Daily Archives: October 18, 2019

ZANZIBAR INAWEZA KUPIGA HATUA KUBWA ZA KIMAENDELEO KATIKA TEKNOLOJIA YA HABARI

Zanzibar inaweza kupiga hatua  kubwa  za  kimaendeleo katika  sekta  tofauti   iwapo teknolojia  ya  habari  na  mawasiliano  itaimarishwa  na kutumika  ipasavyo  katika kuongeza  kasi  ya  utendaji  wa  kaz katika  sekta  mbnali  mbali .

Mkururugenzi  Mtendaji  mamlaka  ya mafunzo ya  amali nd. Bakari  Ali  Silima ametoa  kauli  hiyo wakati akifungua  mafunzo ya matumizi ya teknolojia mpya ya mawasiliano   ambayo  imeshaaza kutumika katika nchi mbali mbali za ulaya  inayoweza kutumika  katika masuala tofauti  ikiwemo  usalama,  kilimo  , uvuvi  na  elimu.

Mkuu wa skuli   elimu endelezi   na utalaamu dk Haji Ali Haji amesema mafunzo hayo yataweza kuwasaidia wanafunzi kuweza kuingia   kutumia   ngazi  nyengine  ya juu ya  teknolojia  itakayotoa fursa  ya  kuongeza  kasi  katika kutambua  mambo  yanayomzunguka  pamoja  na  kujiajiri.

Washiriki  wa  mafunzo  hayo  wamesema kuja kwa teknolojia hiyo hapa nchini  kurahisisha baadhi ya shughuli ambazo mwanadamu anatakiwa kuzifanya kwa kila siku kuwa  nyepesi  na kuongeza fursa  za  ajira.

Mafunzo hayo yanatolewa na mkufunzi kutoka chuo cha teknolojia cha denmark na yamewashirikisha wanafunzi wa  vyuo  shiriki  vilivyo  chini  ya  chuo kikuu  cha  taifa  SUZA

 

WAGONJWA MILIONI SABA WAMEPATIWA HUDUMA ZA MATIBABU YA MARADHI VISIWANI ZANZIBAR

Zaidi ya wagonjwa  milioni saba wamepatiwa huduma za matibabu ya maradhi mbali mbali kutoka timu ya madaktari wa china visiwani Zanzibar katika kipindi cha miaka 55 tangu walipoanza kuisaidia Zanzibar mwaka 1964

Mkurugenzi wa timu ya madaktari wa china nd. Yang Xiaodong  amesema kwa kushirikiana na wizara ya afya ya Zanzibar wamefanikiwa kutoa huduma hizo jambo ambalo limesaidia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Amesema katika kipindi hicho wamefanikiwa kuanzisha vituo na mifumo mbali mbali yenye lengo la kurahisisha hudumam za matibabu visiwani Zanzibar.

Daktari wa tiba vitobo “accupuncture” nd. Zhou Han amesifu mashirikiano wanayopata kutoka kwa madaktari wazawa jambo ambalo linawasaidia katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Wakizungumzia ubora wa huduma wanazopata kutoka kwa madaktari wa kichina wagonjwa wa hospitali ya mnazi mmoja wamesema madaktari hao wamekua msaada mkubwa katika kutatua matatizo ya kiafya kwa wagonjwa wanaofika spitalini hapo.

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!