Daily Archives: October 17, 2019

UMEFIKA WAKATI KWA VIJANA KUJIKITA ZAIDI KATIKA SHUGHULI ZA UJASIRIAMALI

Umefika wakati kwa vijana kujikita zaidi katika shughuli za ujasiriamali ili kuweza kutimiza malengo yao ikiwa pamoja na kujikimu kimaisha na kuachana na utegemezi wa ajira kutoka serikali kuu.

Akitoa taaluma kwa vijana wa magharibi A muwezeshaji kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na idara maalum za SMZ Bi ZAINAB kibwana ili kuweza kuzitumia fursa zilizopo ndani ya shehia zao kupitia dhana nzima ya ugatuzi katik kuangalia bajet ya maendeleo za manispaa kwa ajili ya kuwawezesha wakaazi wake kiuchumi.

Amesisitiza vijana kuzitambua nafasi zao ktk halmashauri zao ili kuweza kuzitumia vyema asilimia 5 za ruzuku zinazotolewa kwa vikundi vya ushirika ili kuwa na vyanzo vya mitaji itayowatoa ktk utegemezi.

Nao vijana hao wameiomba serikali kupitia wizara kilimo na idara uwezeshaji kuwapatia taaluma zaidi ya shughuli zao za mikono ili kuweza  kuwapatia tija na kuepukana na malalamiko ya ukosefu wa ajira.

Mratibu wa mradi huo wa uibuaji wa fursa za maendeleo kwa vijana nd Mbarouk Said amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha vijana kuzitambua fursa zilizopo ikiwa pamoja na kujua bajet iliopo ktk manispaa zao zinawasaidiaje ktk kuwajengea uwezo wa kujiajiri wenyewe.

WAFANYAKAZI WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA UFANISI

Wafanyakazi wa wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto kisiwani pemba, wametakiwa kutimiza majukumu yao  ili kuleta ufanisi katika wizara hiyo.

katika kikao cha kawaida na wafanyakazi wa wizara hiyo,chenye lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wafanyakazi hao,kilichofanyika katika ukumbi wa wizara hiyo gombani chakechake pemba.

Mdhamini Shein amesema kuwa mafanikio  katika kazi  ni jambo linalotegemea  utendaji bora kwa  kila mtu katika nafasi yake,na iwapo kila mmoja atatimiza majukumu yake, basi maendeleo makubwa yatapatikana katika wizara hiyo,

Pia amewataka wafanyakazi hao kuweka wazi changamoto  wanazokumbana nazo  katika kutimiza majukumu yao ya kila siku ili zipate kutatuliwa , na kuondosha  uwezekano wa changamoto  hizo  kusababisha  matatizo makubwa zaidi.

Nae afisa utumishi wa wizara hiyo, Yusuf Mselem Khamis  amewataka wafanyakazi hao  kufika katika ofisi ya mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF mara kwa mara  ilikuhakikisha michango yao  inawasilishwa  ipasavyo  kwa maslahi yao ya baadae.

Kwa upande wa wafanyakazi hao  wamemuombaofisa mdhamini huyo  kuunda kamati ya ushauri  itakayoweza kutatua  changamoto ndogondogo  za kikazi ili  kuwafanya waweze kutimiza majukumu yao kama inavyotakiwa.

ZANZIBAR INAWEZA KUWA NA KIWANGO BORA CHA UFAULU KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE

Zanzibar  inaweza  kuwa  na  kiwango  bora cha  ufaulu  katika  mitihani  ya  kidato  cha  nne  iwapo wanafunzi  wenyewe  watajitambua  na  kuweka  mkazo  katika  kusoma  badala  ya  kjiingiza  katika mambo  mengne.

Kauli  hiyo  imetolewa  na  mkuu  wa  wilaya  ya  mjini  Mh. Marina Joel  Thomas  wakati akitoa nasaha kwa wanafunzi wa kidato cha nne wa skuli za wilaya mjini wanaotarajiwa kufanya mitihani ya taifa hivi kuanzia hivi karibuni mkutano  ulofanyika skuli  ya  ben  bella.

Amesema ni vyema wanafunzi hao wakajikita zaidi katika masomo yao katika kipindi hiki kifupi kilichobakia ili  kujiepusha na  udanganyifu katika mitihani yao na  kuwasisitiza  kufahamu  kuwa  elimu  ndio  ufunguo  wa  maisha yao  ya  baadae .

Msaidizi mkurugenzi wa  elimu manispaa ya mjini Bibi  Kibibi Mohammed Mabrouk amesema  kuwa  wilaya ya mjini  ina  jumla  ya  wanafunzi  5,501 wanaotarajia  kufanya  mtihani  wa  taifa   ambapo    wanaume  ni  1,981  na   wanawake  3,524 .

Baadhi  ya  wanafunzi wakaeleza  kufarijika  na  nasaha  za  mkuu wa wilaya  ya  mjini na kuahidi kufanya mitihani yao  kwa  uadilifu  na  kujiamini   na  kukwepa udanganyifu ili  kuongeza nafasi  za  ufauli  kwa  skuli  za  wilaya  ya  mjini.

error: Content is protected !!