Daily Archives: October 16, 2019

WIZARA YA ELIMU KUTHAMINI JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SKULI BINAFSI KATIKA KULETA MAENDELEO

Wizara  ya elimu  na mafunzo ya amali  imesema itaendelea Kuthamini  juhudi  na kutambua michango  inayotolewa na skuli binafsi katika kuwakuza watoto na  maendeleo  ya  sekta  hiyo.

Naibu waziri wa wizara hiyo Mh Simai  Mohd Said akizungumza katika mahaafali  ya 20 ya skuli ya stone town  Intrenational iliopo  migombani   yaliyohusisha wanafunzi wa kidato cha nne,, darasa la sita na  maandalizi amesema  kutokana na mchango huo  serikali kupitia wizara  hiyo   itaendelea kuunga  mkono  na   kuzipatia usajili  skuli  binafsi na kuzitaka  kufuata miongozo  inayotolewa  na  wizara.

Amesema elimu ni haki ya msingi ya  kila mtoto  hivyo  ni vyema wazazi na walezi kushirikiana katika kumlea mtoto katika misingi iliyo  bora pamoja na kutoa wito kwa madereva  kuonesha  upendo  kwa  wanafunzi  wapopanda  gari  kwenda  na  wanaporudi  skuli.

Mwalimu mkuu wa skuli  hiyo Jamila Jaffar Gulam amesema skuli  hiyo imeandaa  mapango  maalum  wa  kuhakikisha  wanainua  viwango  vya  ufaulu  kila  mwaka   na  kuotoa  tai kwa wazazi  kuunga  mkono  juhudi  hiyo

Baadhi  ya walimu,  wazazi na wanafunzi  wameelezea matarajio yao sambamba na kuwataka wazazi  wenzao kuchangia maendeleo ya skuli

TAIFA LAFIKIA UZALISHAJI WA CHAKULA KWA ASILIMIA 60%

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati taifa limepiga hatua kubwa  katika uzalishaji wa chakula cha kutosha na kufikia asilimia 60% na ile asilimia 40% iliyobakia  huagizwa nje ya nchi, jamii sasa inapaswa kubadilisha tabia na kurudi kwenye ulaji wa vyakula vya asili ili kujenga afya bora.

Amesema takwimu zinaonyesha wazi kuwa mnamo mwaka 2010 taifa lilikuwa likizalisha chakula kwa asilimia 46% tu na kuagiza chakula nje ya nchi kwa asilimia 54%  jambo ambalo linathibitisha kuongezeka kwa asilimia 6%  sasa  ya uzalishaji huo.

Wakati akiyafunga rasmi maonyesho ya siku ya chakula duniani { world food day} yaliyokuwa yakifanyika takriban kwa wiki moja sasa  katika kijiji cha chamanangwe jimbo la kojani mkoa wa kaskazini pemba.

Amesema jamii inapaswa kufuata taratibu zote za lishe bora na kutoa elimu hiyo kwa kuimarisha afya zao ili waweze kujiepusha na maradhi  mbali mbali hususan yale yasiyoambukiza ambayo kipindi hichi yamekuwa tishio kubwa katika maisha ya kawaida na hatimae kuathiri nguvu kazi za taifa.

Balozi Seif amebainisha kwamba mazao ya kilimo yapo mengi hapa nchini na wakati mwengine kilo moja ya tungule hufikia kuuzwa shilingi mia mbili bei ambayo ni bora zikasindikwa  na kusarifiwa ili kupata bidhaa bora isiyo na chembe chembe za kemikali itayokuwa na uhakika wa kuimarisha afya za wananchi.

Akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wananchi walioshiriki maonyesho hayo naibu waziri wa kilimo, maliasini, mifugo na uvuvi Dr. Makame Ali Ussi amesema muelekeo wa kilimo ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula ikiwa ndio lengo kuu la swerikali.

Katika hafla hiyo makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar alitoa zawadi na vyeti kwa washiriki waliofanikiwa kushinda mashindano yaliyofanywa na wizara ya kilimo katika mulekeo wa kuhamasisha wajasirili amali kushiriki kila mwaka kwenye maonyesho yanayoandaliwa na wizara hiyo

SMZ YASHIRIKIANA NA SERIKALI YA WATU WA CHINA KUTOKOMEZA UGONJWA WA KICHOCHO

Waziri wa afya Mhe: Hamad Rashid Mohammed amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na serikali ya watu wa China imekuwa ikishirikiana katika kutokomeza ugonjwa wa kichocho nchini usiendelee kuathiri zaidi wananchi.

Mh. Hamad amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na walimu wakuu wa skuli za msingi kisiwani pemba katika uzinduzi wa mashindano ya uandishi wa vipeperushi kwa wanafunzi wa skuli za msingi katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo wawi.

Amesema ili mradi huo uweze kufanikiwa imeonekana  kuwa njia moja wapo ni kuwashirisha watoto  kwani wao wanauwezo wa kukamata ujumbe na kuufikisha kwa jamii kwa haraka hivyo walimu hawana budi kuwasimamia ili kufanikisha vizuri kazi hio.

Akielezea njia za maambukizi za maradhi hayo meneja mradi wa kichocho pemba Saleh Juma Mohammed amesema.

Kwa upande wake mtaalamu wa magonjwa ya kichocho kutoka China Hi Jian akitoa muongozo wa uandishi wa vipeperushi hivyo amesema watoto wanaweza kuandika ujumbe wowote ambao utaelezea athari za ugonjwa huo au njia za kujikinga ili kupima ni namna gani wanaulelewa juu ya ugonjwa huo.

Lengo la mashindano  hayo ni kupima uwelewa ili kuona ni kwa  kiasi gani watoto wanafahamu athari za ugonjwa huo na kuweza kubadili tabia hatarishi zinazosababisha maambukizi ya ugonjwa   wa kichocho.

 

error: Content is protected !!