Daily Archives: October 25, 2019

BALOZI SEIF KUWASHAWISHI WAWEKEZAJI KUJA NCHINI KUANZISHA VIWANDA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIiddi amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya ya kuwashawishi wawekezaji wengi kuja nchini kuanzisha viwanda ili kufanikisha dhamira ya serikali ya kuwa na uchumi bora unaotegemea viwanda.

Balozi Seif ametowa tamko hilo katika  hafla ya uzinduzi wa vitabu vitano vya wizara ya biashara na viwandauliofanyika katika ukumbi wa Idrissa Abdul wakil  kikwajuni.

Balozi seif ameeleza kuwa vitabu hivyo vitatumika katika kuwasaidia walengwa kupata taarifa kwa urahisi kuhusiana na biashara, viwanda na kuleta mabadiliko ikiwemo ya kuondosha urasimu katika ufanyaji biashara na utoaji leseni.

Ameongeza kuwa vitabu hivyo pia vitasaidia kutambua viwanda vya kimkakati, kujuwa hatua za kupita wakati wa uingizaji na usafirishaji wa bidhaa nchini, pamoja na kuelewa bidhaa zinazotarajiwa kuuzwa katiak soko la agoa pamoja na kufikia malengo ya utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2020 na mkuza na tatu.

Waziri wa biashara na viwanda  balozi amina salum ali amesema sera mpya ya viwanda ya miaka kumi ijayo inahakikisha mabadiliko katika suala la biashara na viwanda kwani utayarishaji wake umezingatia malengo ya serikali ya kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji wa biashara.

Mwakilishi wa shirika la umoja wa mataifa linalosimamia  viwanda {unido} bwana stephen  na mwakilishi wa balozi wa sweeden nchini tanzania bibi jane akebak wamesema mafanikio makubwa ya uimarishaji wa sekta ya viwanda utafanikiwa vyema endapo sera   zitaimarishwa na kutekelezwa  kwa uwazi.

Akizungumza kwa niaba ya sekta binafsi nd. Hamad hamad kutoka jumuiya ya wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima amesema wanaimani kubwa juu utekelezaji wa sera hiyo mpya jambo ambalo litasaidia kuinua nchi na  kuiweka katika nafasi nzuri ya ushindani wa kibiashara kwa nchi zinazoendelea.

 

 

 

error: Content is protected !!