ya mtambuka abdul hakim machano amezitaka timu zote mbili kuendelea mashirikiano pamoja na kushiriki michezo kwani michezo ni fursa ya ajira.

error: Content is protected !!